Hakuna sababu ya kuomba michango ya mafuriko ya Hanang, Serikali isaidie wananchi kwa pesa zake

Zygot

JF-Expert Member
Apr 14, 2016
2,240
2,866
Rais na umati mkubwa wa Watanzania wenzetu wako Dubai kwa raha zao na kwa matumizi makubwa ya pesa za umma. Je, pesa za safari ya umati wote huo imetoka wapi? Sasa kuna magari ya kifahari yanaelekea Hanang bila msaada ndani yake.

Serikali inaendeshwa kifahari kwa magari ya bei kubwa bila kujali maisha duni ya wananchi, lakini huwa haiombi misaada ya kununua magari hayo. Hii ni pamoja na wizi wa pesa za serikali, Rais anaona ni powa tu. Kitengo cha maafa kina bajeti ya kila mwaka, lakini majanga kama haya hayatokei kila mwaka. Je, pesa hiyo hupelekwa wapi?

Kwa ufupi tuache kutumia visingizio vya mafuriko kutaka michango ya watu walio na mahitaji kibao katika familia zao, na hawana msaada wa serikali, lazima serikali isaidie wananchi wa Kateshi kwa pesa zake yenyewe.

Pia soma > Manyara UPDATE: Waliofariki kwa Mafuriko Wilayani Hanang wafikia 63
 
Serikali hii haina tofauti na mkulima anayecheza ngoma kila baada ya mavuno, kukiwa na mgonjwa anaomba msaada.

CCM walikuwa na kikao cha kifahari wakijidai ni semina ya mafunzo. Sasa hivi wako kimya bila hata mchango wowote. Mwananchi yeyote akijichanganya tu akatoa pesa yake, ameliwa. KUna taasisi zitaanza vihelehele vya michango ya kulazimishana ili wapewe teuzi. Wajue pesa itapigwa tu!
 
Kuna mtu kasema majirani zetu mbona hawajigusi, watajigusaje wanapoona viongozi wamejazana huko na magari ya kifahari? Ni sawa na kutakuka kupeleka msaada kwa mtu ambaye Yuko bar anafuja pesa na vimada.
Hilo nalo neno Mkuu.

KaziKweliKweli/JobTrueTrue
 
Serikali ina pesa za bajeti,hizo pesa zimetoka kwa walipa kodi,ambapo hata hao waliopata majanga,hulipa kodi,kwanini isitoe hizo pesa wakawasaidia hao wahanga?
Ntashangaa sana pesa za serikali,ambazo ni zetu indirectly,zikomee kwenye malipo ya pesa za safari za viongozi ambao wala siyo wahanga.Wawe na utu basi,na siyo kila mmoja kufoji safari ya kwenda Qartesh ili ahalalishe ulipwaji wa posho ya safari.
 
Rais na umati mkubwa wa Watanzania wenzetu wako Dubai kwa raha zao na kwa matumizi makubwa ya pesa za umma. Je, pesa za safari ya umati wote huo imetoka wapi? Sasa kuna magari ya kifahari yanaelekea Hanang bila msaada ndani yake.

Serikali inaendeshwa kifahari kwa magari ya bei kubwa bila kujali maisha duni ya wananchi, lakini huwa haiombi misaada ya kununua magari hayo. Hii ni pamoja na wizi wa pesa za serikali, Rais anaona ni powa tu. Kitengo cha maafa kina bajeti ya kila mwaka, lakini majanga kama haya hayatokei kila mwaka. Je, pesa hiyo hupelekwa wapi?

Kwa ufupi tuache kutumia visingizio vya mafuriko kutaka michango ya watu walio na mahitaji kibao katika familia zao, na hawana msaada wa serikali, lazima serikali isaidie wananchi wa Kateshi kwa pesa zake yenyewe.
Nchi Yetu tupo katika usingizi mzito wa PONO. Tumelalaaaaaaaaaaa na sijui lini tutaamka.

Tubali bila kukwepesha macho na kunyoosha maneno..Tuna "OMBWE la UONGOZI" Bila kuwa na makusudi ya dhati kama Taifa, kutoka hapo, basi tuendelee Kulala Usingizi wetu wa PONO.
 
Rais na umati mkubwa wa Watanzania wenzetu wako Dubai kwa raha zao na kwa matumizi makubwa ya pesa za umma. Je, pesa za safari ya umati wote huo imetoka wapi? Sasa kuna magari ya kifahari yanaelekea Hanang bila msaada ndani yake.

Serikali inaendeshwa kifahari kwa magari ya bei kubwa bila kujali maisha duni ya wananchi, lakini huwa haiombi misaada ya kununua magari hayo. Hii ni pamoja na wizi wa pesa za serikali, Rais anaona ni powa tu. Kitengo cha maafa kina bajeti ya kila mwaka, lakini majanga kama haya hayatokei kila mwaka. Je, pesa hiyo hupelekwa wapi?

Kwa ufupi tuache kutumia visingizio vya mafuriko kutaka michango ya watu walio na mahitaji kibao katika familia zao, na hawana msaada wa serikali, lazima serikali isaidie wananchi wa Kateshi kwa pesa zake yenyewe.
Kuna thread imepandishwa humu kuwa sadaka ya mavuno ya katoliki Jimbo la Dar ni 4.5B... ikatwe nusu ipelekwe huko Hanang
 
Naunga mkono hoja, matumizi ya serikali yamekuwa makubwa hasa kwenye anasa, ila maafa yakija wanapitisha bakuli.

Kazi ya serikali ni kuhudumia watu wake.
Hiyo ni kazi ya serikali inayojielewa.Isiyojielewa inafanya kinyume chake.
 
Back
Top Bottom