Mgomo Wa Madaktari: Jee, Serikali Kuwafukuza Kazi Kwa Summary Dismissal kwa "Insubordination"?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,466
113,548
Wanabodi,
Hili ni opinion question yangu kuwa jee, serikali inajipanga kuwafukuza kazi madaktari wote waliogoma kwa 'summary dismissal" kwa kutumia kipengele cha "insubordination"?. Lengo likiwa ni kuzuia mgomo huu usisambae nchi nzima hivyo ku paralyse sekta nzima ya Tanzania?.

Opinion hii inafuatia majibu ya kimitego mitego yanayotolewa na viongozi wakuu wa seriali na sekta ya afya nchini!
1. Juzi, Waziri Mkuu Mizengo Pinda akizungumza na wahariri wa vyombo vya habari, alisema yuko tayari kukutana na madaktari hao wakati wowote ila concern yake kubwa kwanza ni maisha ya watu yanayopotea!, hivyo akawataka kwanza warejee kazini ndipo mazungumzo yafuatie.
2. Jana Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda, alipanga kukutana nao, lakini badala ya kuwafuata pale wanapokutania, serikali ikatafuta ukumbi mwingine wenye usalama zaidi ili kumwezesha Waziri Mkuu Pinda, kwenda kuwaangukia!, Madaktari hao wagomaji wakataa kwenda pengine popote zaidi ya hapo walipo!.
3. Asubuhi hii Naibu Waziri wa Afya, Dr. Lucy Nkya, ametangaza serikali haiwezi kuwafuata madaktari hapo walipo kwa kwa sababu hawana uhakika na usalama wa eneo hilo la kukutania, na kuwataka wakubali kukutania katika eneo watakalotayarishiwa na serikali ambalo ni salama ili serikali kupitia kwa Mtoto wa Mkulima, Mhe. Mizengo Pinda, iwaangukie!.
4. Leo serikali itatoa taarifa rasmi ya Altimatum kuwa kufikia Jumatatu Saa 2:00 asubuhi, dakitari yoyote ambaye hataripo sehemu yake ya kazi, ajihesabu amejifukuzisha kazi!. Altimutum hii na tishio la kuwafukuza kazi ni mpango wa Iron Lady Mama Blandina Nyoni, "never on earth to bow down on anyone!"!. Serikali itamia vifungu vya sheria ya kazi kuonyesha mgomo huo sio halali hivyo kuhalalisha matumizi ya summary dismissal kwa insubordination!
5. Wakati ninaandika opinion hii, serikali tayari imeshawaandikia barua madfaktari wote wastaafu ambao ni able, kurejea kazini kwa dharura!, madaktari wote wa jeshi wamemepawa amri ya stand by, kuwa tayari kufanya kazi masaa 18!.
6. Mpango huo wa kuwafukuza kazi kwa "summary dismissal",kwa kutumia kifungu cha "insubordination" utawanyima haki zao zote, ukiondoa michango yao tuu waliyokatwa kwenye mifuko ya hifadhi za jamii!.
7. Taarifa za mpango huo wa serikali zimetumwa mjini Davos nchini Uswisi kupata baraka za mkuu nchi, na kuna uwezekano kabla ya utekelezaji wa uamuzi huu, rais Jakaya Kikwete, ataikatiza ziara yake ya nchini Uswisi na kurejea nyumbani over the weekend ambapo kabla ya kumalizika altimatum hiyo, Rais Kikwete atalihutubia taifa kwa mtindo ule wa kuuzuia ule mgomo wa wafanyakazi!.
8. Kitendo cha mtumishi wa serikali, kukataa kutekeleza amri halali ya mkuu wake wa kazi, hiyo ni insubordination na adhabu yake ni summary dismissal!. Hivyo pamoja na genuinity yote ya madai ya madaktari, jee mgomo wao ni halali?, unafuata sheria za migomo kwa mujibu wa sheria zetu za kazi na maadili ya kidakitari?!.

