Hukumu ya Rais kwa TTCL haijakaa sawa kabisa

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,111
18,327
Juzi wakati Rais anapokea Report ya CAG, alitamka mambo mengi kwa hasira na jazba sana hadi wengine wanaona hakuwa sahihi.

Kwa cheo alicho nacho na maana ya report ya CAG hakutakiwa kutoa hukumu wakati ule kwa sababu report ya CAG ina utaratibu wake kwa serikali kuifanyia kazi.

Ndio maana lazima iende bungeni ijadiliwe, kamati za bunge zijiridhishe na zitoe maamuzi kwa serikali kuyafanyia kazi.

Maneno kama stupid, pumbavu hayakutakiwa kutoka kwa Mh. Rais, kwa sababu kwa maneno hayo inaonekana kuna mambo yamemshinda sasa kilicho baki ni kutumia maneno yasiyo na staa kama kuwaadhibu wahusika.

Achana na hayo, Rais pia alitoa hukumu kwamba TTCL wameshindwa kujiendesha hivyo waache biashara.

Kama Rais alitakiwa asubiri bunge lipitie report na litoe maazimi sometimes CAG anakurupuka na kuandika mambo ambayo hata hayapo ila tuu kwa uvivu wake hakupata vielelelezo vya kutosha.

Pili akisema namna hii ni mishirika mangapi anayayaambia yaache kufanya shughli zao za kibiashara?

Ukiangalia report ya CAG ilivyo na mbwembwe hata ikulu itatakiwa ufungwe kabisa.

Swali la kujiuliza, aliye feli ni Rais na serikali yake au TTCL? TTCL inahitaji utashi wa kibiashara.. Kama TTCL inajiendesha katika mazingira yanayo fanana na DAWASA je watashindana na Tigo au voda?

Mbona Moroco telecoms inapeta, mbona france telecoms inapeta? Tatizo la Tz ni nini?

Viongozi wasijizime data kuihukumu TTCL kana kwamba ni kitu cha mbali kisicho wahusu? Kuna watanzania wengi sana wenye uwezo wa kuibadirisha TTCL ikawa kampuni ya faida?

ATCL au TTCL kushindwa kupata faida Rais naye anahusika kwa sababu yeye ndio anahusika na uteuzi wa Viongozi? Kwanini CEO wasifuate mfumo wa uwazi kuwapata? Kazi itangazwe, na interview zifanyike kupitia mashirika maalumu yenye ujuzi katika kupata viongozi.

Mfano, CEO wa TTCL amemtoa kwenye shirika ambalo halifanyi biashara, na hajawahi kuwa CEO wa kampuni ya biashara katika mazingira ya ushindani? Je, unadhani TTCL itajiendesha vipi? Mtu kama Kindama kuwa CEO wa TTCL ni dharau kubwa kwa shirika la umma?

Ushauri TTCL kwa kuwa ina assset zake, waendelee na biashara yake, ila majukumu yagawanywe..

Kuwe na Tanzania Telecoms Group ambayo ndani yake kutakua na kampuni Tanzu mbili.

1. TTCL mkondo wa taifa

2. TTCL mobile

TTCL mobile itafutiwe kajina kazuri (sisi mobile, au yetu mobile, au bongo mobile, serengeti mobile etc) na baadae share ziuzwe kuwa na partenaship kati ya serikali na private sector serikali ibaki na 49%..

Baadhi ya mashirika ya umma kama NSSF, tanoil etc wanaweza take advantage ya kuwekeza hapo kwani telco business ni moja ya biashara inayo lipa sana.

Kwa mtazamo wangu bado tunahitaji TTCL, serikali iige Kenya walivyo fanya hata kupata Safaricom ambayo leo serikali ina enjoy mgao wa maana kila mwaka.

Rais anahitaji kuwa optimistic na aggressive kwenye kusukuma agenda za nchi kuliko mtu yeyote.. Anatakiwa kuonyesha njia wengine wajifunze, anatakiwa kutwambia yanawezekana sehemu ambayo wengine wamekataa tamaaa. Hiyo ni kawaida hata kwa familia, na ndivyo binadamu tulivyo. Mguu ukiumia hatukimbilii kuukata bali tunajibidisha kuusimamia ili upone.

Mungu ibariki Tanzania

Amen.

Screenshot_20230412-175108_Google.jpg
 
Mkitaka hii nchi kila kitu afanye Rais. Tutasubirii sana. Issue ni hakuna utashi wala uzalendo wala ubunifu.Watu wanawaza wizi tu na mizaa.Haya yote yapo tangu bungeni mpaka serikalini. Mnataka Rais yeye kama yeye personally afanye kila kitu...wengine wapo tu?

Kila akigeuza shingo upigani..akienda kulia upigaji, hatuwezi fika kwa stahili hiyo.Watanzanie wabadirike kwanza mentally.

Tunaua mashirika yetu kwa ubinafsi wetu na roho mbaya.

1. Wakuu wa haya mashirika wapatikane kwa interview, tena public interview

2. Performance indices ziwe wazi..kuanzia kwa CEO mpaka wafanyakazi wadogo

3. Mikataba ya kazi iwe kama private sector isiwe ya umilele.

4. Iuze hisa kwa private sector...49% to 51% lkn pawe na mikataba mingine ambatanishi.
 
Pengine tu hujui, hiyo ripoti ya CAG kabla ionekane inakuwa imepelekwa kwa Mheshimiwa na anasomewa mbele ya wataalam wa uchumi

Mpaka kufikia Mheshimiwa kupaniki vile ni kuwa hakuna namna tena,

TTCL wamekula bil 20 hivi unawaza Mheshimiwa angefanya nini ?

Wakati mwingine watu waelewa tu japo ulaji upo pale pale
 
Umeelewa nilichi kiabdika bibie, au ? Kila pesa ttcl ni kutokana na maamuzi mabovu ya serikali kwa TTCL.. unawekaje ukada kama kigezo cha kuwa CEO wa kampuni ya biashara?
 
Juzi wakati Rais anapokea Report ya CAG , alitamka mambo mengi kwa hasira na jazba sana hadi wengine wanaona hakuwa sahihi..

Kwa cheo alicho nacho na maana ya report ya CAG hakutakiwa kutoa hukumu wakati ule kwa sababu report ya CAG ina utaratibu wake kwa serikali kuifanyia kazi.

Ndio maana lazima iende bungeni ijadiliwe, kamati za bunge zijiridhishe na zitoe maamuzi kwa serikali kuyafanyia kazi.

Maneno kama stupid, pumbavu hayakutakiwa kutoka kwa Mh Rais , kwa sababu kwa maneno hayo inaonekana kuna mambo yamemshinda sasa kilicho baki ni kutumia maneno yasiyo na staa kama kuwaadhibu wahusika.

Achana na hayo, Rais pia alitoa hukumu kwamba TTCL wameshindwa kujiendesha hivyo waache biashara.

Kama Rais alitakiwa asubiri bunge lipitie report na litoe maazimio.. sometimes CAG anakurupuka na kuandika mambo ambayo hata hayapo ila tuu kwa uvivu wake hakupata vielelelezo vya kutosha ..

Pili akisema namna hii ni mishirika mangapi anayayaambia yaache kufanya shughli zao za kibiashara?

Ukiangalia report ya CAG ilivyo na mbwembwe hata ikulu itatakiwa ufungwe kabisa..

Swali la kujiuliza, aliye feli ni Rais na serikali yake au TTCL? TTCL inahitaji utashi wa kibiashara.. Kama TTCL inajiendesha katika mazingira yanayo fanana na DAWASA je watashindana na Tigo au voda?

Mbona Moroco telecoms inapeta, mbona france telecoms inapeta? Tatizo la Tz ni nini?

Viongozi wasijizime data kuihukumu TTCL kana kwamba ni kitu cha mbali kisicho wahusu? Kuna watanzania wengi sana wenye uwezo wa kuibadirisha TTCL ikawa kampuni ya faida?

ATCL au TTCL kushindwa kupata faida Rais naye anahusika kwa sababu yeye ndio anahusika na uteuzi wa Viongozi? Kwanini CEO wasifuate mfumo wa uwazi kuwapata? Kazi itangazwe, na interview zifanyike kupitia mashirika maalumu yenye ujuzi katika kupata viongozi.

Mfano, CEO wa TTCL amemtoa kwenye shirika ambalo halifanyi biashara, na hajawahi kuwa CEO wa kampuni ya biashara katika mazingira ya ushindani? Je unadhani TTCL itajiendesha vipi? Mtu kama Kindama kuwa CEO wa TTCL ni dharau kubwa kwa shirika la umma?

Ushauri TTCL kwa kuwa ina assset zake, waendelee na biashara yake, ila majukumu yagawanywe..

Kuwe na Tanzania Telecoms Group ambayo ndani yake kutakua na kampuni Tanzu mbili.

1. TTCL mkondo wa taifa

2. TTCL mobile

TTCL mobile itafutiwe kajina kazuri ( sisi mobile, au yetu mobile, au bongo mobile, serengeti mobile etc) na baadae share ziuzwe kuwa na partenaship kati ya serikali na private sector serikali ibaki na 49%..

Baadhi ya mashirika ya umma kama NSSF, tanoil etc wanaweza take advantage ya kuwekeza hapo kwani telco business ni moja ya biashara inayo lipa sana.

Kwa mtazamo wangu bado tunahitaji TTCL , serikali iige kenya walivyo fanya hata kupata safaricom ambayo leo serikali ina enjoy mgao wa maana kila.mwaka.

Rais anahitaji kuwa optimistic na aggressive kwenye kusukuma agenda za nchi kuliko mtu yeyote.. Anatakiwa kuonyesha njia wengine wajifunze, anatakiwa kutwambia yanawezekana sehemu ambayo wengine wamekataa tamaaa.. hiyo ni kawaida hata kwa familia, na ndivyo binadamu tulivyo.. Mguu ukiumia hatukimbilii kuukata bali tunajibidisha kuusimamia ili upone.

Mungu ibariki Tanzania

Amen.View attachment 2587097
Umeongea fact sana ila chawa hawatakuelewa
 
Niliposikia pendekezo la CAG na Bi Mkubwa kwamba huko TPA bandari wanapaswa kuingia pia watu binafsi na hata TTCL, shirika la umma/serikali kuelekea kujifia, naanza kupata jibu kule wanakotaka tuelekee hawa jamaa.

Rais analalamika kwamba watu hawaendeshi vyema taasisi na miradi ya serikali. Why is she still there anyway?

Naona sasa ni mwendo wa kuwatunuku watu binafsi mashirika ya serikali.
 
Tatizo lako hujaelewa.. Suluhu ya TTCL sio kuifuta.. ni serikali kuacha urasimu kwenye kampuni za kibiashara.
Tatizo liko kwa hao hao Ttcl.kwanini wakubali urasimu wa serikali wakati wanajua utaliua shirika lao.Wewe kama ni mfanyakazi wa hilo shirika jua kabisa shirika limewashinda.Toka miaka ambayo ripoti ya Cag inapelekwa bungeni kwanza hilo shirika limeshakuja na jambo gani jipya?.Mngekua na akili mngefufukia kwa Magufuli kwasababu alishaonyesha nia ya kuwabeba ila bado mkawa hamujielewi.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom