Mada maalum: Karibu tujadili masuala yote kuhusu Mikopo ya Elimu ya Juu

na kuna vyuo vingine registration inaelekea mwishoni kama SUA system ya kuregister inafungwa kwa sisi watoto wa makapuku tunaotegemea mikopo ndoto zetu ni km zinaenda kufifia hatujui tufanye nini pesa majumbani hawana......loooh! Mungu sasa aingilie kati hiyo issue tumechoka na ahadi
Ni maumivu kwa watoto wa wanyonge wengi ndoto za kupata elimu ambayo ni HAKI muhimu katika maisha inaelekea kupotea na hii inakatisha sana tamaa.
 
Zoezi mpaka limeshakamilika, ni wanafunzi 20,183 tu waliopata mkopo kati ya 88,163 ambayo ni sawa na asilimia 23%. Jiulize, asilimia 77 watafanyaje!!!? Kwa Tanzania hii tunakoelekea siko kabbisaaaaa
 
wew umesoma kindagateni , 3m , olevel, 4kwa mwaka , alevel ukasoma , 4.5m kwa mwaka
je bado unahitaji mkopo tu
 
UTOAJI WA MIKOPO KWA WANAFUNZI MWAKA 2016/2017
Baada ya kukamilisha zoezi la Uchambuzi wa maombi ya Mikopo 88,163 yaliyopokelewa hadi kufikia tarehe 11 Agosti, 2016. Jumla ya Wanafunzi wapya 20,183 wamepangiwa Mikopo. Upangaji huu umezingatia vigezo vilivyomo katika mwongozo wa utoaji wa mikopo uliopitishwa na Bodi ya wakurgezi na kuidhinishwa na wizaya ya elimu sayannsi na teknoloji. Vigezo hivyo ni pamoja na:

I. Vipaumbele vya kitaifa vinavyoendana na Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Miaka mitano, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mafunzo ambayo yatazalisha wataalamu wanaokidhi mahitaji ya kitaifa katika fani za kipaumbele ambazo ni;
• Fani za Sayansi za Tiba na Afya,
• Ualimu wa Sayansi na Hisabati,
• Uhandisi wa Viwanda, Kilimo, Mifugo, Mafuta na Gesi Asilia,
• Sayansi Asilia, na
• Sayansi za Ardhi, Usanifu Majengo na Miundombinu.

i. Uhitaji wa waombaji hususani wenye mahitaji maalum kama vile ulemavu na uyatima
ii. Uhitaji wa waombaji wanaotoka katika familia zenye hali duni ya kimaisha
o Wadahiliwa yatima waliopata mkopo 873
o Wadahiliwa wenye ulemavu wa viungo 118
o Wadahiliwa wahitaji wenye mzazi mmoja 3,448
o Wadahiliwa wahitaji waliofadhiliwa na taasisis mbali mbali 87
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi za kipaumbele 6,159
o Wadahiliwa wahitaji wanaosoma kozi zingine 9,867
Jumla 20,183

Kiasi cha Fedha zinazohitajika
Bajeti iliyoidhinishwa kwa ajili ya ukopeshaji kwa mwaka wa fedha wa 2016/17 ni shilingi bilioni 483, kwa ajili ya jumla ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wapatao 25,717, na wanaoendelea na masomo wapatao 93, 295.

Hatua zinazofuata
I. Wanufaika wote wanaopungukiwa na sifa watachunguzwa kwa ajili ya kurekebishiwa au kuondolewa katika unufaika wa mkopo
II. Waombaji waliwasilisha taarifa zenye upungufu, taarifa zao zitahakikiwa, na wakibainika kuwasilisha taarifa za uongo watachukuiwa hatua stahiki ikiwa ni pamoja na kufutiwa mikopo yao
III. Wanufaika wote watatakiwa kuhuisha taarifa kwa kujaza dodoso. Taarifa za ziada za kiuchumi za wazazi au walezi wao zitatumika kutanua uhalisia. Wale watakaokutwa na hadhi zisizo stahili, watapoteza sifa za kuendelea kupata mikopo na kulazimika kurejesha kiasi watakachokuwa wamepokea tayari.

IMETOLEWA NA:
MKURUGENZI MTENDAJI
BODI YA MIKOPO YA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU
Hizi ni sawa na zile hadithi za kale"ngano" zisizo na maana kwa sasa sababu wanafunzi wanalia na kusaga meno huko vyuoni sasa HESLB wanaendelea kuleta hizi ngano zinamsaada gani?
Kama wameshindwa kutoa mkopo ni bora waseme ukweli watu wafahamu.

Vigezo vya means testing, mara matamko ya kutotoa mikopo kwa wanaonunua TV na pombe vyote ni visingizio na kutafuta kichaka cha kujifichia.
 
asee jamaa mimi sikuelewagii asee mbonaa ulikuwaa unadai unafanyaa kazii TCU vp saivii unatakaa tenaa mkopoo au TCU wamekuambia ukasomee teenaa...????????
Humu JF kuna watu wanadhani wakitumia fake ID wanasahaulika jamaa anaboa
kama huyo mchizii wa TCU hahahaaa
Mods wafunge hii thread maana ni dhahiri kwamba huyu jamaa anatoa taarifa za uongo. Mwaka Jana alikuwa anafanya kazi TCU, mwaka huu anameomba kupitia TCU kajichagua kozi ya afya na mkopo kakosa halafu analalamika, wakati ni dhahiri kuwa sifa za kupata mkopo hana.
 
Naomba kuuliza dawati hili kwa wadau wa elimu na wanufaika wa bodi ya mkopo, kuna habari zinasambaa na kunikuta jioni hii kwamba, kwa yeyote ambayo alikuwa na sup au carry hadi mda huu hana sifa ya kupata mkopo, kwa maelezo yao ni kwamba

SOURCE NI MKURUGENZI BODI YA MIKOPO NA IMETOLEWA LEO KWENYE #E NEWS YA EATV.

Nauliza kama kuna ukweli hapo ndani yake
 
Hizi ni sawa na zile hadithi za kale"ngano" zisizo na maana kwa sasa sababu wanafunzi wanalia na kusaga meno huko vyuoni sasa HESLB wanaendelea kuleta hizi ngano zinamsaada gani?
Kama wameshindwa kutoa mkopo ni bora waseme ukweli watu wafahamu.

Vigezo vya means testing, mara matamko ya kutotoa mikopo kwa wanaonunua TV na pombe vyote ni visingizio na kutafuta kichaka cha kujifichia.
daah ni kweli bora wawe wawazi ili ambao hatuna uwezo tuandike barua za kuairisha mwaka
 
Back
Top Bottom