Madereva wa mikoani wasitisha mgomo wao!

Miaka 30 ni mingi sana ukiangalia kuwa uzembe si wa madereva tu bali pia ni barabara, trafiki polisi na wenye mali kutojali hali ya mabasi yao!!
 
Kwenye mengi mliyosema, machache ya kuchangia sikosi, wazeya kama kuna watu walikua hawaamini kwamba wakuu wameoza hutakuja kufahamu tena mpaka utakapuchimbiwa shimo na tani kibwena za mchanga kuja juu yako.

HUKUMU
Kusema za ukweli hukumu haikuwa fea kwa kuwa jamaa katika ajai hiyo iliyohusisha basi la Mohamed Trans, ilisababisha vifo vya watu wawili. Chanzo cha ajali kuna kundi la ng'ombe lilipita barabarani na jamaa kuamua kuacha njia na kulipeleka gari porini.

UDEREVA
Binafsi nakubali kwamba madereva walio wengi ni wazembe na wasiokuwa na utashi mkubwa, labda ni kwa kuwa alipomaliza darasa la saba hakukuwa na aina nyingine ya kazi ambayo angeweza kuifanya. Kwa bahati mbaya au nzuri ni watu ambao shule iliwashinda kimtindo hivi...?

LAKINI...
Kwani ni yeye dereva wa kufungwa kengele inapotokea ajali? Mbona Vehicle Inspector haguswi? Vipi kuhusu Trafiki aliyeliruhusu gari kutoka kituoni kwa ajili ya ile Tsh. 5000/=, Not to mention mmiliki wa gari ambaye alitoa injini original ya gari na kuweka ya scania.

YOTE KWA YOTE
Mhe. Rais alisema inabidi kuziangalia upya adhabu je hii ndio jinsi tunavyorekebisha tabia hizo?

Kwakua kila mtu aliyetajwa hapo juu anakwepa kuwajibika tunakwenda kumkandamiza yule aliyepewa leseni bila kuthibitika kwamba anaakili timamu, amefuzu ipasavyo na aliyechukua gari bovu na kuliweka barabarani kwa kuwa ananjaa na anahitaji watoto wake waendelee na waende ******.

Yote kwa yote nasema ahsanteni japo neno hili halina maana tena siku hizi.

Pamoko
 
mi nadhani tatizo liko ndani zaidi kuliko issue ya madereva wa mabasi kuspeed.

though i stand to be corrected but nak8uumbuka kuna kipindi kulikuwa na kamata

kamata ya mabasi yaliyoundwa kwa kutumia engine za fuso. kwa wenye utaalamu gari iliyotengenezwa kwa ajili ya kubeba mizigo ikabeba abiria si lazima iwe nyepesi sana? ni vizuri mamlaka husika zikashughulikia kwanza hili as phase one of the move to curb road accidents.
 
Miaka 30 jamani sio mchezo serikali lazima ifikirie mara mbili kwani tatizo pia lipo kwenye barabara zenyewe zina bamps kibao kila siku gari ina pita ina regeza sana nut na bolt za gari zenyewe. mimi nafikiri hao madereva kogoma sio solutions ya kuwa mwenzao kutoka warudi na wakaae na serikali waangalie tena hiyo adhabu. ila narudi tena kwa serikali kuna majambazi na wahalifu wengine hawapewi miaka kama hiyo kwanini ?
 
Leo hii madereva wa mabasi ya kwenda mikoani wamegoma, mpaka sasa hivi hamna basi lolote lililoondoka katika stendi kuu ya Ubungo. Hii ni kutokana na adhabu iliyotolewa kwa dereva aliyekuwa akiendesha basi la Mohamed Trans lililopata ajali baada ya kupasuka gurudumu la mbele. Dereva huyo alihukumiwa kifungo cha miaka thelathini jela.

