Selous
JF-Expert Member
- Jan 13, 2008
- 1,325
- 144
Hapa ni kuzungushana tu; bado hatujafikia mahali pa litigations zinazowahusu wamiliki. Tumekuwa tukiwaadhibu madereva na watu wengine wa pembeni lakini hatujaanza kuwapa criminal hata civil liabilities kwa wamiliki.
a. Ni nani ana jukumu la kuajiri dereva mwenye uwezo, uzoefu na ujuzi wa kuendesha mabasi? Je, tunajua kama huyo dereva alikuwa ni competent? Je kuna standard yoyote ya uzoefu wa mabasi kabla mtu hajaajiriwa?
b. Basi likiwa bovu nani anajukumu la kusimamia matengenezo yake? Ni dereva au mmiliki? Je kuna utaratibu gani wa madereva kutoa taarifa za mabasi yao mabovu na haki yao ya kukataa kuendesha magari mabovu hadi yatengenezwe? Je akilazimishwa na mmiliki kuendelea na safari baada ya kutoa taarifa na ajali ikatokea na yeye akaonesha uthibitisho kuwa alitoa onyo hilo kwanini mmiliki naye asihusishwe?
Ninaamini njia mojawapo ya kuleta uangalifu na kupunguza ajali ni kuhakikisha kuwa wamiliki wa vyonmbo vya usafiri nao kwa namna moja wanabeba mzigo mkubwa wa lawama. Kwa mfano mwenye mabasi ya Mohammed Trans angelimwa faini ambayo ingemsababisha afilisike lingekuwa funzo kwa wenye mabasi kufikiria wao kama wamiliki wafanye nini wasijikute kwenye hali hiyo.
Kwa mtindo wa sasa tunajaribu kutibu dalili tu za tatizo ili kutuliza hisia zetu japo si akili zetu.
This fall under "Does SUMATRA have SAFETY MANAGEMENT SYSTEM? Does SUMATRA Act require any transporter or bus company to have such system?