Madaktari kugoma nchi nzima!

Nilipenda sana vazi la Jf katika mazishi ya Regia hususan yale maneno yake.

Kwanza msahihishane, mkosoane ndio msameheane.

Jf Ni zaidi ya habari.
 
i support. wakaze uzi tuone kama wauguz na watu wa maabara wanaweza toa huduma pekeyao. najua mpaka saa nane usiku madai yao yatakuwa yamefanyiwa kazi.
 
waliwahi kugoma wakaongezewa mshahara kwa 100%, ni bora wagome, madaktari wengi hawamudu kuzilipia huduma wanazozitoa kama wakiwa wagonjwa, wengi hufa kwa magonjwa ya kawaida kwa sababu hawezi kumudu kwenda REGENCY, AGHAKAN n.k , kama akitakiwa kwenda huko.
 
Wagome mara ngapi?
mbona hawa wapo katika mgomo siku nyingi maana huduma zao duni sana na ndiyo maana wagonjwa wanawakimbia na kwenda India.

Wale hoi kama mimi ndio tunao kiona, hao akina wakuu serikalini wakiugua tu wanaenda apolo.
 
point of correction mkuu sio mgomo coz MAT kisheria hairuhusiwi kuanzisha mgomo.kwa kifupi tuna 'extension meetings' ambazo zitaendelea mpaka pale serikali itakapotatua matatizo yetu.......naibu wizara wa afya kachomoa kukutana nasi saa hizi ingawa about one hour ago alisema atakuja.kaomba tukutane naye kesho,nadhani wanajipanga na propaganda zao
 
ha ha ha ha....ukigua unapiga kimya na ugonjwa wako home mpaka mgomo uishe....
kugoma kwa madaktari ni aibu kwa serikali na hii ni changamoto kwa serikali..
hapa ni kuhakikisha hakuna kuugua hadi mgomo utakapo malizika!!
 
Namaunga mkono kudai maslahi bora! wekeni uwezekano msizitelekeze ward za wazazi, wengine waendelee na vikao, wakati wengine wakiwapokea walipakodi watarajiwa Na MUNGU atawabariki.
 
point of correction mkuu sio mgomo coz MAT kisheria hairuhusiwi kuanzisha mgomo.kwa kifupi tuna 'extension meetings' ambazo zitaendelea mpaka pale serikali itakapotatua matatizo yetu.......naibu wizara wa afya kachomoa kukutana nasi saa hizi ingawa about one hour ago alisema atakuja.kaomba tukutane naye kesho,nadhani wanajipanga na propaganda zao

komaeni wakuu
mbona wao maposho wanajiongezea? inakuwaje kwa watu wanao okoa maisha ya hata wao wenyewe wana wanyanyasa? kwa kizingio cha kiapo hakiwarusu,no no haiwezekani.komaeni kama wao wataenda india kujitibu haina shida lakin i ujumbe uwafikie
tena wanapoteza mapesa kibao kuwaneemesha appolo ambao ni hosptal binafsi
 
ha ha ha ha....ukigua unapiga kimya na ugonjwa wako home mpaka mgomo uishe....
kugoma kwa madaktari ni aibu kwa serikali na hii ni changamoto kwa serikali..


Kwa serikali hii ya raisi kikwete sitoshangaa ikiamua kutunisha msuli bila kujali kwamba kuna wananchi wengi wataumia na hata kufariki kwa matatizo ambayo yangeweza kutibika, simply tu kutaka kuonyesha ubabe wake.
 
komaeni wakuu
mbona wao maposho wanajiongezea? inakuwaje kwa watu wanao okoa maisha ya hata wao wenyewe wana wanyanyasa? kwa kizingio cha kiapo hakiwarusu,no no haiwezekani.komaeni kama wao wataenda india kujitibu haina shida lakin i ujumbe uwafikie
tena wanapoteza mapesa kibao kuwaneemesha appolo ambao ni hosptal binafsi

Juzi nimemsikia Dr. Kigwangala akisema kwamba serikali ilishatangaza kupandisha viwango vya posho za madaktari wanapokuwa on call hadi kufikia tsh.80,000.00 lakini bado wizara ya afya chini ya blandina nyoni imeweka ngumu kulipa kiwango kipya na kuendelea kulipa tsh.10,000.00 kiwango cha miaka zaidi ya saba iliyopita.

