Madaktari wakataa msaada wa Serikali kugharamia matibabu ya Dr Ulimboka

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Jumuiya ya madaktari Tanzania imekataa msaada wa serikali kwa ajili ya kugharamia matibabu ya Dr Ulimboka Stephen.
Msemaji wa wizara ya Afya Nsachris Mwamwaja jana alisema serikali ilikuwa tayari kugharamia matibabu ya kiongozi huyo wa madaktari lakini msaada wao ulikataliwa.Alisema walizuiwa na madaktari ambao waliitaka serikali ikae mbali kabisa na matibabu ya Dr Ulimboka.Alisema kitendo hicho kiliihuzunisha sana serikali.
Ndani ya saa 24 watanzania kwa mshikamano na umoja wa hali ya juu wamechanga zaidi ya shilingi milioni 63 kiasi ambacho kilihitajika kumpeleka Dr Ulimboka nje ya nchi kujaribu kuokoa maisha yake.

Source:Mwananchi Jumapili.
 
Msuli bado unatunishwa, na sijui mwisho wa siku ni nani ataibuka bingwa kati ya mahasimu wakubwa serikali na madokta. Ila naona wachezaji wengi wa timu ya serikali wanaonyeshwa kadi za njano kwa kuwafanyia rafu mbaya wachezaji wa timu ya madokta. Na naona Ikulu imepewa kadi nyekundu baada ya kusadikika kufanya faulo mbaya dhidi ya mchezaji mmoja wa timu pinzani.
God shows his love to us in that while we were yet sinners Christ died for us.
 
Ndani ya saa 24 milioni 63 zimepatikana? Aibu kwa serikali, sijui inajisikiaje katika hili?
 
Mhe waziri mkuu ooh sorry mh spika nimesahau kumbe mimi ndio pm mwenyewe; ofcourse nimesikitishwa sana na hawa doktaz kukataa contribution ya serikali, binafsi namheshimu sana dokta ulimboka ila aahh mmhh oooohhh hili suala lipo mahakamani
 
safi kabisa serikali ilifikiri inajenga kumbe imebomoa tena waombe Mungu asife sbb mwisho wao wa kutawala utatamatika. Huku mtaani watu wanahasira kwelikweli. watawala wamegundua hilo ndo maana wanata kuzima moto kwa kumgarimia. SHAME ON GAVERNMENT!!!
 
Na kama akifa ndipo serikali itapogundua kuwa serikali ni madaraka tu, maana wataakiwa wakae mbali kama wahalifu vile mbele ya raia wema.

Mungu mponye Dr. Ulimboka ili kuepusha mengi na kuibua maovu ya wengi.
 
Mhe waziri mkuu ooh sorry mh spika nimesahau kumbe mimi ndio pm mwenyewe; ofcourse nimesikitishwa sana na hawa doktaz kukataa contribution ya serikali, binafsi namheshimu sana dokta ulimboka ila aahh mmhh oooohhh hili suala lipo mahakamani
Mkuu nilimsikia siku ile PM akijichanganya kwa swali la Mbowe kuhusu Ulimboka.Ilibaki kidogo tumsikie akisema "Shikamoo kiongozi wa kambi ya upinzani" Kujichanganya kule kunaonyesha kipigo cha Dr alikielewa mapema kabla hakijatokea ila hakudhani kitakuwa kibaya kwa kiasi kile
 
Back
Top Bottom