Wasalaam

Pasco (wa jf)
Update:
Nimeona news clip ya ITV. Waziri wa Afya Dr. Haji Mponda amewafuata madaktari walipo akiwa ameandamana na Waziri wa Utumishi, Hawa Ghasia na Naibu Waziri wa Afya Dr. Lucy Nkya.

Waziri wa Afya amepokea malalamiko yao ambayo wameyaelekeza kwa Waziri Mkuu. Pia amewasilisha ombi la serikali kuwa kesho warudi kazini wakati serikali ikishughulikia madai yao.

Madaktari wamegoma na kusema wanasubiri majibu ya barua yao kwa Pinda.

Kesho, Mtoto wa Mkulima atakwenda kuonana nao na kuwaomba waripoti kazini Jumatatu asubuhi. Kama na kesho watagoma, kesho kutwa JK atarudi na J3 atalihutubia taifa hotuba kama ile ya mbayuwayu!.

Sisi wote tunaowaunga mkono madaktari, tuanze pia kuwakumbusha kupunguza misimamo mikali, Tuwaombe madaktari wetu, kesho Pinda akija na kuwaangukia, wamkubalie na kurudi kazini vinginevyo itakuwa ni kukomoana kama vita vya ndovu, ziuniazo ni nyika!

Hizi kauli za shinikizo la kuendelea kugoma, ni kweli umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu, lakini katika umoja huo tangulizeni maslahi ya taifa mbele, mkiendelea kutunisha misuli ni kweli mtakuwa fired, na ni kweli kuna baadhi yenu watagain kwa kwenda kupata kazi nje ya nchi, lakini kuna wengine wata loose na to be rendered jobless overnight!.

Kesho asubuhi ripotini kazini hata kama sio lazima mtibu, then endelezeni go slow mpaka kilio chenu kijibiwe!
 
Jibu langu la haraka ni kuwa serikali haiwezi kufanya hivyo, haiwezi kuombea iweze kufanya hivyo na ikidhania kuwa inaweza kufanya hivyo haitoweza kufanya hivyo kwa sababu ikifanya hivyo itakuwa imepoteza uhalali wa kuwa serikali! Unless wafukuze madaktari wote, wauguzi wote! na wakiweza wagunge na mahospitali yote!

Ila kwa vile naamaini naweza kuwa nimekosea naombea serikali ifanye hivyo mapema zaidi kutangaza kuwa madaktari wote waliogoma wamefukuzwa kazi!!!
 
@Pasco

Naweza kukuridisha nyuma je unaweza kutuwekea hapa Nini hasa madai ya madaktari? Maana ukiona wasomi nao wanakuwa wanasiasa tujue nchi inakwenda pabaya. Na before gmo jithada gani zimefanyika zkashindindwa kuzaa matunda . itapendeza tupate pcha ya pande mbili zote za shilgi. so far naona madakatari wanaaibsha taaluma yao na wamekuwa "wabinafsi" sana.

@ CDM na vyama vingine vya SIASA

Alafu CHADEMA na vyama vyote vya siasa wanatakiwa watoe tamko na msimao wao wa chama juu ya mamba kama haya.

Wasidhani hili ni jambo la CCM tu. Yes CCM inangoza serikali lakini iliyogoemwa ni serikal . Na CDM au CUF wanaweza kuongoza Serikali siku moja . Hii ni wish ya kilwa mpenda mabadiliko na mm nikiwa mmoja wao

Dr Slaa, Mtatiro, au waemaji wenu wa mambo ya afya watanzania tunataa kusikia msimamo wenu Offcial.

alafu Pasco kwa uchokozi wangu zaidi baada ya kutafuta picha ya madokta wawili ukakosa tafadhali mtafute Dk slaa na muulize kuhusu hili. ikiwezekana aapata muda aje atupe msimamo wake (wa chama) kwenye hii thread. Au mtu yeyote mwenye acess na CHADEMA awaambie watoe tamko rasmi
 
Hiyo itakuwa ni kama kuzima moto kwa petroli!!!! na itakuwa imeamsha hasira za hata sehemu ambapo bado mgomo haujafika na pia kada nyingine sekta ya afya. Tusubiri tuone.....
 
