PauloKichaa
Senior Member
- Jun 6, 2011
- 122
- 39
Cha uongo kipi alichosema hapo, je si kweli mtoto wa mkulima aiwahadaa ma dr? Na sasa wamemkalia kooni sijui atatokaje, hii ni faida ya serikali isiyo sikivu, wanalazimishwa kufanya maamuzi kwa lazima
Asiishie hapo kuna makopo mengi tu ya kutupa pale, yameshaisha muda wake
mama Nagu
Kawambwa
Mwakyembe (Mgonjwa)
Mwandosya (mgonjwa)
Ngeleja (hayuko serious)
Malima (boza)
Mponda (zero)
Nkya (conflict of interest, useless)
nk
Du hii serikali yetu kwa kweli inasikitisha, kwa wiki nzima sasa kila chombo cha habari kinahabarisha jinsi walimu wapya wanavyoteseka kwa kukosa stahiki zao. Inafikia mwalimu anakosa mahali pa kula na kulala ataweza vipi kufundisha watoto wetu. Madaktari wagome kabisa wasifanye mchezo na serikali ya mazezeta, yamechoka hayana tena jipya isipokuwa kuliangamiza taifa hili la Mungu.
We are praying for you guys!! Ni mwanzo mzuri, hope the teachers will also stop working for CCM during election!! Walimu wanatucost sana, ukiona mtoto wako anafeli feli darasani siyo kwa sababu hana akili ila walimu hawako motivated!! Madaktari tutawatunukia nishani ya ushujaa huku mbele ya safari kwa kulikoboa hili taifa!! msilegee, hawa viongozi wetu hawana huruma na hii nchi!! They travel everywhere, but for nothing! they use money to win their desire! they are ready to kill anyone who go against their will even when is not a public interests. In short, these leaders are not ours but they are puppets.
Imenisikitisha sana niliposikia tamko la madaktari kupitia ITV habari mpasuka kuwa wataendelea na mgomo ikiwa wabaya wao Dr Haji Mponda na Dr Nkya wataendelea kuwepo wizara ya afya kama mawaziri, kwa mjibu wa ITV, madaktari hao wameipa Serikali siku nne hadi Jumatano ijayo saa 2;00 asbh iwe imewaondoa wabaya wao lasivyo mgomo utaendelea. Kwa kauli hii ya madaktari namuomba JAKAYA atumie busara kuchagua kuendelea kumkubatia huyo waziri na naibu wake na watanzania wasio na hatia waendelee kufa kwa vifo visivyo vya lazima ama awatimue ili kuondokana na janga hilo.
Hawa wana-usalama walikuwa wapi siku zote? Nadhani kama wangekuwa wanafanya lazi zao vizuri, kwanza hata huu mgomo usingetokea, na hata baada ya kutokea na kufikia muafaka, walikuwa wapi kufahamu kuwa haya maamuzi ya madaktari lazima yangefika hapa ikiwa kama mambo kama ya kuwawajibisha hao mawaziri hayakufanyika? Napata shida sana na hao wanaoitwa wana usalama, na ninaona pia kuna uwezekano mkubwa kabisa nao wakawa wameingia ktk vita hii ya makundi ndio maana mambo hayaendi.
Kwa vile Serikali imeonekana kulegea kabisa, basi hakuna ujanja ni lazima ipate shinikizo kama hilo ili itoe maamuzi, na kila siku bila mashinikizo Serikali nyingi za Africa zinakuwa hazieleweki. Na kama madaktari watakuja na mashinikizo mengine, sawa tu, ili mradi yana manufaa kwa watanzania.
Pili, ktk kila historia ya mabadiliko, huwa kunakuwa na Agent of Change, na kwa Tanzania, kutokana na historia yetu ya kimaisha na jinsi Mwalimu Nyerere alivyotukuza na kutufunza, sisi wananchi kuwa change agent ni kazi kidogo.
Kwa nchi kama yetu, professions can be agent of change, na hapa nazungumzia fani kama hawa madoctor wetu, walimu na kadharika. Kwa hapa tulipofika, naona kabisa, madaktari wanaweza kuwa agent of change kwa Tanzania.
Mimi nilisema mwanzo na naendelea kusema, nawaunga mkono, nawaomba wabebe jukumu hili la kuwa Agent of change kwa niaba ya watanzania wote, bila kujali itikadi zao. Nawaomba madaktari, wakisha inyosha serikali kwa masuala yaliyopo ktk sector ya Afya, wahamie na sector nyingine kama Walimu nk. Watusaidie kuleta haya mabadiliko, wanaweza kuja na hoja kuwa wao kama madoctor wamefika hapo walipo kwa ajili ya walimu, sasa kama walimu wasipotekelezewa maslahi yao basi wao wanaitisha mgomo tena.
