Maelezo binafsi ya Mhe. Zitto Zuberi Kabwe dhidi ya tuhuma za rushwa kwa Umma

Nimejiridhisha na maelezo ya Mh.Zitto Kabwe kuwa hahusiki na uzushi huu au siasa majitaka zinazoendeshwa dhidi yake. Hata hivyo siku si nyingi wanafiki wote watajulikana.
 
kaza buti kikomandoo. Mwambie Dr. Slaa huo mwanzo tu, uchafuzi umeanza. Mie nadhani ile kampeni ya kuweka saini na mkakati wa kumfanya mzee avunje baraza la mawaziri limemfanya achukie. Ko wamekutafuta wakahisi hapo ndo kukupa kadoa. Wadau tumelijua hilo kwa kina. Tunacheki upepo unapoenda, usikonde we kula pozi wakikung'oa jembe nami najing'oa u'TZ. We JEMBE ZAIDI YA MAJEMBE. Lima makunguru hayo maoga. Kwa usemi huo yasha banwa na haja makwao huko.
 
Kajitetee kwenye kamati ya maadili kwanza. Si ulisema wewe mwadilifu, ngoja wakuonyeshe kazi. Hiyo kamati yaweza kuongozwa na mbunge yeyote usijifanye wewe ndo mungu wa hiyo kamati
 
Haya tumekusikia Mh Zito, tunaomba utuachie muda tuwasikie wanaokutuhumu nao wakuhoji na kutoa ushahidi wao halafu kama watu wenye fikra pevu basi tutaweza kujua ukweli upo wapi.
 
What goes around comes around huyu Zitto ndio Kinara wa kutumia wandishi wa habari uchwara kwa manufa yake na siasa zake za kubato wanajamnv kwa wale wanaomfuatilia sana zitto wanakumbuka vizuri lile sakata la kutumia waandishi wa habari wa mwananchi ili kudhofisha Chadema tena alikua anatoa maelekezo namna gani zile habari ziandikwe. Asianze kutafuta huruma ya wananchi mimi binafsi nilimkubali sana zitto lakini kwa kweli kwa sasa sina imani naye tena.
Bahati mbaya ni kwamba gazeti letu lilokua linatupa habari za uhakika limefutwa kiujanaja na serikali lakini Zitto ni ndumilakuwili asihurumiwe kabisa watu wanajadili namna ya kuiimarisha chama yeye kila uchao ni uraisi kwanini tusiamini kwamba anadhofisha chama chetu makini kwa hili kapatikana
 
Kuna vitu vingine hata hakutakiwa kuongea bwana ..zaidi anazidi kuharibu cheki hiki kipengele
  1. Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
  2. Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa.....

ni obvious kuwa kuelekea 2015 propaganda za kisiasa zitakuwa nying na hatari si kwa CCM pekee hata Upinzani. hatari zaidi itawakabili wale wanaoonyesha nia ya kugombea urais. busara na hekima ni muhimu sana
 
Kinachotokea hapa ni kwamba Zitto anatumikia kundi moja kule CCM na mkumbuke kuna makundi mengi CCM zitto anaweza kudhani ni cdm wanampiga vita kumbe kule ccm alikolalia makundi yameanza kunyukana kwa vyovyote ataathirika sana kijana, inavyoelekea zitto hajajua nani anampiga haswa.Kule ccm wamemtumia na kuna kundi moja tayari limepata taarifa kuwa anaandaliwa kuwa Emanuel WA ccm KWA SIKU ZIJAZO HASA ATAKPOKAMILISHA mission hapa CDM.GET TUNED

Maelezo yako yana ukweli fulani,lakini niseme kwa upande wangu Zitto amekua karibu na JK kupitia mwanae Ridhiwani. Ni mahusiano ya kifamilia zaidi. Kwa watu wanaoongozwa na chuki hawawezi kubaliana na maelezo ya Zitto. Waliopanga mchezo,walijipanga kuwachafua wote ambao watahoji kama Sheria, Taratibu na Kanuni zimefuatwa wakati wa kuwapatia tenda kampuni ya PUMA. Ktk nchi zetu hizi ambazo tunaanza kujenga utamaduni wa kufuata sheria na taratibu ni dhambi kubwa kumnyamazia mtu anayezikiuka kwa sababu zozote zile. Mtu wa aina hiyo mkimpatia Urais hawezi heshimu hata Katiba ya nchi.
 
Siasa ni ngumu kwa nchi yoyote huwa wanachafuana..........Nani aliamini mpiga kelele Ole Sendeka ni mla mlungula?
 
