Madaktari wafukuzwa Mbeya, Bugando na Dodoma... Mwananyamala walazimishwa kusaini...

Kazi ipo, nitarudi kucheki update, asante kwa taarifa, ingawa si nzuri lakini imeficha mabadiliko makubwa
 
hapa panachimbika bila jembe wadau na kwa hii vita kama unajijua wewe ni nyasi kama mimi jiandae kuumia!
 
haya picha ndio kwanza limeanza hili... serikali kama wanazani limeisha wanajidanganya! Ngoja nikanunue pop corn kabisa ili nije kuona muvie lenyewe
 
Nilishasema na naendelea kusema Watanzania/Tanganyika tusipoelekeza hasira zetu pahala sahihi tutaendelea kuumizwa, hii ndio nafasi ya ku vent hasira zetu na concern zote tulizonazo. Jamani time is now, Dr Ulimboka katuonyesha jinsi ya kudai haki na maslahi ya madaktari na Watanzania kwa ujumla.....lets follow suit
Mimi naamini ukombozi wa Mtanzania/Tanganyika utapatikana kwa roho za ujasiri watu kama Dr Ulimboka Kamanda Godbless Lema na wengine wote waliopoteza maisha au wanaoweka maisha yao hatarini ili tupate kushuhudia na kuikomboa nchi yetu
 
Hii serikali bado haijaelewa somo kabisa,watu wanaongoza kiujanjaujanja tu hawana lolote ni usanii mtupu,dhaifuuuuuuuuuuuuuuuuu!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.

Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.

wewe subiri uone kitu cha ajabu muda si mrefu baada ya madaktari wote nchi nzima kuacha kazi watafuatiwa na wauguzi nchi nzima halafu tuone nani mjanja kama akina pinda na wenzie wataenda kuwatibu. Ikumbukwe kuwa hili litahusu pia na hospitali za watu binafsi , kwa kifupi mpaka kufikia wiki hii mwishoni nchi itakuwa haina dakatari au muuguzi yupo kituoni tuone serikali kama isopiga mogoti tena kwa madakatari na wauguzi.

"Serikali iliyochaguliwa na usalama wa taifa kamwe haiwezi kuwatumikia wananchi".
 
hawa madokta hawa yaani we acha tu..wanachojivunia ni kuwa sio kila mwanasiasa anaweza kuwa dokta, ingawa madokta wote wanaweza kuwa wanasiasa..
 
Hao waliowafukuza madaktari wako juu ya sheria? Leo Bungeni Spika amesema waziwazi kuwa hata serikali haitaruhusiwa kutoa kauli (kama walivyoahidi jana) kwa sababu hili swala liko mahakamani, na amri ya mahakama ni kuwa pande mbili yaani serikali na madaktari wakae kwenye meza ya mazungumzo. Sasa Mbeya, Bugando na Dodoma ziko juu ya amri ya mahakama? Au hawa wako Kenya?

Kwa upande mwingine huu ni mtihani kwa mhimili wa dola - Mahakama. Kama hawatesema chochote kwa hizi hospitali za Mbeya, Bugando na Dodoma basi ni wazi mahakama itakuwa inafanya kazi kwa shinikizo la serikali ya ccm. Hili litakuwa agizo la serikali kuwafukuza chini chini bila na mahakama ikae kimya wakati amri yake inapuuzwa! Tusubiri ili tuone independence ya Judiciary yetu.
 
Liwalo na liwe mimi nitatibiwa Apollo.pinda.
Sasa akili kumkichwa wewe ambaye unategemea uduma za hapa bongo.
Jiulize nani anaumia sasa hivi? Nini atma ya maisha ya watz wasioweza kutibiwa Apollo kama pinda?
Ila chakusikitisha ni kuwa wananchi tunachukulia ili ni kama tatizo la serikali na Drs wakati ni Tatizo letu na serikali, tuishinikize serikali itupatie uduma bora za afya, watajua watakopotoa Drs wengine au wote tutibiwe india kama wanavyotibiwa wao wakiugua,
Kila mtu, mwananchi ana aki yao kupatiwa uduma ya afya stahiki kama wanavyopatiwa wabunge na Mawaziri.
Kama hapa kuna uduma bora mbona wao kila kukicha wanaenda nje kutibiwa, lkn baadae utasikia 40% ya madawa ya malaria ni fake, mara dawa za kupimia magonjwa zimeingizwa nchini zikiwa zimempa expire.
 
Nadhani inabidi serikali iache kiburi lazima tutafute suluhisho la kudumu vinginevyo yaliyotokea Tunisia na Misri yatatokea hapa. Ni wakati muafaka serikali iache kutumia mabavu na busara ichukue nafasi yake, siku zote moto hauzimwi kwa mafuta ya taa, Serikali inatakiwa ijue kuwa uhai wa raia wake uko mikononi mwake.
 
Kufukuzwa madaktari siyo dawa, ila ni funzo. Hakuna haja ya wao kuendelea kuitwa watumishi wa umma wakati hawautumikii umma. 'Fukuza woooteee, kuanza upya si ujinga' Mjomba aliimba. Sifurahii kupigwa Dr. Ulimboka, ila ni funzo kwao na njia ya wananchi kuonesha uchungu wanaoupata kwa mgomo wao. Madaktari hawapaswi kutumia wagonjwa kama kiboko cha kuichapia serikali kwa madai yao hata kama yanamsingi kiasi gani. Sasa je, wamegoma kumuudumia Dr. Ulimboka alipopata matatizo yanayowapata watanzania wengi.

Nakubaliana na unamuzi wa madakatari kufukuzwa wote wanaogoma, na hata wakitaka kujuizuru wote sawa. Serikali ijipange hata kwa gharama kubwa kuwaleta madaktari kutoka majeshi ya nchi marafiki na mashirika km red cross kusaidia wakati suluhu ikitafutwa ya kudumu.

Acha ndoto za mchana wewe! Kwani nani anataka kazi bila ya kuwa na nyenzo muhimu? Hao madocta wako watakuja na mashine na dawa zao?
 
Kuwafukuza madaktari si suluhu.

Akili ndogo kushauri akili kubwa
 
hayo maelezo yalitoka jana saa nne usiku kwenda kwa madaktari wa kila mkoa juu ya swala hili...kikubwa madakatati wawe na umoja....
 
Back
Top Bottom