mabomu yatumika kutawanya mandamano ya CUF

Re: mabomu yatumika kutawanya mandamano ya CUF
Tusishabikie kwa mawazo hasi, tunapaswa tushangae nchi yetu inaelekea wapi maana kila kona maandamano
- Chadema Arusha - uchaguzi bomu wa meya
- Chadema Kigoma - uchaguzi bomu wa meya
- Chadema nchi nzima - upandaji bei umeme
- CUF - Katiba mpya
- Chadema - Katiba mpya
- UDOM - mazingira duni ya kusomea
- Ardhi University - mikopo ya elimu
- Muhimbili???
n.k.
Hivi si vitu vya kuchekelea, tunatakiwa tujiulize wapi pana shida ili parekebisho badala ya kushabikia. Amani ikitoweka mimi na wewe hatutapata fursa ya kukaa mbele ya Laptop/handset na kuandika ushabiki kama tunavyofanya sasa.

jaji werema - dowans lazima walipwe
 
naam kumekucha

kwa kweli haya mambo yanahitaji vyama vya siasa kukaa na kujiangalia pamoja na jeshi la Polisi

watanzania tumechoka kusikia vurugu za kijinga kila uchao mara CUF na Polisi mara Chadema na Polisi ni upuuzi mtupu

kaeni mtazame jinsi ya kuendesha siasa za kistaarabu hebu igeni CCM

huenda na wewe una kaswende ya ubongo!
 
Haki ya nani tena nilipomuona huyu jamaa anagombea ubunge kupitia CUF nilijua haya yatatokea, rijamaa migomo ipo kwenye damu, jana nilimskiliza akiongea kwenye habari du linatisha hili, sijui limetoka wapi, chuo kikuu walishapigwa sana mabomu kwa ajili ya hili lijamaa, kuweni makini wanaCUF kama ni kwa maslahi ya wananchi haya ila isije kuwa ni kwa maslahi ya watu flani flani halafu nyie mteseke.kuna watu walikula sana shavu chuo kikuu pale kwa sababu ya migomo na wengine waliishia kuteseka na kufukuzwa chuo, sina uoga maana wanaJF mwaweza kusema naogopa LA HASHA ila nataka watu wakigoma na kuandamana basi iwe ni jambo la msingi,wafanye tathmini kwanza la sivyo MUTATIRO JULIUS atawatembeza barabarani hadi mkome
 
Watu tunaoona mbali tumeshalisema hili mara nyingi, sioni hata haja ya kuchangia chochote kwenye thread hii, sasa wewe uliona wapi chama tawala kikaandamana kuipinga serikali yao wao wenyewe? maalim seif ndio katibu mkuu wa CUF je alikuja kuongoza hayo maandamano?
Huyu kijana anayeitwa Mtatiro nadhani ana kaswende ya ubongo, anadhani anaweza kupata public sympathy kirahisi kwa movement za kitoto namna hii. sisi Watanganyika asije akazani anaweza kutufananisha na wapemba, wenye chama chao cha Cuf wanajulikana wazi ni Lipumba na Maalim Seif, na wao wamekaa pembeni hivi mtu unaejuwa namna nzuri ya kufikiri unaweza kumsikiliza mwehu kama mtatiro?
wapemba wengi wamepoteza maisha yao kule pemba kwa sababu ya mwehu mmoja tu ambaye shida yake ilikuwa ni tumbo lake tu, wanafikiri hapa Tanganyika kuna majuha wa kuwaingiza mkenge huo?
Angalizo: Asiyekijuwa vizuri chama cha CUF aende kwa Profesa Abdalah Safari atapata kuijuwa CUF.
kaka pole sana kwa machungu uliyonayo juu ya mtatiro, mtaongea sana, mtakasirika sana, but the fact remain that the guy is more useful to this nation than a millions of your type, he is brave, daring and courageous lakini kwa kuwa wabongo zenu hamtaki kuona mwenzenu anafanya kitu roho yake ipendacho na anafanikiwa basi mtabaki kuchonga na kutoa kasoro.
Huyo profesa si aje mwenyewe hapa aseme yaliyomkuta huko cuf? na anangojea nini huko cuf kama hakufai? Halafu, who gives you the mandate ya kumwita mtatiro mwehu au ana kaswende ya ubongo/ wewe umefanya nini katika taifa hili? nikisema wewe ndo una kaswende ya ubongo ntakua nakosea? maana mtu mwenye akili timamu hawezi kuja kumu attack mtatiro hapa kisa anafanya movement za kudai katiba mpya, you must be sick.
 
