Mabraza wa enzi hizo Dar kumbukumbu zangu

ILIKUWA VITA KUNA MAKUNDI YALIKUWA YANA JIITA CHEARSE SIJUI
Kuna bro alikua anaitwa jeshi.....alitokea block 41...wengine akina membe......mwengine Ninja....mwingine Kambanga.....akina Hafidhi.....na wengine wengiii...
Tambaza walikua wamepinda kuliko Azania......na yile aliyejiua baada ya kumpiga denti mwanafunzi.....Its been long time bro!!!! Nazungumzia 1992 hapo
 
Kuna bro alikua anaitwa jeshi.....alitokea block 41...wengine akina membe......mwengine Ninja....mwingine Kambanga.....akina Hafidhi.....na wengine wengiii...
Tambaza walikua wamepinda kuliko Azania......na yile aliyejiua baada ya kumpiga denti mwanafunzi.....Its been long time bro!!!! Nazungumzia 1992 hapo
ugonvi wa makonda wa dalala na wanafunzi pale fire unakumbuka ulisababisha kifo cha mwanafunzi
 
Mcheki Pascal Mayala mzee wa diplomasia akupe darassa......sisi tushazeeka mdogo wangu🤣🤣🤣
shida nyingine huyu Pascal Mayalla mimi ni mkwe wangu 🤣 ila ni miongoni mwa watu ambao nawakubari sana....!

nipe mbinu hata za kwenda mbele huko nikajaribu bahati... passport ninayo kaka mkubwa.... fanya jambo​
 
Kuna bro alikua anaitwa jeshi.....alitokea block 41...wengine akina membe......mwengine Ninja....mwingine Kambanga.....akina Hafidhi.....na wengine wengiii...
Tambaza walikua wamepinda kuliko Azania......na yile aliyejiua baada ya kumpiga denti mwanafunzi.....Its been long time bro!!!! Nazungumzia 1992 hapo
Puzo mtoto wa ubungo ..mdg wake wakuitwa aliko
 
Ila Maisha ya Tambaza na Aza Boy ni kitabu ambacho kimewatoa wengi sana.
Hizi shule miaka 1990 zilikuwa hub inayowaunganisha watoto wa kiburugwa, buza, tandika, keko, mzambarauni, kisukuru, mabibo, sinza Tandale, magomeni, Kinondoni, Kariakoo, kitunda n.k na watoto wa kishua kutoka Masaki, Obei na Upanga.
Wana kutoka Uswahilini walikuwa wanakuwa inspired na kuiona dunia mpya kupitia maisha ya watoto wa Kishua, na Watoto wa Kishua nao walikuwa inspired na lifestyle ya wana wa magetoni hali iliyofanya waone umuhimu wa kutengeneza bond.
Inspiration hiyo imekuwa chachu ya kuwahamasisha wana wa magetoni kufanya juhudu za kuvunja minyororo ya umasiki na kadhaa wametoboa kimaisha.
Sasa hivi ukikutana nao haujui yupi wa Gomzi na yupi wamasaki
 
Kuna visa kadhaa sitavisahau katika maisha ya Aza Boi

Tukio la wana kutoka Tambaza kutembea kwa mguu kutoka Tambaza kupitia muhimbili Hospital na kuvamia Azania. hasa jaribio lao lililoshindwa la kuichoma chemistry lab kwa mabomu ya petrol yaliyotengenezwa kwa chupa za bia safari. Mapigano yaliyotokea uwanja wa mpira pale azania kwangu ilikuwa maajabu.

Nilikuwa kila siku napita Kariakoo kutokea uswahilini kwa mguu kuelekea Azania, sasa pale Kariakoo kulikuwa na dada/mama kiwete anatembea kwa magoti na mikono. Nikifika alipo lazima nisimame nimwangalie jinsi kiuno na makario ya yalivyokuwa yanacheza kwa kugombana akitembea ingawa alikuwa machafu sana. Cha ajabu kila mwaka alikuwa ana zaa mtoto hadi namaliza Olevel alikuwa na watoto wanne na wowowo likawa balaa zaidi. siku moja uzalendo ukanishinda nikamuuliza imekuwaje na speed kubwa ya kuzaa. Akanambia kuna wazee kila usiku ukifika wanakuja kumchukua na magari yao wanaenda kumla. sijui yupo wapi huyo mama kwa sasa.

Pale nje ya Azania barabarani kulikuwa na mabanda machafu ya mihogo. Ile Mihogo wanafunzi walikuwa wanaiona mitamu balaa, kiasi kuigombea.

Kuna siku Madaktari wanafunzi wa Muhimbili walifika Azania kutoa Elimu ya Magaonjwa ya Zinaa, hivyo Jangwani na azania wote kwa pamoja wakaalikwa kusikiliza. Sasa ikafika kipindi ikawekwa video inayoonyesha K inavyolika na kuharibika kutokana na magonjwa ya zinaa. Kuona hivyo wana wakaanza kuwazomea mademu na kuimba kuwa hawawataki kwamba revola inatosha. Mademu wa Jangwani wote walikimbia Ukumbini kabla seminar haijaisha.

Tulikuwa tunatembea kwa Mguu kutoka Azania hadi mzimuni kila siku kisa tuition. Sasa tukifika tuition nusu yetu tunamkopa mwalimu. Heshima kwa walimu wote waliokuwa wanaruhusu watoto wa masikini wasome tution bure.
 
Cool Moe Cee (Mosi) Mnyamwezi fulani hivi alikuwa ana hang sana na Kwanza Unit na watoto wa IST.

Jamaa alitoka Marekani miaka ile akarudi Bongo akazibuka Kinyamwezi ile mbaya.

Jamaa anadunda mpaka unaona kama ardhi itatetemeka hivi.
Nimecheka sana hapo jamaa anadunda mpaka unaona kama ardhi itatetemeka hivi.
 
Back
Top Bottom