Infropreneur
JF-Expert Member
- Aug 15, 2022
- 5,266
- 10,774
Habari wakuu wana jamii forums..
Moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu napenda kuzungumzia suala la mabishano ya kidini baina ya waumini wa dini mbalimbali hasa dini kuu mbili zenye wafuasi na waamini wengi duniani Ukristo na Uislamu...
Kwanza kabisa Binadamu yeyote anapozaliwa anakuwa hana dini,Hajui imani yeyote ile hadi pale anapofikia umri wa kujielewa na kuwa na ufahamu wa imani(Dini) inayomzunguka ndipo naye huanza kuingia kwenye imani hiyo kwa kufuata imani za watangulizi wake..Hapa watoto hufuata dini za wazazi wao na hufundishwa dini hiyo tangu wakiwa utotoni na kuendelea kukua nayo hadi ukubwani.Hapa kwa watoto wa dini ya ukristo huenda mafundisho ya kiimani ya ubarikio (Komunio, Ekaristi) na kipaimara pia watoto waislamu huenda madrassa kufundishwa pia imani yao ya kiislamu.
Kulingana na mafundisho ya dini zote mbili kila mtu huona dini yake aliyonayo ndio ya kweli na sahihi kuliko ya mwingine..mfano kwa dini ya kiislamu wana amini mtu yeyote asiye muumini wa dini ya kiislamu ni "kafiri" na hivyo hivyo kwenye ukristo wana amini yeyote asiye mkiri kristo kama mwokozi na mkombozi wa ulimwengu basi imani yake sio sahihi amepotoka kiimani.
Kutokana na mafundisho haya sasa,ndipo kumedumu na kushamiri "MABISHANO" makali kila siku miongoni mwa waumini wakibishana usahihi na ukweli wa dini zao.. mabishano haya ni sawa na mchezo wa "KUVUTA KAMBA" kila mtu hujaribu kuvutia na kutetea upande wake ili ashinde.
Hali ni tete zaidi kwa viongozi wa dini zote mbili,wengi wao huwafundisha na kuwa hubiria waumini wao kwamba imani au dini waliyopo ndio ya kweli na sahihi na endapo mtu yeyote yule atajaribu kuwashawishi kubadili dini au kuhama imani hiyo wapingane nae VIKALI mno, ikibidi kupoteza Maisha kabisa kutetea imani yao kwa kigezo eti ndio watapata thawabu na baraka za mwenyezi Mungu.Hii imepelekea vikwazo vingi sana kwa watu hasa kwenye suala la NDOA.. inakuwa ni vigumu sana kwa baadhi ya familia za kikristo na kiislamu kukubali utofauti wao kidini kwenye maswala ya ndoa hivyo inakuwa kikwazo kwa vijana wa dini mbili tofauti kufunga ndoa.
Kwa maoni, mtazamo na Ushauri wangu kwa jamii ni kwamba:Kila mtu anatakiwa aheshimu Dini (Imani) ya mwenzake kwa sababu kuu kwamba, kila mtu amezaliwa,amekulia, amefundishwa na kuaminishwa dini yake tangu utotoni na wazazi wake, hivyo asione dini ya mwingine "Haina ukweli na usahihi" maana hamna mwenye uthibitisho kamili wa "usahihi na ukweli" wa dini yake zaidi ya kuegemea na kujikita kwenye Maandiko ya kidini (Vitabu vya kidini,Biblia na Quran) vinavyo kinzana kwenye hoja mbalimbali hivyo kupelekea ubishi usio na mwisho.. nimalizie kwa kusema RELIGION IS NOT GOD.....
Karibuni kwa maoni, mitazamo na ushauri.kejeli na ubishi wa kuanza tena kutetea dini hapa haitasaidia kuelimishana...
Nawasilisha.kwenu wakuu!