Wakimaliza hapo waje kwa watumishi wazembe na hasa mafisadi Serikalini, waseme, haiwezekani watu wachache watumie rasilimali za nchi kwa manufaa yao pekee, wakati watanzania wengi wanakufa kwa kukosa dawa na hospitali za kutosha, basi waseme wanataka watu wote waliotuhumiwa kwa ufisadi wafukuzwe kazi na wakamatwe na wafikishwe ktk vyombo vya sheria, na waitishe mgomo kama Serikali haitaka kufanya hivyo.
Wakimaliza hapo waende katika sector nyingine, mpaka wamalize zote. Nadhani Madaktari wanaweza kututoa hapa na kutupeleka mahali pengine bila hata kutumia vyama vya siasa.
Tena wanapotoa hayo mashinikizo watoe na timeframe, kama vile wanavyo-prescribe dawa zao kwa mgonjwa, 2X3 kwa Wiki Moja, au 1x1 for two weeks au etc etc. Basi waipe serikali time frame kama dozi za dawa, kama walivyofanya hili la sasa, kwamba mpaka J5 hao mawaziri wawe wameondoka - dozi safi sana kama ya dawa ya siku tatu.
Hongereeni Madaktari na naomba mlifikirie wazo langu la ninyi kuwa agent of change na watanzania tuwape support hawa. Aluta continua!....
wapendwa,
kumbukeni kuwa si kazi ya madaktari wala kada nyingine yoyote kupanga baraza la mawaziri. huko ni kukiuka katiba. watanzania kama jamii ya watu wastaarabu hatupaswi kukiuka katiba yetu wenyewe.
mara nyingi tunawanyooshea vidole viongozi kuwa wamekiuka katiba lakini tunasahau kuwa kila raia anapaswa kuheshimu na kuilinda katiba iliyopo.
hao madaktari wana madai ya msingi, sawa. tena si peke yao. karibu kila kundi nchini mwetu lina madai kadhaa ya msingi kabisa, lakini wasisahau kuwa haki yao ni hayo madai waliyonayo na sio zaidi ya hapo. kumlazimisha mponda , nkya au waziri yoyote atoke kazini ili wao "wafurahi' ni kinyume cha katiba. hao kina mponda ni watanzania kama watanzania wengine na wana haki ya kufanya kazi iwe ni uwaziri au kazi nyingine yoyote, kama walivyo na haki kama hiyo watanzania wengine wote.
mimi binafsi sioni haki wala haja yoyote ya madaktari kugoma kutimiza wajibu wao wa kikazi hadi waone sura wanazozipenda wao kwenye baraza la mawaziri. hiyo si haki ya kikazi kwa kada ya madaktari, labda watuambie wana maslahi gani katika hilo.
hao madaktari wameishaonja "nyama ya mtu", wameishaua wagonjwa waliokwenda kupata huduma yao huku wakiwa wameishakula mishahara na stahili nyingine, iliyotokana na kodi walizotozwa hao hao waliowaua kwa mgomo wao uliopita! na sasa wamezoea harufu ya damu za watanzania wenzao masikini wasioweza kukimbilia india wala hospitali nyingine ghali zaidi za binafsi nchini.
ni wauaji wakubwa na siungi mkono mgomo wao mwingine kwa sababu za eti fulani na fulani bado ni mawaziri au manaibu mawaziri! hiyo si kazi yao, wao wazingatie kazi zao na wapeleke serikalini madai yanayoendana na haki au maslahi yao kama madaktari. hilo la kulazimisha mabadiliko ya baraza la mawaziri ni uhujumu wa kiraia na ukiukwaji wa katiba. imefika wakati sasa katiba na sheria ziseme, raia asiye kiongozi wa umma akikiuka katiba afanyweje.
siungi mkono hoja na nawalaani sana kwa nia na azimio lao hilo (kama ni la kweli)
mbarikiwe sana wapendwa
glory to God!
Blackmailing a president,! chantaje!
sasa mgomo wa madaktari utakua meaningless sabab madai na vitisho vyao sasa vinaboa, mi nawaungamkono katika kudai mishahara na mazingira mazuri ya kazi, wakishapata hivyo tu wafanye kazi watulie, ila wakianzakusema sijui wataachia watanzania wafe kisa tu eti rais hajabadili waziri, it's nonsense! na sio maadili ya kazi alio tuachia Esculapio
Hahaha madokta wanachekesha sana, badala ya kudai mambo yao ya msingi wamekuwa kama chama cha siasa.Rais akiwakubalia madaktari atakuwa ameonesha udhaifu mkubwa sana na next thing watasema pinda hawamtaki naye atoke hakutakuwa na serikali. Ningependa jk aache hao jamaa wagome wakae benchi kwakuwa kimsingi wakigoma wataenda kufanya kazi hospitali binafsi ili wasife njaa.