"The anticipation of death can be worse than death itself"Leo hii madereva wa mabasi ya kwenda mikoani wamegoma, mpaka sasa hivi hamna basi lolote lililoondoka katika stendi kuu ya Ubungo. Hii ni kutokana na adhabu iliyotolewa kwa dereva aliyekuwa akiendesha basi la Mohamed Trans lililopata ajali baada ya kupasuka gurudumu la mbele. Dereva huyo alihukumiwa kifungo cha miaka thelathini jela.
Jamani Tanzania tunaelekea wapi. Dereva miaka 30, mafisadi wanapeta...
Kulikoni?...
Hao madereva hawatumii comon sense..wanawasababishia hasara maboss wao.Wanafikiri wapo peke yao wenye uzoefu wa kuendesha magari?
Kama kuna uwezekano wenye ma-bus wawaajiri watu wengine kwa sababu hawapo peke yao,i think hii inaweza ikasaidia..Na kama wataleta fujo sheria ichukue mkondo wake.
du ila jamaa wanamsimamo mkali sana, kugoma watu wote si kitu raisi hasa kwa tz,
yaani leo ubungo ilikuwa mshikemshike.we acha tuuu
Pia hatuwezi kulinganisha kesi ya ufisadi na utoaji wa roho za watu, uizi na ubadilifu wa mali ya uma ni ufisadi ambapo vyote vinaweza kutafutwa ila roho ya mtu ikishapotea utaitafuta wapi?
. Kifungu ni Skendo la Richmond amabapo Luwasa aliwajibishwa kutokana na Utendaji mbovu wa watendaji wake. Pia Mwinyi alijiuzuli akiwa waziri wa mambo ya ndani kutokana na utendaji wa askari wake.
Nawasilisha hoja
uwe unafikiri kabla ya kuweka post au comment hapa...wewe na hao wenzio wanaocha mifiadi ya EPA bila kuifunga jela ,wanaishia kuagiza madereva wapewe adhabu kali...yaani umeona wapi dereva anataka kuangusha gari makusudi watu wafe..kusababishia hasara hao unaowaita maboss maana yake nini
nawapongeza jamaa kwa mshikamano wao, kama waTZ wote wangekuwa na mshikamano kiasi hichi basi tungefika mbali....Miaka 30 ni mingi sana ukiangalia kuwa uzembe si wa madereva tu bali pia ni barabara, trafiki polisi na wenye mali kutojali hali ya mabasi yao!!
nasikia madreva wamelowanisha mustendi!
hahahahahahahaha
Maneno makubwa haya ndugu yangu. Umenifanya niiangalie hoja kama ilivyo. Ni kweli madereva wa mabasi nao wanastahili kabisa kupewa mafunzo maana ni wazembe kupindukia. Lakini hata mafisadi nao wanastahili hayohayo maana nao wanaua tuMafisadi wanaua wengi kwa mwendo wa taratibu, Madereva wanaua na kujeruhi wengi kwa mwendo wa spidi kali....
Kutetea maderava wahuni na wauaji waliojaa katika barabara zetu ni sawa tu na kuwatetea mafisadi wahuni na hatari waliojaa miongoni mwetu ambao wengine tunakunywa, kucheza, kusali, kuomboleza na hata kulala nao....
omarilyas
Nafikiri ni dalili ya kuwa hawana imani na mfumo wa sheria. Hivi ile kesi ya Chenge naye si aliua, nasikia kesi yake itaanza kusikilizwa Sept 18. Ajali ilitokea March 27!