Point yako ni nzuri sana, lakini hukuifanyia utafiti kwani hiyo inawezekana katika nchi ambazo wasiokuwa na kazi ni 10-15%. Kwa maneno mengine umeleta nadharia uliyosoma Ulaya bila kuitafsiri katika mazingira ya Afrika au Tanzania kama ukipenda.
Katika nchi kama Tanzania ambayo ina watu wasio na kazi mpaka kufikia 35% hiyo nadharia haifanyi kazi. Kwa vile suala la elimu sio la kungoja, ndio maana seriukali ikaja na mtindo- kama huna kazi basi pata kazi ya kujenga shule, vyatua tofali na kujenga na serikali kwa kutumia hizo kodi ndogo itajazia pale pesa inapohitajika.
Mkisoma ulaya, pindi mnaporudi nyumbani mnakazi kubwa sana ya kutafsiri hayo mliyoyasoma katika mazingira mnayofanyia kazi, vinginevyo elimu mliyosoma ni kazi bure.
Dada sio ulaya, piga hesabu ndogo tu, hizo pesa zilizoibwa kwenye EPA, RADAR, NDEGE YA RAIS, RICHMOND, MEREMETA, APTL, TWIN TOWERS na zingine nyingi tu zinazofujwa kwenye semina, safari za viongozi zisizokuwa na tija n.k unafikiri zingeshindwa kufanya kazi ya kujenga shule na kununua madawati? Angalia kiasi cha magogo yanayokwenda nje, kweli TZ ni nchi ambayo watoto wanatakiwa kukaa chini? Hebu angalia upotevu wa mabilioni kwenye halmashauri zetu (Pathetic!)
Issue kubwa inayoliangamiza taifa letu ni governance tu, tukiweza kwenye governance basi sidhani kama kuna nchi EAST AFRICA if not Africa inayoweza kutusogelea kwa maendeleo.