Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...

Vancomycin

Senior Member
Jan 7, 2011
171
111
Taarifa ambazo zimethibitishwa zinatabanaisha kuwa madaktari walio katika uzoefu kazini, INTERN doctors wameanza kufukuzwa katika hospitali mbalimbali ambapo katika hospitali ya DODOMA madaktari 11 kati ya 33 wamefukuzwa na madaktari wote 70 waliokuwepo hospitali ya rufaa mbeya chini ya ulinzi mkali wa polisi wameambiwa waondoke kufikia saa 11 jioni ya leo wakati huo huo mkurugenzi wa hospitali ya BUGANDO amewafukuza madaktari wote 44 na kuwataka warudi wizarani wakati madaktari waliosajiriwa wameamuriwa kufika kesho wawe kazini au la wanafukuzwa.

Wakati huo huo madaktari wakazi waliitwa na senate ya BUGANDO na kulazimishwa kurudi kazini lakini walikataa mbele ya senate hiyo hivyo wakaambiwa watafutiwa udahili wao na wote kwa pamoja wakapiga makofi wakisema wako tayari kwa hilo.

Habari zaidi zinazidi kupasha kuwa hospitali ya Mwananyamala wameletewa fomu za kujaza kama wako tayari kuendelea na kazi au la,ila madaktari wamesimamia msimamo wao huo kuwa mgomo uko pale pale.

Katika hatua nyingine CHUO CHA TIBA BUGANDO NA KILE CHA MUHIMBILI VIKO MBIONI KUFUNGWA kutoka na walimu wao ambao ni madaktari kugoma na mazingira kutokuwa rafiki kwa kujifunzia.

Wakati hayo yakiendelea taarifa zinasema hsopitali ya Tanga BOMBO imeingia rasmi kwenye mgomo na ile ya MOUNT MERU

Habari zaidi madaktari wanajiandaa kwa mass resignation muda wowote

attachment.php

attachment.php
 

Attachments

  • bugando.jpg
    bugando.jpg
    124.7 KB · Views: 806
  • mbeya-wafukuzwa1.jpg
    mbeya-wafukuzwa1.jpg
    36.7 KB · Views: 583
Ndio hayo alipanga kuyasema bungeni ila la Olimboka likaingilia mikakati
 
Unajua serikali dhaifu bado inaamini kuwa watu wataogopa kupoteza kazi zao.
Madaktari wanawabipu, nyie wapigieni tu.
 
Kuna wajinga wanataka wageuze majengo ya hospitali magofu na magodauni yakuwekea mali zao za kifisadi.
 
Wakuu endeleeni kutujuza kila linaloendelea kutoka kila mkoa na nawaomba sana Madakatari msivunjike moyo kwa lolote,maana nchi yenyewe ndo hii,maamuzi kama yatakuwa ndio haya wala msihofu,tafakarini hili,je ni kweli kwamba hakuna maisha nje ya ajira za serikali?na ni vipi muendelee kuwa watumwa?
 
Hivi mwisho wa haya yote nini jamani? sasa inahitajika kufanya maombi na mafungo kwajili ya Taifa letu tunakokwenda ni kubaya hali inazidi kuwa ngumu tuu kwa mlala hoi na inazidi kuwa nzuri kwawalio nacho.
 
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.

Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.
 
Back
Top Bottom