Majala Kimolo
JF-Expert Member
- Aug 3, 2007
- 342
- 39
Labda zimezidi mno. Utaratibu unaofaa ufuatwe. Madereva waliogoma wamekosea. Si abiria waliomhukumu huyo dereva. Kama hujui uzito wa hilo waulize wafiwa na mayatima waliokatishiwa ustawi wa maisha yao na ajali ile tena miaka zaidi ya 30 ya hukumu aliyopewa huyo dereva. Kama wanaodai wanampenda wana haki ya kukata rufaa kwenye mahakama za juu. Mashahidi wapo watasema waliona nini katika ajali hiyo. Alistahili hukumu hiyo kwa mujibu wa mwenendo wa kesi katika mahakama ile.