Ciril
JF-Expert Member
- Jan 10, 2011
- 8,558
- 7,156
Jumuiya ya madaktari Tanzania imekataa msaada wa serikali kwa ajili ya kugharamia matibabu ya Dr Ulimboka Stephen.
Msemaji wa wizara ya Afya Nsachris Mwamwaja jana alisema serikali ilikuwa tayari kugharamia matibabu ya kiongozi huyo wa madaktari lakini msaada wao ulikataliwa.Alisema walizuiwa na madaktari ambao waliitaka serikali ikae mbali kabisa na matibabu ya Dr Ulimboka.Alisema kitendo hicho kiliihuzunisha sana serikali.
Ndani ya saa 24 watanzania kwa mshikamano na umoja wa hali ya juu wamechanga zaidi ya shilingi milioni 63 kiasi ambacho kilihitajika kumpeleka Dr Ulimboka nje ya nchi kujaribu kuokoa maisha yake.
Source:Mwananchi Jumapili.
Safi sana madaktari,asanteni sana Watanzania kwa kuonyesha mshikamano wenu kwa Mtanzania(Dr Ulimboka)mwenzenu masikini Kama ninyi.