Jamani Tanzania tunaelekea wapi. Dereva miaka 30, mafisadi wanapeta...
Kulikoni?...
"The anticipation of death can be worse than death itself"
 
Hao madereva hawatumii comon sense..wanawasababishia hasara maboss wao.Wanafikiri wapo peke yao wenye uzoefu wa kuendesha magari?
Kama kuna uwezekano wenye ma-bus wawaajiri watu wengine kwa sababu hawapo peke yao,i think hii inaweza ikasaidia..Na kama wataleta fujo sheria ichukue mkondo wake.

uwe unafikiri kabla ya kuweka post au comment hapa...wewe na hao wenzio wanaocha mifiadi ya EPA bila kuifunga jela ,wanaishia kuagiza madereva wapewe adhabu kali...yaani umeona wapi dereva anataka kuangusha gari makusudi watu wafe..kusababishia hasara hao unaowaita maboss maana yake nini
 
Pia hatuwezi kulinganisha kesi ya ufisadi na utoaji wa roho za watu, uizi na ubadilifu wa mali ya uma ni ufisadi ambapo vyote vinaweza kutafutwa ila roho ya mtu ikishapotea utaitafuta wapi?

. Kifungu ni Skendo la Richmond amabapo Luwasa aliwajibishwa kutokana na Utendaji mbovu wa watendaji wake. Pia Mwinyi alijiuzuli akiwa waziri wa mambo ya ndani kutokana na utendaji wa askari wake.

Nawasilisha hoja

Umefulia Mkubwa!Chenge yuko wapi?Ukiwaona Ditopile Wamzuzuri walimfanyaje? Ufisadi unaona sio dili kabisa mkubwa,dawa za malaria zinauzwa sh ngapi? Nenda pale Kibiti helthcenter hamna ALU wala panadol,wajawazito wanakufa kila siku (578 )
Bado watoto under fives,kwa watani Kigoma full vibatari,Wenyewe wakiumwa sauzi,india au kwa bibi(UK).
Natamani nikulaani,ila sina uwezo.
 
uwe unafikiri kabla ya kuweka post au comment hapa...wewe na hao wenzio wanaocha mifiadi ya EPA bila kuifunga jela ,wanaishia kuagiza madereva wapewe adhabu kali...yaani umeona wapi dereva anataka kuangusha gari makusudi watu wafe..kusababishia hasara hao unaowaita maboss maana yake nini

Nadhani unafahamu kama hawa madereva wanakatazwa kuendesha gari kwa mwendo wa kasi!
Angalia nchi za nje,wao wanapangiwa kabisa speed wanayotakiwa waende kwa saa,na atakayekiuka kufanya hivyo adhabu kali hutolewa dhidi yake,na hiyo husaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza ajali kwenye nchi zao.
Tanzania isipochukua hatua mnalalamika,sasa mtu kachukuliwa hatua tena mnaanza tena kulalamika!!!Mtu gani wewe usiyekuwa na uelewa na kukubaliana na hali iliyotokea?!
Think twice before you say!
Mafisadi kama wameshindwa kufuatiliwa hiyo ni issue nyingine,here we are talking about madereva waliogoma..!
 
Lakini inauma kuona Chenge anatanua mtaani na ili hali aligonga na kuua. Bora DITTO mungu aliona asifike mbali lakini serikali ya JK ilisha mkingia kifua.
 
Miaka 30 ni mingi sana ukiangalia kuwa uzembe si wa madereva tu bali pia ni barabara, trafiki polisi na wenye mali kutojali hali ya mabasi yao!!
nawapongeza jamaa kwa mshikamano wao, kama waTZ wote wangekuwa na mshikamano kiasi hichi basi tungefika mbali....

dereva kufungwa miaka 10 tu ni mingi, sembuse 30....
kuna mwalimu kafungwa miaka kibao kwa kuchukua hela mbuzi wakati jamaa wa epa wanatembea
justice please, hata dereva wanatakiwa wapewe haki yao
hawa viongozi wanatafu cheap publicity kutoka kwa wananchi kwa kuadhibu watu wengine sana ili waonekane wanafanya kazi
 
Mafisadi wanaua wengi kwa mwendo wa taratibu, Madereva wanaua na kujeruhi wengi kwa mwendo wa spidi kali....