He is confident maybe hizo tuhuma ndio ziile "gutter politics" zilizobobea CCM it's time for CDM now to stand with him.. Ili waendelee kuwaumbua hawa mabaradhuli, eti naskia na Ole Sendeka ndani! Kweli Mungu hamfichi mnafki.

Why CDM should stand with him? Kwani wakati anaanza malumbano na Wizara ya Nishati na Madini alipata baraka za chama? Zitto kama Mwenyekiti wa POAC ana kauli gani kuhusu wingi na ukubwa wa hujuma walizogundua Muhongo na Maswi ndani ya kipindi kifupi? Mbona hata siku maoja hajatoa kauli hata moja ya kuwapongeza?

Tunatambua kuwa hivi sasa Zitto ana mahitaji makubwa ya pesa za kujenga mtandao wa kusaka urais kupitia fronts mbali mbali ikiwemo ADC etc hivyo si ajabu kugeuka FISADI kwani hao walichotoa fedha za umma kujenga mitandao na wakafanikiwa kuukwa urais wamechukuliwa hatua gani si mabo yameisgia blah blah tu. Hiki ni kivutio kikubwa cha wakati kugeuka mafisadi. Ushauri wangu kwa Zitto ni kuwa awaache Muhongo na Maswi wachape kazi tunataka umeme.

Zitto asisahau kuwa malipo ya ubaya waote ni hapa hap duniani. Wakati alipofadhili maasi huko NCCR hakujua kuwa kle pia kilikuwa ni chama Pinzani? KUTOKANA NA KUZIDIWA NA TAMAA, ITS AN END OF AN ERA
 
Zitto Kabwe !! Poor Zitto Kabwe !!

Umeanza kuvuna ulichopanda kwa muda mrefu,na this time kitu ambacho hujajua bado ni kwamba maadui zako wa kisiasa walioko ndani ya CHADEMA,CCM na kwingineko wamepata mlango wa kukutolea nje (this is your exit door brother !)!
Nimesoma ufafanuzi wako taratibu na kwa makini sana ! unayao hofu kubwa sana kaka! Na hofu yako imejengeka kuwa kamati yako inaweza kuvunjwa na hakuna kitu usichoomba kitokee kama hicho ! Shukuru humu JF ni wengi and they can't read between lines! Unajua kabisa kamati yako ya POAC ikivunjwa historia itakuwa imeandikwa na you will go down the history!
Zitto tunaokujua tangu DARUSO tunajua beyond reasonable doubt kuwa huwezi kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu !
Ni mara ngapi ukiwa Katibu Mkuu wa DARUSO ulitaka kumpindua Rais wako (Julius Rugemalira) kwa kuwatumia "remote control" wako akina Alberto Msando? Na main reason ni kwamba uliamini sana kuwa wewe ni Smart kuliko Ruge na ulipaswa wewe ndo eti uwe President! Hii wrong atitude imeendelea kukutafuna hadi leo ndani ya CHADEMA Brother!

Nimecheka sana pale ulipodai kuwa wewe umebeba matumaini ya wanyonge na vijana wa Taifa hili!
Mnyonge gani au kijana gani anaota kuendesha Hammer kama yako na kumiliki magari mengi ya kifahari kama uliyonayo na yasiyo na kazi! Tunatambua kuwa wewe ni mchapakazi na unajituma sana lakini zaidi panapokuwa na person interest zako kaka!
Kanuni aliyotumia Baba wa Taifa kum disqualify Lowassa the same applied to you brother!
Kwa ukwasi uliojikusanyia kwa muda mfupi ndani ya siasa hata kama hatuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa umepata kwa njia isiyo halali lakini pia hakuna anayeweza kutufanya tusifikiri vinginevyo!
Nimesoma hotuba ya Mnyika kama waziri kivuli bungeni na niki compare na maelezo yako brother this is your time,u have to go! Your political destiny lies in the hand of Speaker Anne Makinda.

SAMAKI WENYE VURUGU WAENDAO KWA PAPARA MARA NYINGI WAMEMEZWA NA SANGARA ZIWANI!
 
