Madaktari wamuweka JK kikaangoni! Ni kuhusu uamuzi wa kumfukuza kazi Dr Mponda

Status
Not open for further replies.
Hofu yangu naogopa pale mwananchi wa kawaida anaposhindwa kuishi inavyostahili kwa kupata huduma muhimu,hapa hata subiri kauli ya KUOMBA au KUTAKIWA.Kitakachofuata ni kutafuta mbinu za kupata huduma anavyojua mwenyewe bila kufuata sheria.hapo patakuwa pagumu sana kwa watanzania wa kawaida.hima tutafute suluhisho mapema
 
NI NANI MKUBWA? SERIKALI AU WANAHARAKATI, WANASIASA NA MADAKTARI

Wakati Serikali ikitumia kauli ya kistaarabu ya "TUNAWAOMBA Madaktari " Kundi la pili na hasa Wanaharakati wao wamekuwa WAKIITAKA Serikali. Sasa mimi najiuliza hizi nchini yetu inaendeshwa kinyume ? Anayeagiza ndiye anaomba na anyetakiwa kuomba ndiye anayeagiza? Hakika sasa nimeshatambua Nini maana ya msemo "DEMOKRASIA IKIVUKA MIPAKA". Watanzania tutambue kuwa hata kama ili tuendelee kupata misaada toka nje kuendesha NGO zetu ni lazima tupete midomo yetu sana , pia tuna wajibu wa kuheshimu Mamlaka zilizochaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu
Nawasilisha.

Mamlaka zilizochaguliwa huheshimika pale zinapokidhi matarajio ya waliozichagua! kinyume chake huzaa hali tunayoishuhudia sasa!
 
serkali imewekwa na watu ambao ni wewe na mimi,
sasa tuiombe kufanya nini,
yenyewe ndiyo inatakiwa ituombe, kwa hivyo walivyofanya ni
sawa kabisa.
 
NI NANI MKUBWA? SERIKALI AU WANAHARAKATI, WANASIASA NA MADAKTARI

Wakati Serikali ikitumia kauli ya kistaarabu ya "TUNAWAOMBA Madaktari " Kundi la pili na hasa Wanaharakati wao wamekuwa WAKIITAKA Serikali. Sasa mimi najiuliza hizi nchini yetu inaendeshwa kinyume ? Anayeagiza ndiye anaomba na anyetakiwa kuomba ndiye anayeagiza? Hakika sasa nimeshatambua Nini maana ya msemo "DEMOKRASIA IKIVUKA MIPAKA". Watanzania tutambue kuwa hata kama ili tuendelee kupata misaada toka nje kuendesha NGO zetu ni lazima tupete midomo yetu sana , pia tuna wajibu wa kuheshimu Mamlaka zilizochaguliwa kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu
Nawasilisha.
Hii ni sawa katika demokrasia pevu wala hakuna mipaka iliyovukwa!! hapa. Wanaharakati wako kwa niaba ya wananchi. Hivyo wananchi KUITAKA serikali tuliyoiweka madaraka na tunayoilipa kodi zetu ni sahihi kabisa. Mkuu ni kama unamtaka mwajiriwa wako tumia fedha kiasi fulani afanyie jambo muhimu.
Hizo kodi au fedha ni zetu!!! hatuwezi "kuomba" kilicho chetu!! na hao "wanaotakiwa" ie serikali (rais, mawaziri nk)kufanya ni waajiriwa wetu tunawalipa mishahara kwa kodi zetu!! hatutakiwi "kuwaomba" tumewaajiri.
Huu utamaduni wa kuomba umetudumaza tumeshindwa kuelewa nani anawajibika kwa nani kati ya serikali na wananchi!! Tumeshindwa kudai maendeleo kama haki yetu!! Tumewafanya watawala waone maendeleo kwetu ni fadhila!! na siyo haki tena! tumewafanya watawala kutumia hata fedha/raslimali zetu wanavyotaka siyo tunavyotaka wenye mali!! TUAMKE JAMANI!!
 
Hapa ndipo unapojiuliza uwajibikaji uko wapi? hapo ndipo unapojiuliza mara kumi kumi utashi wa kisiasa kweli upo hapa Danganyika land?
 
Nani kawadanganya JK yupo kwa ajili ya kutatua matatizo yenu?

Nadhani kwa hilo halimhusu labda umuulize ratiba ya kusafiri ndo anaijua.

Poleni waTz cjui haya majanga ya kila siku yataisha lini

Haya yote yana mwisho! Wanachopaswa kutambua ni kuwa 'hatesi mtesa akafululiza'. Itafika wakati kusafiri hakutasaidia. Itakuwa vizuri akitambua kuwa 'kurukaruka si dawa ya ulimbo!'
 
Nani kawadanganya JK yupo kwa ajili ya kutatua matatizo yenu?

Nadhani kwa hilo halimhusu labda umuulize ratiba ya kusafiri ndo anaijua.

Poleni waTz cjui haya majanga ya kila siku yataisha lini

Haya yote yana mwisho! Wanachopaswa kutambua ni kuwa 'hatesi mtesa akafululiza.' Itafika wakati kusafiri hakutasaidia. Itakuwa vizuri akitambua kuwa 'kurukaruka si dawa ya ulimbo!'
 
huwezi kuona kibanzi kwenye jicho la mwenzio wakati boliti kwako hujalitoa.yeye mwenyewe mbovu je ataona ubovu wa wasaidiziwake? kama anawapenda wananchi basi awatoe hao la sivyo wananchi ndo wataumiamaana yeye na wasaidizi wake wanaenda kutibiwa njeee!
 
Kwa kosa lipi, maana tusije kuwa twasema bila facts in issue

walishindwa kuutatua mgogoro tangu mwanzo badala yake wakawa wanakimbilia vyombo vya habari. Hivi kama wewe wananchi unaowaongoza wamekosa imani na wewe kwa nini uendele kulazimisha wawe chini yako?
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom