Jiwe Linaloishi
JF-Expert Member
- May 24, 2008
- 3,736
- 2,137
mkiandika ZZK nakumbuka Zana Za Kilimo... kumbe mnamaanisha Zitto Zuberi Kabwe.... kwa sasa sina la kusema nasubiri nichanganye na zangu then nifanye conclusion..
1. Re: Zitto: Sijahongwa, ni siasa za urais na hasira za posho!
Hekima inanikumbusha katika historia ya wana wa Israeli na kisa cha wao kuingia na kukaa nchini Misri. Alikuwa ni nabii Yusuph juu yake iwe rehema na amani aliyechukiwa na ndugu zake. Wakafanya fitina kubwa ya kukamia na kutaka kumuua. Azma yao ilipotimia Mwenyezi Mungu akamuokoa. Ikaja suala la kutaka kubakwa na mke wa bwana wake kwa sababu ya uzuri wake usiomithilika. Akakimbia nje na mwanamke akamchana kanzu yake kwa nyuma. Ghafla bwana mwenye nyumba akawa anaingia na kukutana na sekeseke hilo. Mara yule mwanamke akamsingizia Yusuph uongo na kusema; "Hakuna malipo ya mtu anayetaka kumbaka mkeo isipokuwa jela". kitoto kidogo kikamsafisha Yusuph na kusema; ikiwa kanzu ya yusuph imechanwa mbele basi yusuph ana makosa, na ikiwa imechanwa nyuma basi yusuph ni msafi na mwanamke ana makosa".
Mzee akaona kuzima soo bora ampeleke jamaa jela.
Huko jela akawabashiria waota ndoto juu ya yatakayowatokea na ikaja kuwa kweli. Yule jamaa aliyepandisha cheo akaombwa amkumbuke katika ufalme lakini kama ilivyokawaida ya binadamu - kuhukumu mtu kwa ubaya na kusahau mema yake yote, yule jamaa kampotezea. Uzalendo wake wote, ukweli wake wote na uadilifu wake wote ukawa sio kitu bali na kejeli juu.
Zama zikapita na Ikaja wakati mfalme wa wakati huo akaota ndoto iliyoashiria miaka ya neema na tabu. waganga na makuhani wakaitwa na wote wakashindwa kukokotoa ndoto ile. Wakasema hizo ni ndoto zilizoparaganyika. Mshikaji kakumbuka yule jamaa wa gerezani aliyemsaidia kupata cheo.
Nabii Yusuph akaitwa na kukokotoa ndoto ile na a asema ni YEYE PEKEE AMBAYE ANAWEZA KUSIMAMIA ILE KAZI YA KUKUSANYA MAVUNO KWA MIAKA SABA ili iwafae kipindi cha miaka saba ya shida. Mfalme AKAMKABIDHI KAZI ILE NA AKAIFANYA KWA USTADI. Mfalme hakuangalia UMRI wa kijana Yusuph bali AZMA na Uwezo wa kiakili.
Sharti la kwanza aliloweka Yusuph ili kukubali kazi ya uweka hazina ni kuwa aletwe yule mama aliyetaka kumbaka ili athibitishe ni nani aliyekuwa mkosaji. Yule mama (mzee sasa na aliyepoteza nuru ya macho) akakiri kuwa alimpenda sana yusuph kinyume na matakwa yake kiasi cha kushindwa kujizuia.
Baada ya hapo Mwenyezi Mungu akamrudishia nuru na macho yule mama na akamfanya mzuri (KIGORI) na akaja kuwa ndiye MKEWE YUSUPH.
HALELUYA!!!!!!!!!!!
My stance: HEKIMA HUPEWA WACHACHE.
Hivi Zitto mbona anaandika vitu kama mtoto wa darasa la kwanza? Sasa hii sentensi ina maana gani ". Naamini katika nchi yetu tunazo rasilimali za kutosha mahitaji/haja ya kila mmoja wetu lakini si ‘tamaa/ulafi' wa baadhi ya watanzania wenzetu;"
hapo red sijaelewa zzk....mmmh
- Nafahamu pia kuwa kuna wanasiasa hasa wa Upinzani ambao wanautaka sana Uenyekiti wa POAC na wanafanya kila njia kutaka kuidhoofisha. Lakini hawajui kuwa anaepanga wajumbe wa Kamati ni Spika wa Bunge.
