Maelezo ya Zitto kuhusu amri yake kwa wabunge wa CHADEMA

Watu wa CCM hamna mamlaka ya kutuchagulia viongozi.
Watu wa CCM hamna mamlaka ya kutuchagulia viongozi.

Mkuu, ni maoni yangu tu juu ya utendaji kazi uliotukuka wa ndugu Zitto na wala sio kwamba nawachagulia hawe kiongozi wenu.

Watu wa aina ya Zitto hapa Tanzania ni wachache sana, ukimuacha mtu kama mhe Membe, mhe Mwakyembe, mhe Salim Ahmed Salim, mhe Sitta, mhe January Makamba n.k ndio unawakuta wakina Zitto huko upinzani, kwahiyo ni katika kutoa maoni kwamba, CCM tunawatumia watu potential effectively na tunaendelea kuishikilia dola, je, hamuoni kama kuna haja ya kuwapa watu wa aina Zitto mamlaka makubwa huko CHADEMA ili upinzani ulete ushindani sahihi? na sio huu wa sasa ambao ni legelege na sababu kubwa ya ulege lege huu ni kusinzia kwa mwenyekiti na katibu mkuu wa chama chenu.
 
Mhe Zitto nakupa pongezi sana kwa kutufundisha namna ya kuwa kiongozi said:
Mawazo yak ni mazuri ILA yanafanana na wale watu ambao huwa nawasikia wakisema "Timu ingalifungwa goli nyingi NI golikipa aliyewasaidia!"Wanasahau kwamba kazi ya golikipa ni kuzuia mipira kutinga kwenye nyavu!Kazi ya Zitto na wabunge wengine wa CHADEMA ni kutumia vipawa vyao kuijenga CHADEMA! Kwa hilo sioni kama amezidisha kwa kufanya wajibu wake kama kiongozi!
 
kuna watu hapa JF Jana walileta hii hoja katika namna iliyonifanya nikashindwa kumuelewa Zitto matokeo yake nikaishia kumshambulia, leo asubuhi nimesikia clouds FM Vizuri na ninamuunga mkono pia. Alisema anapiga marufuku kuisifia serikali kwa sababu amegundua inatumia vibaya appreciations zao.

Siku ingine jitahidi uwe unatulia na kutafiti kidogo kabla hujaanza kulaumu ili pia uepuke kujilaumu!!
 
Mkuu kutoappreciate au kuapreciate yote sawa tu cha msingi yaliyofanyika yanaonekana na yamefanyika kwa uadilifu
 
Serikali ya ccm inajiuza kwa wananchi kwa mazuri yake, haina shida na sifa za kijinga

Ingekuwa inajiuza kwa mazuri nafikili bei ya korosho isingeleta maafa kwa viongozi wa CCM huko kusini, barabara zisingekuwa zinajengwa kwa kiwango hafifu kama ilivyo kwa barabara ya Kilwa, maji yangepatikana kwa wananchi bila usumbufu, umeme ungepatikana katika maeneo mengi bila kukatikakatika na zahanati zilizojengwa na wananchi zisingekosa wahudumu na vifaa mpaka leo kiasi cha kutofunguliwa.
 
Amri ya zito ni ya kinafki,ndio maana haijaheshimiwa. Leo msigwa kamsifia sana waziri wa viwanda na biashara.
 
Hivi kwanini maccm mnampenda zitto? Mnavyompenda ndivyo ninavyozidi kumchukia.
 
Uko wapi uhuru wa kutoa maoni? Kanuni za bunge zinawalinda wabunge wako huru kusema chochote ingawa wengine wanautumia vibaya

Sasa Zitto anawazuia ipo wapi demokrasia?
Kumbe mtu unaweza kuwa mtumwa uku ukiamini uko huru. Nitawashangaa sana wabunge wa CDM kama watamsikiliza

Poleni sana watumwa wa mawazo ya wengine

Elewa ujumbe kwanza ndo uandike, siyo kukurupuka. Mantiki ni kuwa appreciation ndo unakuwa mtaji kwa kubeza upinzani. Sio kukatazwa kaka. Tanzania tuna hali ngumu ya kuelewa maana halisi. Mh, kazi ipo sana kuelimisha.
 
Mtataga mwaka huu kwa kuiwaza na kuitamka chadema kila saa!!!magamba ni rubbish eti wanauzika!!mbona mnalazimisha mwenyekiti wa kijiji anatangazwa na polisi?mmemwingiza choo cha kike na raia tunasema ahamishie ofic kituoni kwa polisisiem..
 