Nasisitiza CUF hawakuwa na grounds za kuandamana.Nilimsikiliza Kova kwa makini alisema kwamba,hakuna sababu ya msingi ya maandamano kwani serikali haijakataa hoja ya katiba mpya (though wanaonekana kutaka kuiwekea viraka iliyopo).For sure hali haijawa shinikizi kiasi hicho kiasi cha kuhitaji maandamano.Kinachoonekana ni CUF kupambana ktk kile kinachoonekana kutaka kuteka agenda ya Katiba Mpya ionekane ni yake.Si wangemsusia JK bungeni na wao?
 
Kaazi kweli kweli!!!
Hivi tunataka kuandika ngonjera au katiba? kwanini watu wazima wasikae watulie wakaandika katiba ya kueleweka kama issue ni katiba au kama ili kuwa kukabidhi rasimu ya Katiba ya CUF maandamano ya nini? si mpeleke kama Mnyika alivyo peleka hoja yake ofisi ndogo ya Bunge? waandishi wa habaro walikuepo and nobody was hurt ustaarabu kitu cha bure! and remmember lazima ijadiliwe wala si mwisho wa discussion unless CUF wanadhani lazima vyama vyote vikubaliane nao!!! Hivi wanajua maana ya katiba ya nchi? LAAAAAAAAAAAZIMA TUIKUBALI WOOOOOOTE !!!!!!!!!!!!!!!!! DO YOU UNDERSTAND? YOU CAN ANDAMANA AS YOU LIKE LAKINI MWISHO WA SIKU TUTAKAA TUIJADILI AND WE SHALL HAVE TO AGREE TO DISAGREEE ON SOME ISSUES!!. I am out.
ni hapo mnapokuwa washabiki wa vyama hadi reasoning inawatoka, just common sense my God. Nani kasema kudai haki kuna njia moja tu ambayo ni aliyoitumia mnyika na chadema? give me a break. kila tatizo lina options tofauti za kutatua. kama mnyika alitumia hoja binafsi, mtatiro aliamua kutumia maandamano ya amani ambayo ni haki ya raia, ila kwa kuwa ccm yenu na polisi wenu wasivyotumia akili kazi yao kuzuia maandamano ya vyama vya upinzani huku ccm wakitaka kuandamana hata kumpokea makamba akitokea dodoma wanaruhusisa. think, msiwe tu washabiki, badala ya kuwatia moyo hawa vijana wanaofight kwa ajili ya mema ya nchii kila siku kazi yenu ni kuwa discourage huku mmetulia kwenye viti na computa za wahindi maofisini doing nothing. Kila inachofanya chadema ndo mnaona kinafaa, vyama vingine hata vikifanya kitu kizuri hamkubali wala kusifia kazi yenu kutoa makosa tu. Ingekuwa ni chadema ndo wameandamana leo polisi wakafanya walichofanya, hapa mngekuwa mnaongea story tofauti, acheni unafiki, hizi double standards, hazimsaidii yeyote, mwisho wa siku wote mnakuwa loosers na ccm wanazidi kupeta.
 
Watu tunaoona mbali tumeshalisema hili mara nyingi, sioni hata haja ya kuchangia chochote kwenye thread hii, sasa wewe uliona wapi chama tawala kikaandamana kuipinga serikali yao wao wenyewe? maalim seif ndio katibu mkuu wa CUF je alikuja kuongoza hayo maandamano?
Huyu kijana anayeitwa Mtatiro nadhani ana kaswende ya ubongo, anadhani anaweza kupata public sympathy kirahisi kwa movement za kitoto namna hii. sisi Watanganyika asije akazani anaweza kutufananisha na wapemba, wenye chama chao cha Cuf wanajulikana wazi ni Lipumba na Maalim Seif, na wao wamekaa pembeni hivi mtu unaejuwa namna nzuri ya kufikiri unaweza kumsikiliza mwehu kama mtatiro?
wapemba wengi wamepoteza maisha yao kule pemba kwa sababu ya mwehu mmoja tu ambaye shida yake ilikuwa ni tumbo lake tu, wanafikiri hapa Tanganyika kuna majuha wa kuwaingiza mkenge huo?
Angalizo: Asiyekijuwa vizuri chama cha CUF aende kwa Profesa Abdalah Safari atapata kuijuwa CUF.
[/QUOTE