Madaktari wasipoungana kudai haki yao, wajue kabisa hakuna wa kuwasimamia kwani madaktari wenzao walioko serikalini kwenye nyadhifa za kiutawala wamewatosa. Nakumbuka ule mgomo wa akina Dr. Kigwangala na Dr. Ulimboka Steven ndio ulisababisha angalau serikali kuongeza malipo ya madkatari. Sijui alipotelea wapi Ulimboka?
 
ombi la MAT lilikuwa dogo tu,kuwarudisha interns waliofukuzwa muhimbili kwani serikali ilikiri kile walichokuwa wanakidai ni haki yao iliyocheleweshwa bila taarifa.sasa kwa kuwa waziri,katibu mkuu na mganga mkuu kiongozi hawana huruma kwa watanzania wakaamua kuwadhalilisha,kuwakebehi na kuwafanya kama wanafunzi wakati wamewapa jukumu la kuhudumia wagonjwa pale muhimbili.
kuna madaktari bingwa wa siku nyingi na uzoefu lakini hawana thamani mbele ya watawala wetu.wanafanya kazi kwa moyo wote huku wakilipwa ujira kidogo lakini wanapougua hawapelekwi india,yote haya yanabebwa na mioyo stahimilivu ya madaktari kisa wito.tunapokaa na kujisifu ya kuwa afya ya mtanzania inaboreka ni kwa nini hatujiulizi ni nani aliyefanikisha?
inauma kuona kijana huyu anayeitwa intern akiteseka wakati anasoma kozi ya medicine kwa masomo magumu huku akiangaikia posho za kujikimu board ya mikopo halafu leo hii amegraduate na kukosa posho zake za internship,kesho akitembea mtaani kusubiri kupangiwa kituo na keshokutwa akiwa kituoni anasubiria kuingia kwenye payroll kwa miezi kadhaa na baadae anakosa call allowance kwa miezi kadhaa bila taarifa huku akishuhudia classmate wake wa form four akiongezewa posho kwa kulala pale mjengoni.....
mheshimiwa rais chukua hatua usichukiwe kwa uzembe wa watu wachache wasiotimiza wajibu wao.
 
"extended meeting"
Imekaaje.
Hamjagoma?
Yani unaaga kazini kwako unaenda kikaoni,
siku nzima...
alaf kila siku....
Duh...
 
(a) Hakuna Unyonyaji:
Nchi yenye Ujamaa kamili ni nchi ya wafanyakazi: haina ubepari wala ukabaila. Haina tabaka mbii za watu: tabaka ya chini ya watu wanaoishi kwa kufanya kazi, na tabaka ya juu ya watu wanaoishi kwa kufanyiwa kazi. Katika nchi ya Ujamaa kamili mtu hamnyonyi mtu, bali kila awezaye kufanya kazi hufanya kazi, na kila mfanya kazi hupata pato la haki kwa kazi aifanyayo na wala mapato ya wafanyakazi mbali mbali hayapitani mno. Katika nchi ya Ujamaa kamili watu peke yao ambao huishi kwa jasho la wenzao, na ni haki yao kuishi kwa jasho la wenzao ni watoto wadogo, wazee wasiojiweza, vilema na wale ambao, kwa muda, Jumuiya imeshindwa kuwapatia kazi yo yote ya kujipatia riziki kwa nguvu zao wenyewe. Nchi yetu ni nchi ya Wakulima na Wafanya kazi, lakini si nchi ya Ujamaa kamili. Ina misingi ya ubepari na ukabaila na vishawishi vyake. Misingi hii ya ubepari na ukabaila yaweza ikapanuka na kuenea.
 
Pamoja na unyeti wa taaluma yao sijui kwanini Madaktari wanakubali kunyanyasika kama walimu(ambao kwa wingi wao wanashindwa kushikamana!).
 
mmenyanyaswa sana,mmeonewa sana,mmetukanwa sana nadhani kuna kitu mnatakiwa kugrand si kingine ni kugoma tu

Umenikumbusha wakata jamaa aliyejiuzulu na sasa anataka ajulikane kama aliyestaafu alipokuwa anamwaga manyanga
 
Back
Top Bottom