Elections 2010 Madiwani wapanga kumwengua meya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Madiwani wapanga kumwengua meya


Na Suleiman Abeid, Shinyanga

BAADHI ya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Manispaa ya Shinyanga wanadaiwa kula njama za kutaka kumuengua Meya wao
, Bw. Gulam Mukadam wakimtuhumu kwa kosa la kubadili kinyemela wajumbe wa kamati za kudumu.

Imedaiwa kuwa kutokana na maamuzi yake hayo, madiwani hao hivi sasa wanajiandaa kupiga kura za kutokuwa na imani naye katika kikao kijacho cha baraza kinachotarajiwa kufanyika Januari 29, mwaka huu ambapo kura hiyo ikifanikiwa meya huyo ataondolewa katika wadhifa huo.

Kwa mujibu wa habari za uhakika zilivyolifikia gazeti hili mjini hapa, hatua hiyo ya madiwani wa CCM inatokana na kuenguliwa kwa baadhi ya wajumbe wawili (majina yao tunayo) katika kamati za ardhi na ile ya miundombinu, uamuzi ambao unadaiwa
kuwaudhi madiwani husika.

Imedaiwa kuwa ili hatua hiyo iweze kufanikiwa tayari baadhi ya madiwani hao wameanza kukutana na wenzao wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kwa lengo la kuwaomba wawaunge mkono katika kusudio lao hilo.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mstahiki Meya Gulam Mukadam alisema hakuwa na taarifa juu ya kusudio hilo lakini pia alikiri kufanya
mabadiliko katika baadhi ya wajumbe wa kamati ndogo kwa kuzingatia kanuni za manispaa.

“Kwa kweli sina taarifa kama wenzangu wemepanga njama za kutaka kunikataa kwa njia ya kunipigia kura za kutokuwa na imani na mimi, lakini ukweli ni kwamba nilichokifanya ni kwa mujibu wa kanuni zetu za Manispaa.

“Tumelazimika kufanya mabadiliko katika baadhi ya kamati zetu ndogo hii ni baada ya kubaini kufanyika kwa makosa wakati tulipokuwa tukiwateua wajumbe wa kamati hizo, kamati ya ardhi ina wajumbe wawili, lakini ni lazima suala la jinsia lizingatiwe.

“Awali sisi hilo hatukuliona, tuliweka wajumbe wanaume pekee, ilibidi tubadili, maana tungepeleka majina ya wanaume watupu kwa waziri angetushangaa, lakini pamoja na kumbadili huyu diwani (anamtaja jina) bado nilimfuata na kumuomba radhi, na
nilimweleza sababu iliyosababisha tumbadilishe,” alieleza Bw. Mukadam.

Alisema mabadiliko ya diwani mwingine katika kamati ya miundombinu yalitokana na umuhimu wa kamati hiyo kwa vile mambo mengi yanahitaji watu wasomi ambapo pia naye alielezwa kuhusiana na mabadiliko hayo akakubali.

“Kwa kweli nitashangaa kama hawa wenzangu watachukua uamuzi huo, itakuwa ni aibu kwa
CCM maana kikao kijacho ndiyo kitakuwa kikao chetu cha kwanza cha kufanya kazi, leo wananchi wakisikia tumeanza na malumbano watatushangaa hawatatuelewa,” alieleza Bw. Mukadam.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Shinyanga, Bw. Festo Kang’ombe alisema hakuna taratibu zilizokiukwa katika uteuzi wa wajumbe wa kamati za kudumu katika
manispaa yake na kwamba kila diwani anapaswa kuwa katika moja ya kamati za kudumu na siyo kwa kamati ndogo.

“Ni kweli kuna mabadiliko madogo yamefanyika, na hii ni kwa mujibu wa kanuni za manispaa, meya anayo fursa kwa mujibu wa kanuni hizo kuchagua diwani gani awe kwenye kamati ipi, lakini kila diwani ni lazima awe katika katika moja ya kamati za kudumu,” alieleza Bw. Kang’ombe.

Baadhi ya wanachama wa CCM waliozungumza na Majira
jana wameelezea kushitushwa kwao na hatua hiyo ambapo wamedai inachangiwa na hali ya kutokuelewana kutokana na makovu ya uchaguzi mkuu uliomalizika hivi karibuni.

Mapema wiki iliyopita mmoja wa wenyeviti wa kata wa CCM, Bi. Rehema Nhamanilo alilazimika kujitoa kwenye chama hicho kwa madai ya kuchoshwa na tuhuma zilizokuwa zikitolewa juu yake na wana-CCM wenzake akidaiwa kukihujumu wakati wa uchaguzi.

 

Akizungumza na gazeti hili jana, Mstahiki Meya Gulam Mukadam alisema hakuwa na taarifa juu ya kusudio hilo lakini pia alikiri kufanya
mabadiliko katika baadhi ya wajumbe wa kamati ndogo kwa kuzingatia kanuni za manispaa.

"Kwa kweli sina taarifa kama wenzangu wemepanga njama za kutaka kunikataa kwa njia ya kunipigia kura za kutokuwa na imani na mimi, lakini ukweli ni kwamba nilichokifanya ni kwa mujibu wa kanuni zetu za Manispaa.

"Tumelazimika kufanya mabadiliko katika baadhi ya kamati zetu ndogo hii ni baada ya kubaini kufanyika kwa makosa wakati tulipokuwa tukiwateua wajumbe wa kamati hizo, kamati ya ardhi ina wajumbe wawili, lakini ni lazima suala la jinsia lizingatiwe.

"Awali sisi hilo hatukuliona, tuliweka wajumbe wanaume pekee, ilibidi tubadili, maana tungepeleka majina ya wanaume watupu kwa waziri angetushangaa, lakini pamoja na kumbadili huyu diwani (anamtaja jina) bado nilimfuata na kumuomba radhi, na
nilimweleza sababu iliyosababisha tumbadilishe," alieleza Bw. Mukadam.

Tatizo hapa ni je ulitafuta ridhaa ya kikao hicho ambacho kilifanya makosa katika uteuzi wa kamati tajwa au ulijichukulia sheria mkononi?
 
Mapinduziiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii???.......halafu wao wenyewe wanajijibu''daimaaaaaaaaaaaaaaa''sasa wanamlaumu nini?
 
Hii ni nzuri lakini kama amefuata kanuni na wale wanataka kumuengua tu kwa sababu nafasi zao zimechukuliwa na wengine basi huo utakuwa uroho wa madaraka na si kwa faida ya wananchi. Yaani, wanasiasa wa TZ hasa wa CCM wanaangalia sana maslahi binafsi kuliko maslahi ya wananchi na mustakabali wa nchi kwa ujumla.
 
ni aibu tupu. pengine anajaribu kulipa fadhila huyo bwana kwa waliomfikisha hapo; mafisadi???????
 
Lakini kama Kamati ziliundwa kwenye kikao, hiyo mamlaka ya kubadilisha peke yake anaitoa wapi? That is autocracy!
 
Wampige chini tu hana maana hata kidogo,huu ni wakati wa kubwagana tuu,hakuna sababu ya kuwavumilia wajinga!!
 
Back
Top Bottom