Msubirini bwana wenu Silaha aandame ndio muunge mkono. Kumbe mnashabikia watu sio jambo linalohusu maslahi ya Taifa? kweli Tz ni zaidi ya uijuavyo. Hawa ndio % kubwa ya Watz tulionao, wakati mwingine hata hamjui kinachoongelewa zaidi ya ushabiki tu. Poleni sana.

Sasa tushabikie walishatuonesha Rasimu yenyewe? Hata hao waliopigwa mabomu sijui kama wameiona! Seif na Lipumba wanakula kiyoyozi huku mbumbumbu wanabugia moshi, kaaazi kweli kweli!
 
Nasisitiza CUF hawakuwa na grounds za kuandamana.Nilimsikiliza Kova kwa makini alisema kwamba,hakuna sababu ya msingi ya maandamano kwani serikali haijakataa hoja ya katiba mpya (though wanaonekana kutaka kuiwekea viraka iliyopo).For sure hali haijawa shinikizi kiasi hicho kiasi cha kuhitaji maandamano.Kinachoonekana ni CUF kupambana ktk kile kinachoonekana kutaka kuteka agenda ya Katiba Mpya ionekane ni yake.Si wangemsusia JK bungeni na wao?

here we go again? inakuwaje hoja ya kijinga kama hii inamjia mtu kichwani? eti cuf wanataka kuifanya hoja ya katiba mpya ionekane yao, whaat? mbona hamkui jamani? pls people grow up and think like mature people. katiba mpya inahitajika kwa ajili ya taifa zima lenye waislam, wakristo, wapagani weusi na weupe, wafupi na warefu wa chama cha ccm, cuf, chadema na hata wale wasio na chama. sasa inakuwaje watu wakiamua kutumia njia tofauti kuidai mnaanza eti wanataka kuifanya iwe hoja yao? hii ni hoja ya wananchi na siyo ya chama chochote.
Na Cuf kutomsusia JK walifanya cha maana coz what happened chadema waliposusia/ si hao wamerudi tena na kusema wanamtambua, what a shame? na huyo kova usimtetee, kwani wanaccm wanapokuwaga wanaandamana kuwapokea viongozi wao walioshinda uchaguzi dodoma au kutoka airport huwa ni sababu ya msingi kushinda hii ya katiba mpya?
 
Vyanzo vya habari kadhaa vyaarifu kuwa risasi za moto na mabomu zimetumika katika kutawanya maandamano ya CUF mitaa ya Buguruni hali haikuwa shwari asubuhi hii.

Bado CDM hiyo tarehe 5 January wanayo sema wanaandama, wao ndio tutawamaliza kabisa , asiguse mtu barabarani, na kama mnabisha hata mliomo humu JF ambao mlikuwa na nia ya kufanya hivyo jaribuni muone dola itakavyo wafanya
 
Sasa tushabikie walishatuonesha Rasimu yenyewe? Hata hao waliopigwa mabomu sijui kama wameiona! Seif na Lipumba wanakula kiyoyozi huku mbumbumbu wanabugia moshi, kaaazi kweli kweli!
sasa kwa attitude hii haata wangekuonyesha undeiangalia? unafikiri ukombozi wa nchi au taifa huwa unakuja kwa watu kukaa ofisini na kukatisha watu tamaa ? kila mahali penye ustaarabu na uhuru kuna watu walijitoa mhanga hata maisha, kama hao unaowacheka kwamba wamepigwa mabomu. sometimes huwa najiuliza kama kuna hata wazalendo wachache wamebakia kwenye hii nchi.
 
naam kumekucha

kwa kweli haya mambo yanahitaji vyama vya siasa kukaa na kujiangalia pamoja na jeshi la Polisi

watanzania tumechoka kusikia vurugu za kijinga kila uchao mara CUF na Polisi mara Chadema na Polisi ni upuuzi mtupu

kaeni mtazame jinsi ya kuendesha siasa za kistaarabu hebu igeni
CCM

Mtu wa pwani, polisi wanafanya hivyo kwa maslahi ya nani? CCM wana ustaarabu gani zaidi ya kukandamiza demokrasia? and then ni kipi kitaigwa kutoka CCM?
 
sasa dah cuf bwaana kwahiyo lipumba anataka uwaziri mkuu au umakamu kwa asilimia ngapi waliopata
 
Bado CDM hiyo tarehe 5 January wanayo sema wanaandama, wao ndio tutawamaliza kabisa , asiguse mtu barabarani, na kama mnabisha hata mliomo humu JF ambao mlikuwa na nia ya kufanya hivyo jaribuni muone dola itakavyo wafanya

Mwalimu wangu wa biology wakati akifundisha abdomalities za binadamu alisema wapo binadamu wengine akili zao zipo MAKALIONI,wewe ni mmoja wao!
 
kuna mambo mawili jamani:

waliofunga ndoa na ccm ni viongozi wa cuf.

wafuasi wao hawana habari, wao hawana taarifa kuwa wako ccm
 
si mbaya kuiga CCM kwa inavyojipanga na kujua ni wakati gani wa kufanya mikutano yake

na siku zote CCM inaweka mbele maslahi ya wananchama wake, kamwe hawawi wahanga na wengine wakastarehe

vyama vya upinzani wanapenda kuwafanya wafuasi wao kuwa ni ngao ya kufikia yao, ni aibu nzito kubwa kwao
 
C*F wamekariri kuwa kila jambo linahitaji maandamano,
vyama mbadala vioneshe kuwa vimekomaa na vinaweza kuchukua nafasi ya kuongoza nchi,
waache maamuzi ya kukurupuka kwa kutaka "cheap popularity"
 
Amanibaraka vipi hujawasuruhisha hao Mume na Mke?
AAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA CCM acha kupiga Mkeo. Aibu hiyo, mbona mmeoana hivi karibuni vipi hakumsomana vizuri tabia?

1.Mtego wa Noti « sasa mbona wanajibishia wenyewe? kwani wao si wako ndani ya serikali? sasa mbona wanatuchanganya?....anyway....ngoja wapigwe virungu...
....na bado.... «

2.Ledman Mtana. « Wanataka serikali ya mseto na bara. wameshaonja utamu huko zenji sio? »

3.Buchanan. « CCM - A inapambana na CCM - B, kaaazi kweli kweli! »

4.Maishapopote. « Hahahahhaha wavunjwe hata miguu »

Great thinkers

Munajidhalilisha kama uwezo wenu wa kufikiri ndio huu !

Yaani mtanzania mwenzako,anapigwa, anajeruhiwa au anauawa katika dai ambali wewe pia ungeandamana kama chama Chengine cha siasa kingeitisha maadamano hayo, sijui niite tabia gani !!

Hayo ya Polisi kupiga CUF inafaa muone kuwa CUF sio chama tawala kama wengi humu munavyotaka tuamini.

Halafu hili la kusema CUF kaolewa au wanalala kitanda kimoja inaonesha wazi vipi mawazo yetu yametawaliwa na fikra ya unyanyasaji wa kijinsia katika mila za hapa Tanzania. Tunaona wanawake ni watu wa « kufanywa tu »,kudharauliwa.

Tumesoma lakini hatujaelimika ! Fikra potofu. Munawatukana, munawadhalilisha mama na dada zenu na hizo dharau munazipeleka katika ulinganisho hata wa kisiasa.

Siku kibao kikiwageukia , nitawakumbushia thread hii.
Badilikeni kama tunataka mabadiliko ya kweli.
 
Huu ni ugomvi ndani ya team moja sisi hatuhusiki kabisaaa yanii First Eleven wanapigana na Team B? Wacha huyo chambo Mtatiro aone Serikali ya Mseto
 
Back
Top Bottom