Vibaka wa CCM acheni kutumwa bila kupewa akili na principle za kazi yenyewe,hv zitto angekuwa fisadi kulikuwa na haja gani kuwa na operation ya kuwafichua mafisadi? Si angeungana nao kisela tu kama wanavyofanya ccm waliokutuma? Me naelewa jamii imekuwa na ckio la pekee kwa sababu ya wa2 kama zitto.
 
anayo
sema
Mh.Zito ni ukweli kama ilivyoelezwa na Mh. Rostam Azizi kuwa hizi ni siasa Uchwara na watanzania tusipowashtukia hawa watatupeleka pabaya. Kama tatizo ni uenyekiti wa POAC basi waitafute kwa utaratibu maalum na sio siasa za kupakana matope. Naamini ukweli utajulikana tu na tutajua ukweli na uongo. Nachelea kusema lengo la hili kweli ilikuwa kuinusuru bajeti ya wizara ya nishati na madini ila tusubiri ukweli utajulikana.
 
What goes around comes around huyu Zitto ndio Kinara wa kutumia wandishi wa habari uchwara kwa manufa yake na siasa zake za kubato wanajamnv kwa wale wanaomfuatilia sana zitto wanakumbuka vizuri lile sakata la kutumia waandishi wa habari wa mwananchi ili kudhofisha Chadema tena alikua anatoa maelekezo namna gani zile habari ziandikwe. Asianze kutafuta huruma ya wananchi mimi binafsi nilimkubali sana zitto lakini kwa kweli kwa sasa sina imani naye tena.
Bahati mbaya ni kwamba gazeti letu lilokua linatupa habari za uhakika limefutwa kiujanaja na serikali lakini Zitto ni ndumilakuwili asihurumiwe kabisa watu wanajadili namna ya kuiimarisha chama yeye kila uchao ni uraisi kwanini tusiamini kwamba anadhofisha chama chetu makini kwa hili kapatikana
naamini umeshapanik wewe...hebu kaka zitto endelea kukaza uzi kitaeleweka tu...
 
Wa ndugu Jf
Kwa kupitia jukwaa hili napenda kutoa Pongezi zangu za dhati kabisa,zikiambatanishwa na salamu za pongezi toka kwa wana DIASPORA waliopo pale MAREKANI na AUSTRALIA jimbo la Autras(es.AO#1774) kwa namna MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI ALIVYOWEZA KUTOA MAJIBU YA KURIDHISHA MACHONI NA MIOYONI MWETU
Tumekuwa tukifuatilia kwa ukaribu sana zoezi lote la kuhusishwa na kashfa ya Rushwa kwa mbunge huyu tegemeo kwa Taifa letu la Tanzania.Lakini kupitia mkaelezo yake aliyoyatoa kwenye media tumeshangazwa namna mbunge huyu alivyo jawa na ujasiri wa hali ya juu huku akiwafungulia milango wale wote wanaomtilia mashaka hadi muda huu kwamba

  1. Ni kwa sababu hiyo, na kwa kujiamini kabisa nimeunga mkono suala la tuhuma za rushwa zinazotajwa zichunguzwe na Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa kina;

  1. Nimekwenda mbali zaidi kukiomba chama changu CHADEMA kifanye pia uchunguzi na tathmini yake kwa kina kujiridhisha na tuhuma hizo;

  1. Natumia fursa hii pia kuomba vyombo vya Dola vichunguze tuhuma hizo kwa nafasi yake ili kuweza kupata ukweli;

  1. Ninaahidi kushiriki kikamilifu iwapo nitatakiwa katika uchunguzi wowote utakaofanywa na niko tayari kuwajibika iwapo nitakutwa na hatia yeyote.

Watanzania mwenye shida na Mbunge huyu bila shaka amefunguliwa milango amchunguze.
Tuanakuombea mafanikio mema ya vita dhidi ya rushwa,Watashindana lakini hawatashinda.
Kwaniaba ya watanzania wa chuo kikuu Arved unv.
Mmassy Kesi,Calfonia provi.

Asanteni:
 
Nimeyasoma hayo maelezo mkuu wangu lakini ambacho hakijatajwa na ambacho ndicho naulizia, ni taratibu zipi specifically ambazo hazikufuatwa katika kumsimamisha kazi mhando??

Kwakuwa zipo taratibu/ kanuni za kufuata katika kumchukulia mtumishi hatua za kinidhamu, sasa hapa ndipo nataka kufahamu ni taratibu zipi ama kanuni gani haikufuatwa?
mkuu nimeperuzi hadi page ya 14 sijaona popote Mohammed Shossi alipokujibu, hahahahaha
zaidi nilikutana na post moja jamaa inasemekana anautetea sana uongozi wa mzee mwinyi na huu wa JK, pia anamtetea sana zito, nashindwa kuunganisha dots, Mwinyi, Jk then ZZK. loh!
 
