furaha, amani na upendo...ndio maneno makuu mliyoyagusia Gaijin na JouneGwalu...
mmewahi kufikiria ili kufikia hiyo furaha, amani na upendo mnahitajika kupitia njia gani
ambayo/ambazo unaweza kumbana na vikwazo vya aina kwa aina?
je, mnakabiliana vipi na changamoto hizo...!
Furaha kwangu binafsi inahusisha vitu vinavyogawanyika kwenye mafungu mawili.
1) Nikiwa kwenye uhusiano mzuri na watu ninaowapenda nakuwa na furaha. Na ili niwe kwenye uhusiano mzuri na watu natumia kanuni ya kuwa mkweli ( to be me), kutoingilia maisha ya watu wengine, kuwa mcheshi kwa watu (though sometimes hii huibua tatizo)
2) Huwa na furaha nikiweza kufanya yale yanayonivutia na kunipendeza (hobbies) pamoja na kusambaza furaha kwa wengine (charities and presents). Ili niweze kufika hapo, nahitaji pesa.
Kikwazo kikubwa nafikiri kinakuja kwenye means za kutafuta pesa yenyewe. Mimi nakwenda na kanuni kuwa kazi si kazi unless iwe nafurahia kuifanya hata iwe na mshahara kiasi gani.
nadhani definition ya "mafanikio kimaisha" inatofautiana mtu na mtu kwa sababu inakuwa influenced na vitu vingi sana ikiwemo malezi, mazingira mtu aliyokulia, utamaduni wa eneo husika, pamoja na elimu
Hayo mawili yanahusiana sana...
Unapotafuta pesa, kuna na mwingine anazitafuta na kuna wakati inabidi m-compete kuzipata na hapo mahusiano yanakuwa compromised. Kwa haraka haraka, zaidi ya 50% ya magomvi kwenye jamii yanahusiana na pesa kwa namna moja au nyingine.... (challenge)...
Unachoongea kipo, lakini kwangu hadi sasa hakijawahi nikuta....labda ndo kwanza mapema kwenye haya masuala ya kuzisaka faranga
MbuKusema ukweli, kufanikiwa kimaisha (being successful) is a very subjective term ambayo mara nyingi huwa pia inategemea na society's standards. Kwa wengine mafanikio au kufanikiwa inamaanisha kuwa responsible, you make more than enough to pay your bills, you're married with children, you have a college degree and you have a prestigious job. Sure, kila mtu atakuangalia na kukudefine kama mtu mwenye mafanikio. Mara nyingi wengi wetu tunaishi kwa jinsi jamii inavyotumould na kujikuta mtu unajihesabu umefanikiwa kwa kuangalia acknowledgement ya wengine kwako kuwa umefanikiwa. Kwamba kwa wewe kujiita mtu aliyefanikiwa ni lazima kuwe na a general acknowledgement kutoka katika jamii, mfano watu wengi tunamwona Mzee Mengi kama mtu mwenye mafanikio sana
Lakini kama alivyosema Gaijin hapo juu……nani alishawahiuliza kama hawa tunaowaona wana mafanikio kama wana furaha, upendo na amani ndani ya mioyo, familia na nyumba zao?
So to me, being successful ni kuweza kuishi maisha yako to the fullest, ukiwa happy, umezungukwa na amani na upendo no matter una pesa kiasi gani, elimu kiasi gani au materials gani. Uwe na amani, upendo na furaha kiasi cha kuweza kufulfil malengo yako uliyojiwekea maishani.
Furaha kwangu binafsi inahusisha vitu vinavyogawanyika kwenye mafungu mawili.
1) Nikiwa kwenye uhusiano mzuri na watu ninaowapenda nakuwa na furaha. Na ili niwe kwenye uhusiano mzuri na watu natumia kanuni ya kuwa mkweli ( to be me), kutoingilia maisha ya watu wengine, kuwa mcheshi kwa watu (though sometimes hii huibua tatizo)
2) Huwa na furaha nikiweza kufanya yale yanayonivutia na kunipendeza (hobbies) pamoja na kusambaza furaha kwa wengine (charities and presents). Ili niweze kufika hapo, nahitaji pesa.
Kikwazo kikubwa nafikiri kinakuja kwenye means za kutafuta pesa yenyewe. Mimi nakwenda na kanuni kuwa kazi si kazi unless iwe nafurahia kuifanya hata iwe na mshahara kiasi gani.
Ah Mkuu sasa hii imekuwa kama interogation, nldhani tunapeana xperience kwamba na wewe utuambie maono yako!
Ila ok! Kufikia hayo mafanikio kwa kweli ni kuna changamoto sababu ile kuishi na kukutana watu tu ni changamoto tosha sana.
Hivyo mbinu mama ni kujielewa na kujitambua malengo yako, hii itakufanya usipoteze focus.
Kwa mbinu hyo itakufanya uweze kuelewa watu wa aina zote na namna ya kuishi nao, hii itakufanya kupata amani katika mapito unayopitia na vilevile upendo!
Amani na Upendo huzaa furaha ambayo huchochea nguvu ya kupambana