Magufui njoo CMA, ucheleweshwaji wa Kesi za Ajira ni tatizo

Hamnipati

New Member
Jan 21, 2014
4
4
Rais Magufuli amekerwa na mahakimu ambao wanachelewesha kesi na kukosesha haki isitoke mapema.

Lakini Rais inaelekea hajaelezwa ukweli wote wa sekta hii na kibaya zaidi hakuwahi kufanya kazi katika sekta ya Kazi na Ajira na inawezekana hana picha kamili.

Kinachotokea kwa mahakimu ndiho kilkile kinachotokea kwenye kesi za ajira pale Tume ya Usuluhishi na Uamuzi yaani CMA.

CMA ilipoanza kesi za ajira zilikuwa hazimalizi hata miezi sita. Lakini ssa hivi CMA pameanza kupoteza matumaini kwani kesi sasa zinamaliza hata miaka miwili kwa sababu ambazo hazina mashiko kabisa.

Unashitukia kwamba malamikiwa hakuja na shahidi halafu eti kesi inaahirishwa, tena ikiahirishwa si chini ya mwezi. Watu wa CMA wanaoitwa "Mediator" au "arbitrator" haaoni shida yoyote kuahirisha, tena kuna siku tulishuhudia mtu unaingia tu unakuta anajitayarisha kuiahirisha, tena jamaa hana wasiwasi.

Hii imefanya CMA pawe na mrundikano wa kesi na ukienda pale kwenye saa nne asubuhi utakuta pamejazana sawa tu na Muhimbili ambako Magufuli anaenda kila mara.

Pale CMA kwenye jengo la "Simba Building" lililoko kwenye makutano ya barabara ya Morogoro na Bibi Titi, imefika mahala ukiambiwa kesi yako fika saa 04:00 asubuhi na ukafika kamili muda huo, ukifungua mlango unatarajia kumuona "arbitrator" anakusubiri kuanza kesi.

Lakini kwa wingi wa mrundikano wa kesi, badala ya kuingia moja kwa moja kwa sababu muda ni ule uliandikiwa kwenye summons, unakuta bado kuna watu ama wanafanya kesi (mediation au arbitration).

Sasa inapotokea hivyo, huku nje hamjui sasa msubiri kwa muda gani nampo wengi. Vurugu ni pale wanaotoka wale waliokuwemo, utadhani wewe wa saa 04:00 utaitwa kama tunavyoitwa wagonjwa hospitali. Si hivyo, eti kinachotokea ni mjanja kuwahi na kuingia na kukaa kwa mheshimiwa.

Ukiachilia mbali matatizo ya kupigwa joto wakati hakuna AC na hata wamuzi wenyewe kuvuja jasho, tabia hizi mbili za pale CMA ni kikwazo kikubwa, kwani kadiri unavyosota na kesi yako pale CMA basi mwajiri ndivyo anavyovimba kichwa na kuwakomesha waajiriwa wengine kwani wanaona jinsi unavyosota na CMA na hivyo wanaogopa.

Mwaka jana wakati wa Mei Mosi, Mgaya wa TUCTA alisema wazi tena magazetini kwamba CMA pananuka rushwa na uchunguzi ufanyike. Sasa sijui uchunguzi unafanyika kweli au la,au sasa hasira za wafanyakazi wa CMA zimegeuka katika sasa wacheleweshe kesi ingawa ni kweli mwishoni unaweza kuipata.

Siku moja hukumu ya jamaa japo alishinda ilichelewa eti kwa sababu CMA hawakuwa na orinter na ikaahirishwa kwa zaidi ya wiki. Siku nyingine hakukuwa na sababu anawaambia njoo kesho

Hivyo, Rais Magufuli afanye kama Muhimbili. Siku moja aende pale CMA, siyo lile jengo ma Headquarter, bali lile la pembeni yake liitwalo SIMBA, na akute watu wamejazana pale awauize sababu za kujazana na awaulize kwa nini kesi zao zimechelewa. Ukweli sababu ni kama nilivyoeleza na wengine mtaongezeamliokwishapata matatizo hayo.

Kama Rais kataarifiwa kwamba kuna mahakimu wameshindwa kufikisha kesi 200 kwa mwaka, kwani hata CMA kusiwe na kiwango kwamba "arbitrator" awe na kesi kadhaa kwa mwaka na asipofikisha atumbuliwe jiu kwa sababu anachelewesha haki.

Hivyo, CMA ni jipu linalostahili kutumbuliwa kama mtakavyoeleza wengie humu.

Mchangiaji.
 
Watanzania bwana, tumefikia hatua kila kitu ni Magufuli, na mnamwambia akatumbue, mbona hamdhauri Rais akatatue kero za kiutendaji na kiutawala pale CMA?
CMA wanafanya kazi katika maxingira magumu sana, kwanza pesa hawana, wanaishi kimungu mungu tu
 
CMA haina watumishi wa kutosha hasa wale wasaidizi, NJOMBE kwa mfano, Mumuzi msuluhishi ndo karani, mfagizi, mhudumu, mfungua kesi, msuluhishi na Muamuzi, hivi unategemea performance hapo? Kwa mshahara ule ule bila motisha??
 
Rais nenda pale c kwa kutumbua, bali kuwajengea uwezo wale vijana, matokeo yataonekana!! Wape fedha za kutosha, wape vitendea kazi, wAPE MOTISHA, budget yao ikipita itoke kwa wakati na waachwe huru km sheria inavyotaka!! Wapewe ofisi zao nje ya idara ya kazi, wapewe salary scale yao, na wapewe rent , professional atire allowances, nk kisha baada ya hapo matokeo yasipoonekana ndipo president akawatumbue
 
Mtu hapewi motisha ndipo afanye kazi ILA anapewa motisha baada ya kufanya kazi tena yenye viwango vya kuridhisha.
Sasa CMA mnataka yooote hayo wakati matokeo ya kazi mnazofanya hatuyaoni.!!?
Pigeni kazi,hudumieni watu na watu wenyewe watakiri kuwa kwa kazi mnayowafanyia mnastahili motisha.
 
Watanzania bwana, tumefikia hatua kila kitu ni Magufuli, na mnamwambia akatumbue, mbona hamdhauri Rais akatatue kero za kiutendaji na kiutawala pale CMA?
CMA wanafanya kazi katika maxingira magumu sana, kwanza pesa hawana, wanaishi kimungu mungu tu


Kumbe na wewe mtanzania bbwana
 
Yupo jamaa yangu alikuwa na kesi CMA Dodoma. Arbitrator akaficha ushahidi wake makusudi baada ya kuona atamshinda mwajiri wake. Inasemekana mwajiri alimpa fedha nyingi huyo Arbitrator ili aivuruge kesi. Jamaa yangu akashindwa kesi. Alipokata rufaa High Court (Labour Division), wakati wakili wa jamaa anafanya perusal, akakuta lundo la documentary eveidences alizowasilisha halipo kwenye faili. Kesi ilipoanza akamwambia Jaji. Jaji alikasirika sana, akamwita Arbitrator atoe maelezo ya wapi zilipo nyaraka za ushahidi wa Mlalamikaji. Jamaa kwa aibu akajifanya eti alizisahau ofisini kwake. Akapewa amri azilete, akazileta. Jaji alipochunguza proceedings akakuta nazo zimechakachuliwa. Tendering ya evidences kwenye proceedings haikuwa imefanyika kwa mujibu wa utaratibu wa kisheria. Jaji akalazimika kuifuta hukumu ya Arbitrator pamoja na record ya procedings zote (Trial Denovo). Kwahiyo shauri limeanza upya chini ya Arbitrator mwingine hapa Dar.

Baadhi ya hawa jamaa ni majipu makubwa kabisa. Wanapotezea watu muda na haki zao kwa sababu ya rushwa.
 
Back
Top Bottom