Kwa kawaida, inapofika wakati serikali inayoongozwa na chama cha mapinduzi (CCM) inapofanya utekelezaji wa kazi zake kulingana na Ilani ya chama, mipango ya maendeleo na maazimio ya bunge huwa inapongezwa bungeni kwa utekelezaji wao huo, na ni kama desturi kwa baadhi ya mawaziri wakiwa bungeni upongezwa na wabunge bila kujali itikadi zao za kichama.

Jana, wakati wabunge wakichangia katika hotuba ya wizara ya ujenzi, wengi wa wabunge hao waliipongeza wizara na baadhi ya taasisi zake, mfano wakala wa ujenzi barabara (TANROADS), katika kupongeza huku wabunge wengi wa upinzani walikuwa miongoni mwa wabunge walioipongeza wizara ya ujenzi.

Lakini kizaizai kilikuja pale mhe. Magufuli alipokuwa akifanya majumuhisho ya hotuba yake na michango mbalimbali ya wabunge, hapa mhe. Magufuli alionekana waziwazi kuwabeza wapinzani kwa kuisifia kwao wizara yake inayoongozwa na mtu wa CCM. Jambo lililoonekana kuwakera baadhi ya wabunge wa upinzani akiwemo naibu kiongozi wa kambi hiyo, ndugu Zitto Kabwe.

Haya hapa ni maneno aliyoyasema ndugu Zitto Kabwe alipoonyesha kukerwa kwake na waziri Magufuli, nanukuu, "Tumekuwa na uungwana wa kutambua juhudi mbalimbali za serikali katika kuleta maendeleo nchini. Mara kadhaa mimi binafsi, kiongozi wa upinzani bungeni na wabunge wengine wa chadema tumekuwa tukitambua juhudi hizo. Hata hivyo “appreciation” yetu ya nia njema kabisa imekuwa ikichukuliwa kisiasa na mawaziri wa CCM na hivyo kutubeza. Leo waziri Magufili kaja na flash disk yenye kauli ya ndugu Mbowe huko Hai. Pia kabeza wabunge wengi wa upinzani. Nikiwa kiongozi wa upinzani bungeni, nimeagiza kwamba kuanzia leo ni marufuku kwa mbunge wa chadema ku appreciate kazi ya serikali. Uungwana wetu usitumike kutuponza. Tufanye kazi yetu kuisimamia serikali."

Maoni yangu:

Katika siku ambazo nimeona mhe Zitto ametumia mamlaka yake kikamilifu katika kuongoza ni baada ya kutoa hii kauli, huyu kijana ana sifa za kuwa kiongozi, jambo kama hili kwa kiongozi legelege hasinge thubutu kulitamka hata kama alipaswa kufanya hivyo, kiongozi anae ogopa ogopa kuyatumia madaraka yake ipasavyo hana sifa za kuwa kiongozi, kiongozi ni kauli na inapotolewa kauli inapaswa iheshimiwe na unao waongoza.

Mhe Zitto nakupa pongezi sana kwa kutufundisha namna ya kuwa kiongozi, naamini huu ni mwanzo tu na hata mhe Mbowe kama kiongozi wa upinzani ataiga namna bora yakutumia mamlaka yake aliyo nayo ndani ya CHADEMA na hata bungeni. Kama mhe Zitto angekuwa mwenyekiti wa CHADEMA, basi upinzani ungekuwa umeimarika sana na hata ndoto za wapinzani kuingia Ikulu zingeweza kuwa na tija, lakini ndio hivyo tena, nabii akubaliki kwao.
HAMY-D Kauli ya Zitto nimeikubali, ila hapo kwenye red, naona umekaribishwa sebuleni, unakimbilia chumbani. Zitto ni kiongozi mwandamizi wa Chadema na Ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, in absence of Mh. Mbowe Zitto ndo Kiongozi wa Upinzani na anaruhusiwa kutumia Mamlaka hayo na aliyatumia vyema.
 
Last edited by a moderator:
Magufuli anadhani kwa vile utendaji kazi wake angalao unakubalika kuliko mawaziri wenzake anaweza kudharau au kubeza wengine. Kama ni kweli amewabeza wapinzani wakati wao wamekuwa waungwana na kuonyesha kumuunga mkono hana maana kabisa.

Naunga mkono msimamo wa Mh. Zitto Kabwe.
 
Back
Top Bottom