Is anyone here is taking Pasco serious!!??
Mkuu Matola, don't take me serious, but just wait and see!.
Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.
 
Pasco,

Hakuna summary dismissal kwa sheria za kazi zilizopo hivi sasa.
Inachoweza kufanya serikali ni kuwasimamisha kazi (huku ikitakiwa kuendelea kuwalipa stahili zao zote ) hadi hapo discpilinary hearing itakapofanyika. Kuhusu Madaktari kufuata procedure za kugoma sina hakika kama zilifuatwa.
Hata hivyo ni wazi kuwa namna serikali ilinyohandle swala hili tangu mwanzo ndiko kumechochea mgogoro zaidi. Kwahali ilipofikia hivi sasa ni wazi kama serikali itaamua kutumia mabavu itazidi kupalia moto mgogoro.
 
Mkuu Matola, don't take me serious, but just wait and see!.
Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.

kwa kweli sikukatalii moja kwa moja kwani kimoyomoyo naombea itokee hili kwani mpasuko kati ya watawala na wataliwa utazidi kuongezeka tu kwa sababu unlike in 2006 walipofanya kwa wale interns safari hii madaktari wana support tena hata toka kwa wananchi wenyewe! This is the X factor!
 
Jibu langu la haraka ni kuwa serikali haiwezi kufanya hivyo, haiwezi kuombea iweze kufanya hivyo na ikidhania kuwa inaweza kufanya hivyo haitoweza kufanya hivyo kwa sababu ikifanya hivyo itakuwa imepoteza uhalali wa kuwa serikali! Unless wafukuze madaktari wote, wauguzi wote! na wakiweza wagunge na mahospitali yote!

Ila kwa vile naamaini naweza kuwa nimekosea naombea serikali ifanye hivyo mapema zaidi kutangaza kuwa madaktari wote waliogoma wamefukuzwa kazi!!!
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.

Na baada ya tamko la kuwafukuza kazi hiyo next Monday, Tuesday mtaona Tangazo la ajira za madaktari equal na number ya waliotimuliwa jana yake, na tangazo hilo litasema, madaktari waliotimuliwa ruksa kuomba kazi upya, na belive me, wataomba, kwa masharti yale yale waliyoyagomea!, na this time masharti yao ya ajira mpya yatatamka 'expresisly' not 'impliedly' ni marufuku kugoma, na ukigoma tuu jihesabu you have lost your job!.
 
Mkuu Matola, don't take me serious, but just wait and see!.
Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.
then?.....ww una maoni gani?
 
Pasco!
Jambo usilolijua ni usiku wa kiza. Kanunue employment Act 2004 uisome na baada ya hapo anzisha thread upya.
Nenda na wakati. Anyway kuwafukuza kazi sio suluhisho ila ni sawa tu na mpumbavu anapoamua kwenda kulewa pombe ili apunguze mawazo na akiamka ngoma iko pale pale. Narudia WATANZANIA hawako serious. Kwa watu makini na if we had any opposition then nauona mgomo wa Madaktari ungekuwa ni chachu ya Mapinduzi ya umma. Kila mtu angegoma kufanya kazi kwani kwa kuwa matabibu wamegoma ukiumia una uhakika wa kufa kwani kuna mgomo. But nimefurahishwa na wale Doctors wa KCMC wao wameweka a functional strategy kwamba huduma za dharura zitaendelea kutolewa ila out patients hawatahudumiwa. That is professional ila hizi fujo za hao wa Dar sijui ni kinyume na kiapo chao. Let us do something tools down mpaka viwanja vya ndege tugome wote. Huyu Dr. Mponda ni mwongo na asulubiwe au apigwe mawe mpaka afe TRA wabslipwa kuliko Madaktari Kama anabisha alete data to prove that Doctors are the highiest paid civil servants.
 
