Zak Malang
JF-Expert Member
- Dec 30, 2008
- 5,404
- 234
Jamani eeeeh!
Kama tunavyoshuhudia suala la ufisadi ndani ya CCM na serikali yake linashika moto kwa kasi sana huku vigogo wao kadha wa chama hicho wanajitokeza na kuzidi kulimwagia mafuta.
Kwa maana nyingine huenda imewadia wakati wa kuonyeshana vidole wenyewe kwa wenyewe. Jee kwa mwenendo huu, si dhahiri kwamba sasa hivi ni bora hicho kifanyike?
Maana sasa hivi imekuwa kurushiana ngumi kijuu juu yule dogo Nape anarusha makonde kwa adui zake ambao hataki, hana ubavu wa kuwataja kwa majina. Ni unafiki tu kama alivyosema kada mmoja wa CCM Amb Peter Ndobho.
Mimi naona ni bora sasa mafisadi wakatajana majina bila kujificha, pengine hii ndiyo njia itakayomaliza mambo yote.
Kwa mfano imefikia wakati wale wanaoonyeshewa kidole katika ufisadi wa Kagoda nao wataje wahusika wengine maana Kagoda haikuwa hao tu wanaonyeshewa kidole. Kwa mfano RA ataje wahusika wengine.
Vivyo hivyo kwa rada. Chenge hakuwa peke yake. Asiogope kuwataja akina Mkapa, JK, Dr Rashid na wengine bila shaka. Tukija Richmond nayo hivyo hivyo.
Tumeshuhudia kwa mbali jinsi Jeetu Patel alivyojaribu kupeleka ujumbe kwa wananchi kupitia kwa wakili wake Mabere Marando kwamba hakuwa peke yake katika dili ile ya EPA ambayo anashangaa kwa nini arudishe fedha alizochota EPA huku kiasi kikubwa kilichukuliwa na CCM.
Kama tunavyofahamu Jeetu ana kesi kwa sababu hakurudisha fedha za EPA na hivyo sasa anaona na lolote na liwe. Sidhani iwapo wengi wetu walimuelewa Marando wakati wa ufunguzi wa kampeni pale jangwani mwishoni wa Agosti mwaka jana.
Sasa basi kabla ya kufika huko, nadhani ni wakati muafaka sasa mafisadi wakaanza kusema ukweli kuhusu walivyofisidi, washirika wao walikuwa akina nani etc etc.