voicer
JF-Expert Member
- Jul 13, 2020
- 5,553
- 11,885
Ni jana tu nimetoka kukuasa kuhusu kupambana na TEC kwa kutumia wadhifa wako wa u-waziri wa habari nchini.
Ukaenda kupiga marufuku ukiwazuia wahariri wa vyombo vya habari ili kutorusha maudhui au kuchapisha maandiko yoyote yanayohusu Waraka wa maaskofu wa "TEC". Kuhusiana na DP-WORLD kuhusu Bandari zetu nchini.
Leo hii inakuja habari ya wewe kukataliwa na machifu na wazee wa kikabila huko Chiponda -Londo.
Kwamba huna asili ya huko bali wewe ni Mnyiramba toka Singida na umekulia Misungwi-Mwanza.
Asiyesikia la mkuu.....
Huu ni mwanzo na ni mfano hai.mengi yatafuata kwa wenzio na kwa njia tofauti.
Pia soma..
Tetesi: - Kimenuka Mtama: Nape akatisha shughuli za Serikali na kuitisha mkutano wa hadhara
Pia ieleweke hivi:
Asili ya mama mzazi wa Nape ni mkoa wa Singida, yeye ni Mnyiramba.
Baba mzazi wa Nape ni Moses Nnauye (marehemu) ambaye alistaafu utumishi wa umma akiwa Brigedia Jenerali wa Jeshi. Asili ya baba yake Nape ni mkoa wa Lindi, yeye ni Mmakonde wa Chiuta, Nyangamara. Mzee Nnauye ni mmoja kati ya wanasiasa mashuhuri wa kizazi kinachoondoka, kazi yake ya kwanza ilikuwa ni “ukuli” wa bandari ya Lindi na Mtwara. Baadaye alisoma kidogo na kushiriki kwenye harakati za kudai uhuru akiwa kijana mdogo na baada ya Uhuru alikuwa kiongozi wa Umoja wa Vijana wa Tanu.