Madai Yangu

Chapakazi

JF-Expert Member
Apr 19, 2009
2,874
310
Madai yangu makubwa ni kupata expenditure za Rais, Makamu wa Rais na Waziri Mkuu kwa mwezi. Naweza kupata wapi hizi data? Na je, Bajeti zao kwa mwezi ni kiasi gani? Ninataka expenditure zao za pesa za umma tu. Sijali juu ya pesa zao binafsi.
Kuna mtu anajua Bajeti ya Rais akisafiri? Je, sio haki yangu kama mlipaji wa hiyo safari kujua hilo?
Tukitoka hapo tunakuja mawaziri, wabunge, wakuu wa wilaya, mikoa mpaka diwani.
Lakini tuanze na hao wa juu kabisa.
Kama ni siri, kwa nini iwe hivyo?
 
ninavyojua mimi maofisa wa kawaida serikalini wanalipwa dola za usa 350 kwa siku wakiwa nje ya nchi,.sijui level ya rais na na wengine wa juu ila ukisoma nyaraka za serikali utapata
 
ninavyojua mimi maofisa wa kawaida serikalini wanalipwa dola za usa 350 kwa siku wakiwa nje ya nchi,.sijui level ya rais na na wengine wa juu ila ukisoma nyaraka za serikali utapata

hiyo sio bajeti mkuu! bajeti ni mpangilio wa matumizi, sasa info yako hainisaidii chochote...
 
ukijua unaweza kufa ghafla, bora tu usijue! manke analipwa some USD milions na hatumii hata senti moja, ubalozi wa nchi anakokwenda ama viongozi wa seriali wa mikoa ama wilaya anazotembelea huandaa kila huduma atakayohitaji yeyey na msafara wake/ isitoshe maisha yao ya kila siku na jamaa zao wa karibu yanagharimiwa na serikali popote walipo duniani!hakuna kazi yenye maslahi makubwa kuliko hizo hapa tanzania, na sitashangaa kama ni afrika au hata duniani kwa ujumla.

anko wewe bora ubaki hivyohivyo bila kujua, BP ya kujitakia ya nini?
 
ukimchunguza bata huwezi kumla,just chill down na endelea na life lako mkuu .
 
response kama hizo ndo sitaki kuziona! Tunaendekeza ujinga kwa maneno ya kiswahili. Mnategemea kuendelea vipi kama hamuwezi kusimamia viongozi wenu? Wewe unadhani kwa nini Uingereza, Ufaransa, Marekani, nk kulikuwa na mapinduzi? As long as i pay taxes, i have the right to know how and where my money is spent!!
 
kwanza kuna watu wanasema Rais akisafiri wanaenda kuchukua hela Hazina na hakuna anayeuliza chochote. Je hili lina ukweli?
 
Ndugu yangu wewe hakikisha unapata kamhogo kako kila siku.

Okay...inaelekea kuna ugumu wa uelewa kwenye hii ishu! Ngojea niweke kwenye point based system.
1. Ni kosa la jinai kwangu mimi kukwepa kulipa kodi (tax evasion)
2. Kodi yangu inatumiwa na serikali katika mambo kibao.
3. Ni kosa kwangu kutaka kujua hiyo bajeti?

Kwa nini inakuwa ngumu kwa waTz kuelewa kuwa kujua matumizi ya kodi yako ni HAKI YAKO? Na kwa nini ukubali haki yako imsafirishe mjinga mjinga kila siku kwenye vikao visivyokuwa na maana?
Hamuoni kuwa huo ni wizi?
 
Jamani chapa kazi atauwa mtu na pesa zake, hebu mwenye data ampe.
Nafikiri hii safari ya Paris imezidi kumtia hasira ndugu Chapa kazi
 
Back
Top Bottom