Madaktari kugoma nchi nzima!

Mazee

Senior Member
Dec 6, 2007
128
24
Kikao cha mkutano mkuu wa dharura wa chama cha madaktari Tanzania (MAT) kilichofanyika leo siku ya jumamosi, tarehe 14/01/2012 ukumbi wa JAFFARY COMPLEX kimejadili kwa kina yafuatayo:

1.
Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimejadili na kuazimia kutoa masaa 72 kwa serikali kuwa “Intern doctors” wote waliohamishwa warudishwe Muhimbili mara moja wakamalizie muda wao. Na kwamba ifahamike kuwa interns huomba kwenda kufanya internship katika hospitali Fulani kutegemeana na malengo ya baadaye waliojiwekea. Na pili kuna baadhi ya vifaa vipo mf. Muhimbili na huko kwingine haviko. Madaktari wemesikitishwa sana na uamuzi huu kwa vile haieleweki ni kwa nini “intern doctors” waadhibiwe wakati walidai walipwe mishahara yao tu na serikali ilikiri kosa hilo. Wanachama wangependa kuona waliofanya uzembe huo wanawajibishwa mara moja na sio kuachwa waendelee kuwaadhibu madaktari wasio na kosa.

2. Kwamba, kwa kuwa Intern doctors wamekuwa wakifanya kazi bila malipo kwa muda mrefu na hali hiyo ikapelekea kusitisha kazi ndipo serikali ikaamua kuwalipa mishahara yao. Kufuatia kuendelea kusababisha adha kwa madaktari na wataalamu wengine wa afya na hatimaye kusababisha huduma mbovu kwa wagonjwa, Chama cha madaktari kimeona kimshauri Mh. Rais atafute ajira nyingine kwa ajili ya maafisa waandamizi wafuatao:
a. Katibu Mkuu, wizara ya Afya , Ms. Blandina Nyoni b. Mganga Mkuu wa serikali, Dr. Deo Mtasiwa
3. Kwamba waziri wa afya Dr. Hadji Mponda (MB) afute kauli yake inayoashiria kwamba “intern doctors” ni wanafunzi wa udaktari wa mwaka wa 5. Ieleweke kwamba ni madaktari kamili, waliohitimu mafunzo yao na kula kiapo rasmi cha udaktari. Na chama cha madaktari kimesikitishwa sana na upotoshwaji huuu wa mara kwa mara. Kutokana na hayo hapo juu basi chama cha madaktari Tanzania kina msamehe kwani inaonekana hajui atendalo. Ijulikane kwamba mjadala wa hivi ulishawahi kuibushwa mwaka
2005 na waziri wa afya kipindi hicho alikiri bayana kwamba intern ni daktari kamili aliyefuzu.

4. Kwamba, chama cha madaktari Tanzania kimeamua kumsimamisha uanachama wa chama hiki Dkt. Deo Mtasiwa, ambaye pia ni Mganga Mkuu wa Serikali (CMO), kwa kosa la kusaliti fani ya udaktari na pia kwa kushindwa kumshauri waziri wa afya vizuri kuhusiana na mambo yanayohusu fani ya udaktari Tanzania. Mkutano huu unamsimamisha rasmi Uanachama huo kwa kipindi cha mwaka mmoja. Taratibu za kumrejesha zitajadiliwa kwenye Mkutano mkuu wa kawaida wa chama. Hii itakuwa fundisho kwa madaktari wengine wote nchini.

5. Kwamba chama cha madaktari Tanzania (MAT) kimeazimia kuitisha mkutano mwingine mkubwa wa wanachama wote siku ya jumatano tarehe
18/01/2012, kuanzia saa tatu asubuhi na kuendelea kwenye ukumbi
utakaotangazwa. Agenda za mkutano huo, pamoja na mambo mengine, zitakuwa zifuatazo:
i. Hatma ya heshima ya fani ya udaktari na mustakabali wa huduma za afya kwa watanzania
ii. Kwa nini serikali haijaanza kulipa posho ya kazi muda wa ziada (on call allowance) kama ilivyopitishwa mwaka 1990 na kufanyiwa maboresho mwaka 2008.
iii. Mshahara mpya wa daktari unaoendana na elimu, ujuzi, umuhimu, hadhi, majukumu, na hali ya uchumi wa sasa na mfumuko wa bei.
iv. Maslahi mengine ya madaktari kama nyumba, posho ya mazingira magumu, ufadhili wa masomo ya elimu ya juu na posho ya kufanya kazi kwenye mazingira hatarishi( Risk allowance).
v. Kuhamishwa hovyo hovyo kwa madaktari bingwa 61
vi. Mengineyo (kwa idhini ya mwenyekiti)
IMETOLEWA​

DR. NAMALA MKOPI
RAIS – CHAMA CHA MADAKTARI TANZANIA (MAT)
 