Kutetea maderava wahuni na wauaji waliojaa katika barabara zetu ni sawa tu na kuwatetea mafisadi wahuni na hatari waliojaa miongoni mwetu ambao wengine tunakunywa, kucheza, kusali, kuomboleza na hata kulala nao....

omarilyas
Maneno makubwa haya ndugu yangu. Umenifanya niiangalie hoja kama ilivyo. Ni kweli madereva wa mabasi nao wanastahili kabisa kupewa mafunzo maana ni wazembe kupindukia. Lakini hata mafisadi nao wanastahili hayohayo maana nao wanaua tu
 
Hapa ni kuzungushana tu; bado hatujafikia mahali pa litigations zinazowahusu wamiliki. Tumekuwa tukiwaadhibu madereva na watu wengine wa pembeni lakini hatujaanza kuwapa criminal hata civil liabilities kwa wamiliki.

a. Ni nani ana jukumu la kuajiri dereva mwenye uwezo, uzoefu na ujuzi wa kuendesha mabasi? Je, tunajua kama huyo dereva alikuwa ni competent? Je kuna standard yoyote ya uzoefu wa mabasi kabla mtu hajaajiriwa?

b. Basi likiwa bovu nani anajukumu la kusimamia matengenezo yake? Ni dereva au mmiliki? Je kuna utaratibu gani wa madereva kutoa taarifa za mabasi yao mabovu na haki yao ya kukataa kuendesha magari mabovu hadi yatengenezwe? Je akilazimishwa na mmiliki kuendelea na safari baada ya kutoa taarifa na ajali ikatokea na yeye akaonesha uthibitisho kuwa alitoa onyo hilo kwanini mmiliki naye asihusishwe?

Ninaamini njia mojawapo ya kuleta uangalifu na kupunguza ajali ni kuhakikisha kuwa wamiliki wa vyonmbo vya usafiri nao kwa namna moja wanabeba mzigo mkubwa wa lawama. Kwa mfano mwenye mabasi ya Mohammed Trans angelimwa faini ambayo ingemsababisha afilisike lingekuwa funzo kwa wenye mabasi kufikiria wao kama wamiliki wafanye nini wasijikute kwenye hali hiyo.

Kwa mtindo wa sasa tunajaribu kutibu dalili tu za tatizo ili kutuliza hisia zetu japo si akili zetu.
 
Nafikiri ni dalili ya kuwa hawana imani na mfumo wa sheria. Hivi ile kesi ya Chenge naye si aliua, nasikia kesi yake itaanza kusikilizwa Sept 18. Ajali ilitokea March 27!

Hizi sheria zetu za matabaka mawili nazo zinaudhi sana. Sheria za Vingunge na sheria za Makapuku. Huyo huyo Chenge anahusika pia kujipatia pesa kifisadi katika ununuzi wa rada lakini hadi leo hata kuchunguzwa na vyombo husika vya dola hakuna! bado anapeta tu uraiani bila hata kuguswa labda vile alivyonyunyiza ndani ya Bunge ndiyo vinafanya kazi yake.
 
Madereva kugoma si solution serikali ina nguvu na abiria hawakupaswa kunyanyaswa kwa hali yoyote ile. Wangetakiwa kuchukua hatua zinazokubalika katika taratibu za kistaarabu
 
Mfikirie pia katika ajali hizo hizo wanazozisababisha kuna wanaovunjika miguu,mikono pia wapo wanaofariki papo hapo na most of them ni tegemezi katika familia zao...!Watoto wengi hubaki mayatima kutokana na ajali hizohizo...
Adhabu itakapotolewa kwa mmoja,wengine nao wanaweza wakajifunza na kupunguza hizo ajali barabarani.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom