Nina Deni la Maisha

Robert Heriel Mtibeli

JF-Expert Member
Mar 24, 2018
21,340
51,900
NINA DENI LA MAISHA

Anaandika, Robert Heriel Tz

Leo upo Msiba wa Bibi yangu ambaye jina langu limetoka Kwa Mume wake(Babu yangu).

Wale waliotujua Kabla hatujajulikana, walitupa, wakatupa tukakosa cha kuwalipa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Hatukuweza kufidia upendo wao. Hata ingepita Miaka Elfu moja na moja kamwe tusingeweza kulipa Deni😭😭 Limekuwa Deni naam Deni la Maisha.

Tulilelewa na Wazee, hiyo kwetu ilikuwa ni bahati iliyonjema. Ingawaje Ipo Ile kasumba isemayo kuwa Watoto waliolelewa na Bibi na Babu wanaharibika lakini dhana hiyo ingepoteza ukweli wake pale ambapo ungekutana na Mimi, naam ndimi Taikon.

Nilijipata na Akili nikiwa mikononi mwa Ukoo mkubwa uliobarikiwa, naam ndio Ukoo wa Tenga, ukiwa na idadi ya ajabu labda niseme utajiri mkubwa wa Wazee, sio kila mtu kwenye Maisha anabahati ya kuwaona Babu na Bibi zake, lakini kwangu ilikuwa bahati kubwa kujikuta katikati ya wakubwa wenye umri wa miujiza ambao ni nadra Sana kufikiwa katika kizazi Hiki.

Kuwa katika ukoo wenye Mabibi na Mababu wasiopungua 18 sio Jambo la kubeza, Huku Bibi mzaa Mama yangu akifunga Dimba katika mnyororo wa viuno vya ukoo huo Kwa upande wa Mke Mkubwa wa Baba Yao.

Kuishi na Wazee kulinisaidia kujifunza mambo mengi Mno, hasahasa busara na hekima zao. Kuna Wakati Watu wengi hunisifu na kunishangaa Maarifa, ujuzi, ufahamu na Elimu niliyonayo ambayo huwatatiza kwani umri wangu ungali hauendani na yale niliyonayo kichwani. Lakini ukweli ni kuwa Malezi ya wazee na mazungumzo yao ndio yamechangia Kwa kiasi kikubwa vile nilivyo.

Kuishi na Wazee kunakufanya uheshimu Watu. Lakini kamwe sikufundishwa heshima ya woga au unafiki.
Nilifundishwa kuheshimu wastahilio heshima, kuwafunza waliokengeuka.

Nilifundishwa na kujifunza heshima lakini heshima ya Kweli, wala sikufundishwa kuwa mwoga na Mnafiki, Bali nilifundishwa kuwa na heshima ya Kweli. Haitokuchukua muda kung'amua kuwa Taikon Kwa kiasi kikubwa ametawaliwa na mawazo ya kizamani, naam nimetaliwa na mawazo hayo Kutokana na malezi ya Wazee.
Ninaamini katika Uafrika, heshima Kati ya Mkubwa na Mdogo, mipaka baina ya Mwanamke na Mwanaume, mila, desturi na miiko Kwa kweli bado vinanisumbua kichwani. Sifikirii kubadili mtazamo Kwa sababu mfumo wa Wazee bado naona upo Relevant,

Pichani hapo ni Bibi zangu Wawili ambao wanamchango mkubwa katika Maisha yangu. Kama kingeandikwa kitabu cha Historia ya Maisha yangu basi majina ya Mabibi hao lazima yangejitokeza mara kadhaa. Hii ni Kutokana na mchango wao katika Maisha Yangu. Wapi walipowaume zao, Hilo msijali, msije mkasema ninawapendelea zaidi Wanawake lakini ni hakika Mwanamke ni kiumbe kilichopendelewa, upendo na hata upendeleo vipo kwaajili Yao. Hivyo Wazee wangu, Baba zangu, na wajomba zangu mtaniwia radhi, hata nanyi mnaelewa.

Jina langu "Robert" linatokana na Huyo Bibi Mrembo mweupe aliyemkono wa kushoto Kutoka kwetu watazamaji, ambaye jina lake ni Lightness Mwanahawa Robert Kalalu Tenga. Urefu wa jina lake lisikuchanganye, Robert Kalalu ndiye aliyekuwa Mume wake, na Mimi ndiye niliyemrithi jina Hilo, Hii ni kusema kijadi Mimi ni Mume wa utani wa Bi. Lightness Mwanahawa Robert Kalalu.

Pembeni yake katika picha ni mdogo wake Lightness, naye ni Black beauty Nasemba Hilary Heriel chambua Tenga Kikunte ambaye ndiye kamzaa Mama Yangu. Mpaka hapo unaweza kuona ni namna gani ilivyongumu kuandika Historia yangu bila kuwataja hawa malkia Wawili.

Kuna miti na mitishamba, sio kila mti unaweza kuwa mtishamba, hayo nilikuja kuyajua katika makuzi yangu pale nilipokuwa nikipitiwa mara kadhaa na Bi. Lightness ili twende shamba kuchuma Dawa. Nilikuwa mdogo nisiyedharau jambo lolote lenye uhusiano na Elimu na maarifa ya Jambo lolote. Sasa Bi. Lightness alikuja na Elimu na ujuzi, na maarifa ya miiti na Mimea Kwa kile alichokiita ni kuwa ni Dawa.

Tulichuma majani, tukakwangua magome ya miti, tukatunda matunda na mbegu, na hata kuchimba mizizi ya miti tukitafuta Dawa.

Mara Kwa mara nilikuwa namsikia Bibi akitaja magonjwa fulani Fulani ambayo hata mengine sikuwa nayafahamu Kutokana na umri wangu mdogo, mathalani, Chango la Uzazi, ngiri, mimba kuchomoka miongoni mwa magonjwa mengine. Magonjwa niliyokuwa nayafahamu ni pamoja na Malaria, Typhoid, homa, mafua na kikohozi, pia magonjwa kama kisukari na presha nilikuwa namsikia akiyataja.

Na hiyo huja Baada ya kuona mmea fulani, basi ananionyesha na kuniambia, unaona ule mti au ule mmea, hapo nitautazama kisha akishathibitisha nimeuona, akijua nasubiri maelezo yake, ananiambia mmea ule majani yake au mzizi wake ni Dawa ya ugonjwa Fulani.

Niliiona Ari yake na shauku yake ya kuhamisha ujuzi na maarifa Kutoka katika Akili yake kuja katika Akili yangu, nakumbuka! Bila Shaka alijua Wakati wake umepungua na Sisi kama kizazi kichanga tunahitaji kujua Elimu na ujuzi ule.

Sikuweza kushika Mimea yote, hilo kwangu ninaweza kujilaumu na kujiona kama mwanafunzi niliyekuwa mzembe,Ilikuwa fursa ya thamani iliyokuja Kwa Njia rahisi na nafasi ya Bure lakini sikuweza kuitumia kama ilivyostahili.

Hata hivyo Kwa kiwango cha Chini ninajivunia Kwa sehemu ndogo kwani bado ninakumbukumbu ndogo Kwa baadhi ya Mimea.

Nilikuja kugundua kuwa nimechezea bahati miaka Kumi iliyofuata Wakati nipo CHUO, hapo nilipokutana na matangazo ya biashara ya madawa ya mitishamba katika redio, Luninga na magazeti huku mitaani nikiona baadhi ya Watu wakiteseka na magonjwa. Ilikuwa fursa! Ndio ningeitumia fursa hiyo kama ningehitimu masomo ya utabibu kw kutumia mitishamba Kwa Njia ya jadi. Ningeisaidia jamii hapohapo ningejipatia kipato.

Bibi yangu hakuwa na Elimu kubwa lakini kiwango kile cha ufahamu na ujuzi wa madawa kama ningehitimu alafu nikaongeza na Elimu ya Kisasa niliyonayo nafikiri ingekuwa Jambo kubwa lenye maana. Lakini hiyo imekuwa hadithi ya "ninge" ninge" ambayo huja mwishoni kama majuto.

Nilichezea nafasi ya muhimu, nili-score Chini ya kiwango katika eneo hilo labda kama ni matokeo basi ningekuwa nimepata Grade C tuu.

Nyuma ya picha hiyo ni kabati kubwa ambalo lilisheheni makopo mengi yenye Dawa za kila namna.

Mara kadhaa tulipoenda Kwa Bi. Lightness Kwa aidha kuchukua Dawa, au kusalimia, au kutengeneza Dawa, au kuchukua Asali, au maziwa kwani Bibi na Babu Kalalu walikuwa na Ng'ombe WA kienyeji waliokuwa wanafuga, mara kadhaa tulikuwa tunamkosa, hakuwepo nyumbani, alienda Kanisani kuimba, ATI mazoezi ya Kwaya, hahahaha! Bibi Bhana! Alipenda Sana kuimba. Sijui na sidhani kama nakumbuka alikuwa akiimba Sauti ya ngapi lakini ninachokumbuka alikuwa akipenda kuimba Sana.

Natamani kama ungekuwa mahali pale akiwa anaimba Kwaya akiwa na wenzake, hasa wakiwa wamevaa majoho ya Kwaya yaliyowabadilisha muonekano wao ungedhani ni Makuhani wa walawi nyakati zile za Musa na Torati yake.

Hapo Kabla hawajaanza kuimba macho yote ya waumini na wasiowaumini ambao ni wageni macho Yao yangekuwa yametazama Watu Wawili, mmoja alikuwa ni Bibi. Lightness ambaye alikuwa anambwembwe na madoido yenye utukufu wa ajabu, Yule wapili alikuwa ni mwimbishaji wa Kwaya aliyesimama Mbele ya wanakwaya akichezesha mikono huku na huku na kujitingisha Kwa mitindo yenye Mvuto wa kizamani ambao Kwa sasa ni nadra Sana kuiona.

Alipenda Sana kuimba, lakini hiyo kwangu haikuwa na maana yoyote Ile, sikuona kama ingenisaidia ingawaje Kutokana na hulka yangu ya kupenda habari na kuunda visa na mikasa labda niseme alikuwa muhimu katika kazi yangu ya kuhifadhi kumbukumbu ya visa Kwa Njia ya maandishi.

Vitoto vingi vilipenda kufika Kwa Bibi Lightness, kila mtoto kwake alimuita Bibi, naye aliviona kama vijukuu vyake ingawaje vingi vingine havikuwa hata na undugu wa kinasaba. Ukarimu wake wa kuwapa chakula, au maziwa ndivyo vilifanya Watoto wa Kutoka Maeneo mbalimbali kufika hapo nyumbani kwake.

Sijasahau kitu kingine kikubwa kiliichompa umaarufu mkubwa pale Kijijini kwetu, hata ningeitwa Mahakamani hivi leo nisimame kama shahidi, ningesimama kutoa ushahidi kuwa sikuwahi kuona Asali tamu kama Ile iliyokuwa ikitengenezwa na Mzee Robert Kalalu ambaye ndiye nimechukua jina lake. Sega la Asali na Asali yenyewe ya Mzee Kalalu ilikuwa ya kushangaza, nimepata Kula Asali ya tabora, pamoja na Asali ya Rukwa lakini bado hazijafikia Asali ya Mzee Robert Kalalu.

Ilikuwa Asali ya Aina mbili, ilikuwepo Asali yenye rangi ya dhahabu na Ile yenye rangi kama nyeupe Fulani hivi.
Hiyo ndio ilijaza Watoto wengi katika nyumba hiyo licha ya kuwa kulikuwa kulikuwa na Mbwa Wakali lakini hiyo haikuwazuia Watoto kuja kulilia Asali ya Babu na Bibi Kalalu.

Hilo nalo lilikuwa ni pigo jingine Baada ya Mzee Robert Kalalu kufariki bila kutuachia ujuzi wa kufuga nyuki na kurina Asali, achilia mbali kuchonga mizinga.

Utengenezaji wa Asali na ufugaji wa nyuki mbali na kuwa chakula na Dawa lakini pia ni chanzo kizuri cha kimapato ambapo kama ukifanywa vizuri inaweza kusaidia Vijana kujiajiri na kuondoa tatizo la Ajira.

Pia Nyuki ni moja ya wadudu nyeti na walazima katika Uchavushaji wa Mimea katika kuzalisha matunda na mazao pale Maua ya mmea yanapochanua.
Doooh!

Mpaka kufikia hapo machozi ya huzuni yananitoka, kwani muelekeo wa Simulizi hii inaweza kuwa ni majibu ya kile kiitwacho Janga la Ajira linaloendelea kuitafuna Dunia ya Leo.

Ninawaza kama kila kijana au Binti angechukua ujuzi na Elimu na maarifa ya ustadi kutoka Kwa Bibi au Babu yake, basi ni wazi hivi leo kusingekuwa na tatizo la Ajira.

Lakini tuliwaacha wakatulea na tukapuuza kama sio kukataa kujifunza Mambo ya wazee wetu. Na haya ndio Malipo yake.

Mke wangu wa utani wa jadi, ndiye Bi. Lightness Kalalu Jana ndio Tarehe 02/02/2023 amelala naam amafariki akiwa ameshiba siku na miaka ha kutosha, Miaka 90 sio Lelemama.

Nilishawaambia kuwa Bibi na Babu zangu walijaliwa kuishi miaka ya miujiza na maajabu ambayo Kwa Karne ya Leo ni zaidi ya muujiza wa mwamposa kufikisha umri huo. Huku Dada yake aitwaye Zilipa Tenga ambaye ndiye wakwanza kwao katika kuzaliwa akiwa na miaka 100 na yupo hai.

Niliwahi Kupata wasaa WA kuwahoji, sikutaka kuendelea kuchelewa, tayari nilikuwa nimeshapotez maarifa mengi Kutoka kwao. Niliwahi kuwauliza wanipe Siri ya kuishi miaka yote hiyo kana kwamba wanataka waione siku ya kiyama.

Majibu Yao yalifanana ingawaje niliwahoji katika nyakati tofauti kila mmoja akiwa kivyake.

Walinijibu, Siri ya kuishi miaka mingi mpaka kuiona siku ya kiyama, ni kuishi Kwa adabu na nidhamu. Heshimu wakubwa, heshimu kila MTU.

Alafu Siri ya pili, ni Kula vizuri huku ukiepuka unywaji wa pombe kupitiliza.
Mmoja alilifuata sikio langu akaling'ata akisema, Epuka ngono zembe.

Nikasema hivyo tuu, basi na Sura zao zilizozeeka na mikunjo mingi yenye kumbukumbu ya visakale na visasili vya utoto na ujana wao, wakanijibu hivyo tuu.

Halafu Mwisho wakaniambia, Mpende MUNGU kwani yeye ndiye atupaye kuishi.

Pumzika Kwa Amani MKE wangu wa utani wa Jadi, Bi Lightness Mwanahawa Robert Kalalu Tenga,
Nina deni la Maisha ambalo kamwe sitoweza kulilipa.

Ni Yule Mjukuu wa Wazee.

Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam
 
NINA DENI LA MAISHA

Anaandika, Robert Heriel Tz

Leo upo Msiba wa Bibi yangu ambaye jina langu limetoka Kwa Mume wake(Babu yangu).

Wale waliotujua Kabla hatujajulikana, walitupa, wakatupa tukakosa cha kuwalipa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa. Hatukuweza kufidia upendo wao. Hata ingepita Miaka Elfu moja na moja kamwe tusingeweza kulipa Deni Limekuwa Deni naam Deni la Maisha.

Pole sana
 
Poleni kwa kuondokewa na Bibi, apumzike katika Amani! Sijaona picha unayoitolea ufafanuzi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom