Madaktari wa China wapongezwa kwa kutoa huduma bora kwa wagonjwa barani Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
1,010
1,036
VCG111438960234.png


China imekuwa na utaratibu wa kupeleka wataalamu wa afya katika nchi mbalimbali duniani, ambao huungana na wenzao katika nchi husika kutoa huduma za matibabu kwa watu wenye matatizo ya kiafya. Madaktari hao kutoka nchini China, licha ya kuwa na changamoto ya lugha na tamaduni, wameendelea kutimiza wajibu wao kwa moyo wa upendo na huruma, na kusifiwa sana na wakazi wa maeneo waliyopo.

Hivi karibuni, nchini Togo, madaktari wa China waliopo nchini humo wamesifiwa sana kutokana na upendo, uwajibikaji, na kuwa tayari kuwafundisha madaktari wazawa mbinu na njia mpya za tiba.

Muuguzi Mkunga anayeitwa Movia kutoka eneo la Adeta mkoa wa Plateau nchini Togo anasema, amejifunza mengi kutoka kwa madaktari wa China, na hivyo kumwezesha kuongeza ujuzi na uwezo wake katika kazi.

Miezi mitano iliyopita, kundi la 25 la madaktari kutoka China walikwenda kwenye kituo cha afya katika eneo hilo lililoko kilomita 150 kutoka mji mkuu wa Togo, Lome. Madaktari hao walitoa msaada wa kiufundi kwa Zaidi ya wafanyakazi wa afya 20 katika kituo hicho, ambao ulihusiana na maeneo mengi ikiwemo magonjwa ya wanawake na ukunga na mifupa.

Kituo cha afya cha Adeta kinakabiliwa na uhaba wa madaktari, na hata vifaa vya tiba navyo vimepitwa na wakati, na pia, ufundi unaotumiwa na wahudumu wa afya katika eneo hilo umepitwa na wakati.

Kiongozi wa kikundi cha 25 cha madaktari wa China nchini Togo, Liu Yu anasema, vipimo vyote na upasuaji kwa wanawake wanaojifungua vinafanywa na makunga, ambao imewabidi kuchukua nafasi ya madaktari na wauguzi, jambo lililosababisha vifo vya wamama wajawazito na watoto wachanga wakati wa kujifungua, kwa kuwa wanaofanya upasuaji hawana ujuzi unaotakiwa.

Baada ya kujua hali ilivyo, timu ya madaktari wa China ilifanya maandalizi kwa makini na kufuatilia magonjwa ya mara kwa mara na magonjwa sugu katika eneo hilo wakati wa kutoa mafunzo, na pia kuhusisha mafunzo kwa vitendo.

Dr. Liu, ambaye ni daktari wa wanawake na uzazi, aliwafundisha wakunga wa huko, akiwemo Movia, kuhusu jinsi ya kuzuia mwanamke kutokwa na damu nyingi wakati wa kujifungua na ujuzi na masuala mengine yanayohusiana na uzazi, na pia kuwafahamisha hatua za tahadhari wakati wa kusafirisha wagonjwa walio katika hali mbaya.

Madaktari wa China katika nchi mbalimbali duniani, zikiwemo za Afrika, wamekuwa wakitoa huduma za ushauri na tiba ya bure kwa watu wanaokabiliwa na magonjwa mbalimbali katika nchi husika. Kwa mfano, katika mji huo wa Adeta, madaktari hao wametoa huduma ya tiba kwa wagonjwa 2,130.

Dr. Liu anasema, tangu walipofika Lome Oktoba 22 mwaka huu, timu yake imetoa msaada wa kiufundi mara saba, na pia kutoa mafunzo na mabadilishano ya kitaaluma yaliyonufaisha Zaidi ya wati 2,000. Tangu kuanza rasmi kwa operesheni yake katika Hospitali ya Mkoa ya Lome mwezi Agosti mwaka huu, timu hii ya madaktari inayoongozwa na Dr. Liu imetoa tiba kwa wagonjwa wan je 6,548 mpaka kufikia Oktoba 20.

Mjumbe mwingine wa timu ya madaktari wa China, Tian Shujie, alitoa mafunzo kuhusu Tiba ya Jadi ya China kwa wanafunzi wa udaktari katika Chuo Kikuu cha Lome, na kuonyesha baadhi ya tiba za jadi ikiwemo cupping, tiba vitobo (acupuncture), na kusinga.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu hicho Tchalla Toyi, ameeleza kufurahishwa sana na mafunzo yaliyotolewa na madaktari hao wa China, na kusema anatarajia kuona mabadilishano Zaidi ya kitamaduni kati ya China na Togo.

Pamoja na kwamba timu ya Dr. Liu imemaliza muda wake mwishoni mwa mwezi Oktoba na kukaribisha timu ya 26 ya madaktari wa China nchini Togo, lakini mchango wa timu hiyo kamwe hautasahaulika.
 
Back
Top Bottom