Last edited by a moderator:
Zitto Kabwe !! Poor Zitto Kabwe !!

Umeanza kuvuna ulichopanda kwa muda mrefu,na this time kitu ambacho hujajua bado ni kwamba maadui zako wa kisiasa walioko ndani ya CHADEMA,CCM na kwingineko wamepata mlango wa kukutolea nje (this is your exit door brother !)!
Nimesoma ufafanuzi wako taratibu na kwa makini sana ! unayao hofu kubwa sana kaka! Na hofu yako imejengeka kuwa kamati yako inaweza kuvunjwa na hakuna kitu usichoomba kitokee kama hicho ! Shukuru humu JF ni wengi and they can't read between lines! Unajua kabisa kamati yako ya POAC ikivunjwa historia itakuwa imeandikwa na you will go down the history!
Zitto tunaokujua tangu DARUSO tunajua beyond reasonable doubt kuwa huwezi kuwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu !
Ni mara ngapi ukiwa Katibu Mkuu wa DARUSO ulitaka kumpindua Rais wako (Julius Rugemalira) kwa kuwatumia "remote control" wako akina Alberto Msando? Na main reason ni kwamba uliamini sana kuwa wewe ni Smart kuliko Ruge na ulipaswa wewe ndo eti uwe President! Hii wrong atitude imeendelea kukutafuna hadi leo ndani ya CHADEMA Brother!

Nimecheka sana pale ulipodai kuwa wewe umebeba matumaini ya wanyonge na vijana wa Taifa hili!
Mnyonge gani au kijana gani anaota kuendesha Hammer kama yako na kumiliki magari mengi ya kifahari kama uliyonayo na yasiyo na kazi! Tunatambua kuwa wewe ni mchapakazi na unajituma sana lakini zaidi panapokuwa na person interest zako kaka!
Kanuni aliyotumia Baba wa Taifa kum disqualify Lowassa the same applied to you brother!
Kwa ukwasi uliojikusanyia kwa muda mfupi ndani ya siasa hata kama hatuna ushahidi wa moja kwa moja kuwa umepata kwa njia isiyo halali lakini pia hakuna anayeweza kutufanya tusifikiri vinginevyo!
Nimesoma hotuba ya Mnyika kama waziri kivuli bungeni na niki compare na maelezo yako brother this is your time,u have to go! Your political destiny lies in the hand of Speaker Anne Makinda.

SAMAKI WENYE VURUGU WAENDAO KWA PAPARA MARA NYINGI WAMEMEZWA NA SANGARA ZIWANI!
chuki binafsi..
mimi ni kijana na masikini pia ninakubali kabisa kuwa zitto ni chaguo la wanyonge.
zitto ni masikini, zitto ni mlala hoi. na zaidi ya yote zitto anatokea kwenye familia ya kimasikini kabisa...ni mungu tu ndiye aliyependa zitto awe mzalendo hivi. na kwa kweli kama zitto asingekuwa mzalendo kiasi ambacho alichonacho basi kwa sasa angekuwa tajiri sana kwa wizi wa mali za umma.lakini si kwa zitto.
juzi umenzisha operesheni ya kuwasimamia masikini wenzako na watoto pia wa walalahoi, wasanii wa bongo fleva, umeanza kuwaunganisha kupitia wasanii wa kigoma na kuwafanya wajivunie vipaji vyao na kuvigeuza kuwa ajira zaidi.
hukuishia hapo, sasa umekubali kuchukiwa, kunyooshewa vidole kwa kuwasimamia wasanii hao kudai haki zao kwa kujitoa kwenye mikataba ya ringtones ambayo inawanyonya...na leo nimesikia kwenye redio kuwa wasanii wote kwa pamoja wameungana na kuorodhesha majina yao kuomba kujiondoa kwenye mikataba hii mibovu...zitto zitto zitto, nakuomba usivunjike moyo na hawa wanafiki wasioishiwa na hila..nakuomba zitto tafadhali sana endelea kutusimamia sisi masikini wenzio tunaokutegemea...wapinzani wenzio wanaopiga kelele wengi wao ni wafanya biashara ambao hawaujui umasikini hata ulivyo na unafananaje, ninakuomba sana sana sana usituache sisi uliojitolea kutukomboa...MUNGU ATAKUONGOZA ZAIDI NA DUA ZETU ZITAKUFIKIA...KUMBUKA DUA YA ANAYEONEWA MWENYEZI MUNGU HUIPOKEA KWA HARAKA...
UTASHINDA KWA NGUVU ZA MUNGU
 
Back
Top Bottom