- Msishangae pia kuja baadae kubaini kwamba baadhi ya wanasiasa wenye midomo mikubwa ya kutuhumu wenzao wao ndio vinara wa kupokea rushwa
Pole sana, Naona unaweweseka na Matola bure, kwa taarifa yako Matola is no body ni Mwananchi wa kawaida ambaye hata bado sijafikiria kuwa Mwanachama wa Chadema licha ya kuisaidia Chadema kwa hali na mali.Nimeingia leo JF kwa ajili ya post yako maridhawa, umemeliza kila kitu, salaam kwa Matola na wale wote walo ktk upofu, Zito hana wa kumfikia CDM.
Mwisho
Kumejengeka tabia hivi sasa ya kuwamaliza wanasiasa wenye kudai uwajibikaji na uzalendo. Kumeanzishwa kiwanda kwenye medani ya siasa cha kuzalisha majungu na fitna zenye lengo la kuwachonganisha wanasiasa wa aina hiyo na wananchi kwa kutumia vyombo vya habari na nguvu ya fedha. Naamini mbinu hizi chafu, kama nyingine nyingi zilizojaribiwa kwangu huko nyuma nazo zitashindwa.
Naamini katika kweli na kweli daima huniweka huru. Naamini kuwa mwale mdogo wa mwanga wa mshumaa hufukuza kiza. Kwa imani hiyo, sitasalimu amri mbele ya dhamira zao ovu hata nitakapobaki peke yangu katika mapambano hayo ya kulinda na kutetea rasilimali za taifa zinufaishe watanzania wote.
Daima nitaongozwa na busara ya Hayati Shabaan Robert isemayo, Msema kweli huchukiwa na marafiki zake, nitakapofikwa na ajali hiyo, sitaona wivu juu ya wale wawezao kudumu na marafiki zao siku zote, siwezi kuikana kweli kwa kuchelea upweke wa kitambo, nikajitenga na furaha ya kweli itakayotokea pale uwongo utakapojitenga.
Ahsanteni sana.
Hizo mbinu werevu tulishazijua.piga kazi zito,hauko mwenyewe utashinda tu.MUNGU MKUBWA
hoja yako ni dhaifu!
Mkuki kwa nguruwe huo kwani mara ngapi Zitto naye aliweza kukemea tabia ya viongozi wa CC0 na magazeti wanamchonganisha yy na chama chake CDM?
Je ni ara ngapi Zitto aliwahi kukanusha propaganda za udini, Ukabila, na ukanda zinazoelekezwa kwa chama chake?
THINK BIG
Not convinced... Ni yale yale anayoyasema kila siku.. Tuhuma tofauti, utetezi ule ule... kuonewa, kuhujumiwa na siasa chafu. Why wewe tu? Utasema posho na Urais! Ila binafsi nitakuwa wa mwisho kukubaliana na wewe
zito mimi ni mwana chama wa chadema nanina ipenda sana chadema tena mapenz ya dhati kabisa ya kutoka moyoni lakini kwa taarifa nilizopewa na mtu wa karibu sana na muhando kuwa umekuwa ukionekana nyumbani kwa muhando mikocheni mara kwa mara je huwa unakwenda kufanya nini na hiyo mara ya mwisho kuonekana ni kabla ya habari ya gazeti la RAI kutoka na matokeo yake ndo hilo gazeti likatoa habari ya katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini na hata kabla ya hapo mtu aliyekuwa karibu sana wewe alikuwa akikusikia ukizungumza na simu kutoa maagizo juu ya taarifa itakayo andikwa kwenye gazeti na mengine mengi tu ambayo nikiyaa ndika hapa waweza juta kujiingiza kwenye mambo ya ajabu pasipo kujali kuwa chama chako saizi kina nafasi kubwa sana ya kutwaa dola ushauri wangu kwa zito umejisahau sana umebweteka unahitaji kukaa chini ukaangalia mstakabali wako nin ufanye kujisafisha ni mengi tuna jua kuhusu ww zito ila aitusaidi kuyaweka hapa adhalani tunachokuomba jirekebishe ili wananchi waendelee kuwa na imani na wewe.
Well said,
Ila kama ulivyosema tuiachie kamati ya kinga na maadili ya Bunge ichunguze kila kitu na wale walio wasafi na wachafu pumba na mchele utaonekana.
Mapambano yapo Mhe Zitto na sio madogo ila unapokuwa mpambanaji kubali yote.
Kuna kuanikwa mpaka siri zako za ndani ili kuwadhoofisha wale ambao wanapambana ili tuu kukuvunja moyo usipambane ila kama unaamini katika Mungu yote ni mapito wanasema utashinda na mnafiki mwishowe atajionyesha