MADAI: Afisa Mikopo Chuo cha IFM Dar atafuna hela za kujikimu za wanafunzi na kuwatesa wanafunzi

MTUNZA AMANI

Senior Member
Jun 2, 2012
187
21
AFISA MIKOPO NA UONGOZI WA IFM WAWATESA WANAFUNZI KWA KUTOWAPATIA HELA ZAO ZAKUJIKIMU ZA WANAFUNZI NA KUWATESA WANAFUNZI

Inasikitisha sana kwa wanafunzi wa IFM tangu chuo kimefunguliwa wanafunzi hawajapewa fedha zao za kujikimu.

Mbaya zaidi umeshapita takribani mwezi mmoja na wiki kadhaa. Bodi ya mikopo imepeleka fedha lakini uongozi wa chuo hautaki kuwapa wanafunzi fedha hizo.

Huu ni mwendelezo wa tabia mbaya na chafu ya Afisa mikopo wa IFM pamoja na uongozi wa chuo kuendekeza kutumia fedha zitumwazo chuoni hapo kujinufaisha wao binafsi badala ya kuwapa haki yao watoto hawa ambao wengi wao wanatoka mikoani.

Mamlaka zinazohusika hasa Mh Waziri mwenye dhamana Mh Joyce Ndalichako naomba aingilie kati suala hili, pia mkurugenzi wa bodi ya mikopo kama ameona ujumbe huu afatalie jambi hili.

Nakumbuka kauli ya Mh. rais aliwahi kukemea tabia hii alipokua anahutubia katika moja chuo hapa nchini.

Na aliagiza kua Maafisa mikopo wanaofanya mchezo huo kufukuzwa kazi.
Swali kwanini Afisa Mikopo IFM anacheza mchezo huo na kusababisha adha kwa wanafuzni hasa dada zetu ambao hujikuta wanaingia kwenye mtego wa kujiuza ili wapate hela ya kujikimu.

Naomba mamlaka zote zinazohusika wafatilie jambo hili kwa kina ili kuwanusuru watoto hawa.
 
ww upo karibu hapo na ikulu,ifm na ikulu ni karibu nenda hapo mwambie mheshimiwa wetu au nenda pale ilala bomani suala lako litapatiwa ufumbuzi haraka sana.
 
Upumbavu huu.. unataka kusema IFM hakuna balance and checks accounting procedures..?? Mtu mmoja anawezaje kutoa pesa bank bila authorization ya mwingine au checked ya mwingine..??
 
Hata sisi tulipokuwa tunasoma tuliwahi kutamka kuwa pesa yetu ya kujikimu imewekwa kwenye 'Fixed Account' na viongozi wa chuo ili wajipatie faida kutokana na pesa yetu. Lakini kiuhalisia mikopo kuchelewa kutolewa kwa wanafunzi kunasababishwa na mambo mengi sana kama ukifuatilia kwa umakini. Maafisa mikopo wa vyuo sio wa kulaumiwa na wala hawana ubavu na hawawezi kula pesa za wanafunzi, hata mkuu wa chuo hana jeuri hiyo. Kuweni wavumilivu tu pesa yenu mtaipata taratibu zikishakamilika, disbursement ya students' loans sio sawa na kugawa test za mtihani.
 
Back
Top Bottom