Mkuu Mzee Mwanakijiji, Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.

Na baada ya tamko la kuwafukuza kazi hiyo next Monday, Tuesday mtaona Tangazo la ajira za madaktari equal na number ya waliotimuliwa jana yake, na tangazo hilo litasema, madaktari waliotimuliwa ruksa kuomba kazi upya, na belive me, wataomba, kwa masharti yale yale waliyoyagomea!, na this time masharti yao ya ajira mpya yatatamka 'expresisly' not 'impliedly' ni marufuku kugoma, na ukigoma tuu jihesabu you have lost your job!.
hii serikali ya kidhalimu nakuambieni....Docs wastaafu wanaikubali huo mkwanja? aisee 5 solid years miksa sups kibao alafu unakuja kufanywa hamnazo inauma sana....
 
Pasco,

Wansubiri kwanza kuona Bakuli kutoka Davos litarudi na nini. Kama watapata kitu kidogo then madaktari watachekelea. Ila bakuli likirudi tupu nafikiri itabidi utaratibu msioutegemea utumike. Nakumbuka miaka ya 90s mgomo kama huo ulitokea na ulimcost one of my in law mpaka leo hajawa settled kisawaswa.
 
kwa kweli sikukatalii moja kwa moja kwani kimoyomoyo naombea itokee hili kwani mpasuko kati ya watawala na wataliwa utazidi kuongezeka tu kwa sababu unlike in 2006 walipofanya kwa wale interns safari hii madaktari wana support tena hata toka kwa wananchi wenyewe! This is the X factor!
Mzee Mwanakijiji, madaktari sio tuu wanaungwa mkono na wananchi, pia wanaungwa mkoo na wakuu wao wa kazi. Nilimsikia Mkuu wa Hospitali ya Ocean Rd, Dr. Twalib Ngoma, akisema hawezi kuwaamuru madaktari wake warudi kazini kwa lazima kwa sababu madai yao ni genuine. Mpaka sasa sijamsikia Dr. Marina Njelekela akitamka lolote!.

Mpango huu wa kuwafukuza kazi unasukwa na Iron Lady, Bibi Blandina Nyoni, na ili ukamilike lazima uwahusishe wakuu wa hospitali za umma ambao ndio hao watakaozitoa na kuzisign hizo barua za summary dismissal!. Maadam mwajiri wao ni serikali, serikali imewaita wazungumze kwenye location ambayo serikali imeona ndio muafaka, ifikie muda hao madaktari wakubali kuitikia wito na kwenda kuisikiliza hiyo serikali. Kitendo cha kuitunishia msuli na kukataa kuitikia wito wa mwajiri wao, kisheria hii ni insubordination!.

Binafsi naunga mkono mgomo huu kwa asilimia 100%, na hata kama kuna watu watakufa kwa sababu ya mgomo huu, anayepanga saa ya kufa ni Mungu pekee, hiyo wakifa, hiyo ndio saa yao ya kufa waliopangiwa siku wanazaliwa, itakuwa ndio imetimia na waliandikiwa watakufa hivyo watakavyo kufa!, lakini hao madaktari wakomaji lazima wawe rasonable japo kidogo kwa kuitika wito!.
 
Mkuu Matola, don't take me serious, but just wait and see!.
Its just a matter of time subiri tamko hilo within the next 48hrs!, unless madaktari wakomaji wamekubali kuitikia mwito wa serikali kuifuata ilipo, wakishikilia msimamo wao, kuwa lazima serikali ndio iwafuate walipo, serikali haitawafuata and they will be fired!.
Realy!!?? do u think next 48 hours is too long? i will be here in the same thread.
 
Back
Top Bottom