Mzee wa Kaya natumaini ujumbe huu atakuwa ameshapelekewa na timu ya Salva Rweyemamu. Kazi ipo mwaka huu Poleni wa Dr. wa ukweli kwa matatizo mnayoyapata. Haki haiombwi bali inapiganiwa
 
mhh serikali imeingia katika vita ambayo siku zote tunajua mshindi ni nani..? :biggrin:
 
Kwa kweli mimi sifahamu tunakoelekea kama Taifa, hii migogoro kati ya madaktari na serikali kila mwaka imekuwa na athari kubwa sana kwa watanzania na hasa wa vipato vya chini, na ndio maana leo hii madaktari wamekuwa hawawajibiki tena wanapokuwa kwenye vituo vyao vya kazi wanababaisha then wanakuelekeza kwenda kwenye hospitali zao binafsi ambazo ni ghali sana, Serikali angalieni hii mambo bhana wananchi tunaumia.:shock:
 
Siku zote nimekuwa nawaonea huruma sana madaktari!!
Ile wizara ya afya lazima ifumuliwe kabisa ukianzia na huyo nyoni!!
Kwa kweli madaktari msilegeze kamba bana hadi ikibidi kabeni na hiyo penati itakayotaka pigwa na serikali!!
 
Malipo ya madaktari mpaka wagome na watu wafe, lakini posho za wabunge, Tsh. 200,000/= kwa mkao mmoja na waningiziwa kwenye akaunti zao, ama kweli maisha bora kwa kila mtanzania yanawezekana bila serikali ya CCM.:photo:
 
Nimekipenda kipengele cha kumsimamisha uanachama mganga mkubwa wa serikali.
Inaonesha hakuna unafki hapo, na wanaweza kusimamia ajenda zao!
 
hii migogoro yoote, lakini alichoweza kufanya huyu mtu wa magogoni tangu huu mwaka uanze ni ziara ya mabwepande,yaani yuko kimyaaaaaaa kama hayupo,daaaaaaaah kwa kweli kwa usanii tu huyu jamaa hajambo duh.........
 
Hii kali Waziri wa Afya hajui kama Interns Doctor kama ni daktari kamili ama bado mwanachuo!! Ametolewa wapi huyu? Vigezo gani vilitumika kupewa uwaziri ktk wizara muhimu kama hii?
 
Siku zote nimekuwa nawaonea huruma sana madaktari!!
Ile wizara ya afya lazima ifumuliwe kabisa ukianzia na huyo nyoni!!
Kwa kweli madaktari msilegeze kamba bana hadi ikibidi kabeni na hiyo penati itakayotaka pigwa na serikali!!
Madaktari nawaunga mkono 100%, kazeni buti, msilegeze kamba hata kidogo. Tunaweza kuanza ni wizara kwa sasa lakini ikibidi, hata Rais apigiwe kura na bunge ya kutokuwa na imani nae, kwani haya yanayofanyika anayaona na yeye kama msemaji wa mwisho huwa haoneshi concern yoyote. JK OUT!
 
Sasa madaktari mmenena. Ila mmekosea kumpa ban fupi ya mwaka mmoja huyo mganga mkuu wa serikali. Alipaswa kupewa ban ya maisha. Hawa wataalamu wanaogeukia siasa halafu wakasaliti fani zao ni wasaliti wakubwa na adhabu kubwa sana ndio wanayostahili.
 
Hii kali Waziri wa Afya hajui kama Interns Doctor kama ni daktari kamili ama bado mwanachuo!! Ametolewa wapi huyu? Vigezo gani vilitumika kupewa uwaziri ktk wizara muhimu kama hii?

Unashangaa hilo wakati katibu mkuu wake co doctor!!!!Hii wizara ina walakini nyingi 2 na inabidi waivunje yote then waiunde upya.
 
Nawaunga mkono ma DR, maadam tu mbeloe ya safari wasifanye kama ya Gratian Mukoba, makeke mengi kisha kimyaaaaaaaa anaingia mitini
 
Huyu Deo Mtasiwa niliwahi kuinteract nae kikazi wakati fulani, kwa kweli sishangai uharibifu anaoufanya kwa sasa. Kiufupi ni fisadi, mfitini, mwanamajungu, mwenye visa, mtata, asiyeijua kazi yake, asiyethamini sayansi na mtu wa kuzira...
 
Napata shida kidogo hapa naomba ufafanuzi kwa hili,huyu mganga mkuu wa serikali kama amefutiwa uanachama na MAT ina maana kwamba sasa hivi hatambuliki kama daktari na kama ni hivyo basi hana mamlaka ya kutekeleza majukumu ya kidaktari ktk kipindi hicho alichofungiwa sasa hiyo nafasi yake ya CMO anaachia ngazi ama inakuwaje?
 
Yote hayo kiini chake posho ambazo serikali inaona watumishi muhimu kuzawadiwa ni wabunge badala ya hawa wenye taaluma adimu katika kulinda na kuokoa uhai wa binadamu. Sasa hapo ndipo wakulu wanapoona viti vya sponge vimeota miiba ghafla na kuanza safari zisizoisha kutuliza nerves.
 
9 Reactions
Reply
Back
Top Bottom