Igangilonga
Senior Member
- Mar 11, 2006
- 133
- 27
Mimi kuhusu Vincent sina uhakika sana, ila huyo mhindi pia kajitahidi this time jamani ingawa mimi nawafagilia Wababa, Nsami na Walter
we unafauatilia vipind gan visivyo vya kijinga?taja vitatu tu
Hebu kuweni fair, yaani Vincent anarudishwa nyumbani na Salma (mpiga-gita)anabaki hata bila kuingizwa danger zone huku mama Rita anasema hakuna kama huyo na master J anakenua meno tu wakati taaluma inanyewa hivi hivi?
Sipendi kuamini kuwa kuna watu wameandalia ushindi siku nyingi lakini mkiendelea na upuuzi huu sisi wapiga kura tutaanza kuwapigia ninyi kura za kukosa imani nanyi. Angalia mlivyombeba yule Salma (mhindi) amewashinda kubeba mgongoni mwishoe mmeamua kumbwaga kwa uchungu sana. Huyo hakustahili hata kuingia BSS 21 bora, ni dada anaye temea mate tu kwenye kipanza sauti na sauti ya kuua ngoma za masikio ya watu.
As for Salama Jabir huwa hatumchukulii serious maana inategemea kaamkaje na nani kampa kaneno ka kumzuzua perfomer. Lakini kwa Master J (mtaalam wa muziki) na Madam Rita (Chief Judge) angalieni sana mnahatarisha biashara yenu, maana siku za usoni hakuna atakayetoa udhamini kwa kuwa na upendeleo wa wazi namna hii.
Sikilizeni, mimi simfahamu yeyote katika washiriki lakini nawashauri kuwa hivi nyote watatu kaeni mahala m-playback episode ya Jumapili 07/10 mumsimilize Vincent as compared to the others Wavulana kwa wasichana (mtaona Kijana ana sauti ya mvuto, kaimba vizuri, good choice of song with a lot of feelings, anatawala steji, anaimba mistari ya kutosha sio kama wengine wanaimba kidogo tu halafu kudance na kuchombeza viungo yaaa!! yeeee!! n.k. Yaani hata ingawa Wababa namkubali lakini kwa episode ya Jumapili alifunikwa na Vincent maana alikuwa na wimbo wa kubore na hakuna cha maana cha kumsifia kwa siku hiyo na ndivyo ilivyokuwa kwa wengine wachache ambao hakika walikuwa off tune na wamewekwa tu danger zote.
Msibweteke na jina la mtu au alifanya vipi mwanzoni, toeni comments za ukweli kufuatana na performance ya siku hiyo! dada mpiga gitaa anaweza kuwa musician kwa kuweza kuchalaza nyuzi lakini kwa sauti na hata kutamka maneno hawezi anaumauma maneno na anaimba sauti isiyo na mvuto tena yenye pitch ya chini sana kila siku na kujificha chini ya kivuli cha usanii. Naye mumsikilize yeye toka episode ya mwanzo mtaliona hili waziwazi na mtaona aibu kwa kumsimamia na kumsalute wakati ni mweupe.
The more you stand for professionalism, truth & fairness, the more we shall support this Epiq BSS-programme & Benchmark production Ltd.:A S embarassed:
Siku walipomtoa huyu binti na mimi nikafunga milango ya kuangalia hicho kipindi chao. Kwa kweli ingekuwa enzi zile za "Klabu Raha leo Shoo!" sidhani hawa wakina Salama wangepewa hata mic wazungumze. Ndiyo maana mpaka leo nakumbuka enzi zile za "Misakato" na lile gita la solo lililopigwa kwenye sebene la Msondo Namba 5.Ni kweli kabisa mkuu mimi toka walipomtoa rossemerry mpangala nikaona hapo kwenye ujaji kuna walakini na wala sioni kigezo cha kumpa ujaji huyo salama muziki wenyewe haujui kazi kutusi watu na kuongea upuzi tu hana hata aibu na huyo rita angewapisha watu wenye taaluma ya muziki akabaki kuwa mmiliki tu wa bss kweni lazima nae awe jaji au ndio mambo ya uuza sura hana uweledi kabisa huyo ni mlevi tu salama mabangi
kumbe hili shindano lipo? Chanel gani na saa ngap wakuu....?
hii kitu naona wamewaiga x factor maana na kwenyewe kule mambo sio mambo last time yule ma favorite alikuwa astro & chris rene naona wakawababia wakamchukua yule dada aliyekuwa kwenye audition ya florida
Sijawahi kuona hicho kipindi.