Mbu
JF-Expert Member
- Jan 11, 2007
- 12,753
- 7,844
- Thread starter
- #21
Mi inaonekana siridhiki, na sitakaa nifanikiwe kimaisha (sijui wenzangu), maana;
Mwaka 1995 (form 1); niliamini siku nikiweza kusoma hadi nikafika chuo kikuu cha SUA nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 1998 (form 4); wakati wa kombe la dunia, niliamini siku na mimi nikwa nakaa kwenye nyumba yangu (hata chumba cha kupanga), huku nikiwa na TV yangu naangalia kombe la dunia, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 2000 (form 6, bado sijafika SUA, sina TV), nikaongeza 'hitaji', kuwa siku nipate kazi, niwe najitegemea nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2002 (first year SUA); niliamini siku nikifanikiwa kuajiriwa kama mwalimu wa chuo kikuu nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2006 (4th yr, SUA); niliamini siku nikiwa na ajira inayonilipa kama laki nne hivi nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2007 (graduating SUA), niliamini siku nikiwa na ajira, nikaoa mke ninayempenda, nikawa na gari aina ya chaser, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha
Mwaka 2008 (nimeshaajiriwa, nimeshaoa), niliamini siku nikiwa na mtoto, nikiwa na Masters, nikiwa na ajira nzuri zaidi... nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
Mwaka 2010; ninaamini siku nikiwa na nyumba yangu mwenyewe (ghorofa), kipato cha kutosha niende ninapopenda wakati wowotena mke wangu, nitakuwa nimefanikiwa sana kimaisha...
2011; ???
2012; ???
n.k ...
Conclusion; Asilimia 99 ya vitu nilivyokuwa natamani hadi 2008 nimeshavipata, lakini kwa sasa najiona niko duni sana kimaisha, natamani, natamani natamani, na natamani niibadilishe Tanzania ifanane na Netherlands (can you imagine?!!)
Nikiwaza watu 'waliofanikiwa' kimaisha (kifedha), wanavyoendelea kufight kutafuta pesa, nikiangalia watu waliofanikiwa kijamii na kisiasa wanavyoendlea kutafuta kufanikiwa zaidi, inabidi niamini hakuna siku nitakokaa 'nifanikiwe kimaisha'
Decision; Nimeamua kuwa nitatumia 60% ya kipato changu 'kuifurahisha nafsi yangu na ya familia yangu na 40% kuwekeza kwa ajili ya baadae, maana nimeshaona kuwa hakuna siku nitakayorizika eti nimeshavuna sasa nianze kula...
...ni kama vile ulikuwa mawazoni mwangu wakati naitengeneza thread hii...
mwanzoni, nilifikiria kuipa title life starts at 40....kisha nikafikiria mitazamo tofauti ya watu itakinzana na ninachokitafuta.
kiukweli, hayo yote uliyoyaorodhesha hapo juu ni sahihi kabisa....
- inaonekana mtazamo wako kwa kiwangi kikubwa unalingana na mimi. Nitakupa mfano;
- kwa umri wangu (40) tayari nishaonja matamu na machungu ya mapenzi, ndoa na talaka
- kwa umri wangu, tayari watoto wote weshamaliza GCSE wote wapo college na universities
- kwa umri wangu, "i live my dream"...my dream job na maisha overseas
- kwa umri wangu, na freedom ya movement popote pale ulimwenguni (nikitaka!)
- kwa umri wangu, na SWOT analysis...am secured kimaisha sababu ya investments za hapa na pale iwapo nitazi manage vizuri.
who said life starts at 40?