Mabadiliko madogo Baraza la Mawaziri yanalenga kumsogeza January mahali patakatifu?

Ngongo

JF-Expert Member
Sep 20, 2008
18,931
31,176
Heshima sana wanajamvi,

Nayatazama mabadiliko madogo baraza la mawaziri kama sehemu ya mkakati wa kumwinua January Makamba kuelekea kileleni (IKULU) baada ya Wizara ya Nishati kumshinda. Kuendelea kumbakiza wizara hiyo hiyo ilikuwa ni kumharibia kisiasa.

Najua watu wengi wamekimbilia kushangaa nafasi ya Naibu Waziri Mkuu Mh Dotto Biteko,lakini nyuma ya pazia WAZEE wa Msoga Camp safari hii hawataki kukosea kama ilivyokuwa kipindi kile cha 2015.Mzee Magufuli hakuwa chaguo lao mazingira au kivumbi cha Lowassa kiliwasababishia kufanya maamuzi bila hesabu sahihi.

January Makamba anaandaliwa maandalizi kabambe bila WAZEE wa Kanda pendwa kushtuka.Mchezo unaochezwa ni kuanzisha cheo kisichokuwepo kikatiba cha NAIBU WAZIRI MKUU kwa lengo la kuwazubaisha WAZEE wa Kanda pendwa kwamba kumbe wao ni sehemu ya walamba asali,hawana haja ya kulalamika wametengwa, hawapendwi, si sehemu ya watoto pendwa.

Vurugu za chama kileeeee kule kanda pendwa hakika kuwastua wapanga mikakati umuhimu wa kumwandaa mwanasiasa kutokea huko kwa lengo la kumtumia baadae kutimiza malengo yao hasa ahadi ya kuhakikishiwa nafasi ya Mzee wa Korosho.

January Makamba kapelekwa pale Foreign Affairs kupata uzoefu baada ya kushindwa vibaya sana Nishati.Katuachia mgao wa umeme,kashindwa kupanga na kupangika mfumo mzima wa manunuzi ya mafuta.Kaondoka Nishati hali ikiwa tete.

Mtangulizi wake Kalemani kasambaza umeme wa REA karibu vijiji vyote kaingia January REA hakuna kila kitu shabala bagala.NISHATI ilimshanda Makamba hana ujuzi zaidi ya kubebwa na mfumo wa walamba asali.
 
Heshima sana wanajamvi,

Nayatazama mabadiliko madogo baraza la mawaziri kama sehemu ya mkakati wa kumwinua January Makamba kuelekea kileleni (IKULU) baada ya Wizara ya Nishati kumshinda.Kuendelea kumbakiza wizara hiyo hiyo ilikuwa ni kumharibia kisiasa...
Huko mahala patakatifu atafanya kazi gani wakati hizi kazi nyepesi kashindwa
 
Heshima sana wanajamvi,

Nayatazama mabadiliko madogo baraza la mawaziri kama sehemu ya mkakati wa kumwinua January Makamba kuelekea kileleni (IKULU) baada ya Wizara ya Nishati kumshinda.Kuendelea kumbakiza wizara hiyo hiyo ilikuwa ni kumharibia kisiasa...
Uzuri wilbroad slaa anawaona... huyu mzee ana nguvu za ushawishi!! Chadema wacheze karata yao hapa.. kanda ya ziwa ni karata ya ushindi...!
 
Heshima sana wanajamvi,

Nayatazama mabadiliko madogo baraza la mawaziri kama sehemu ya mkakati wa kumwinua January Makamba kuelekea kileleni (IKULU) baada ya Wizara ya Nishati kumshinda.Kuendelea kumbakiza wizara hiyo hiyo ilikuwa ni kumharibia kisiasa...
Ujinga mtupu
 
Soma taratibu kijana usikimbilie keyboard.
Tazama kati ya maRais 6 wangapi wametokea Mambo ya Nje ?.Kama si kundi la Lowassa ndani ya CCM Membe angekuwa Rais.Magu Dodo lilimdondokea.
Hamna kitu cha namna hiyo tuombe uzima acheni kukariri watanzania
 
May be ... may be not.

Kwanini Makamba anawaweka roho juu sana? kwamba ndie kijana potential kwa wakati huu zaidi ya wengine wote? if yes, why?

Kwanini msijiulize Dotto Biteko ndie anaandaliwa kwa nafasi hiyo baada ya kupewa cheo kikubwa zaidi ya Makamba?

Makamba zaidi ya hilo jina, hebu niambieni, ana record gani nzuri kwenye utendaji, hasa wizara alizowahi kupita ili nione kama kweli anastahili hiyo nafasi?

Naona wengi wenu mmeleweshwa na hilo jina, lakini mlengwa ni mtupu, asiye na utendaji wowote, mwenye maneno mengi, na mpenda sifa binafsi.
 
Tutakuwa nchi ya ajabu sana kuwa na watu ma-failure na wenye elimu duni na yenye utata kuongoza akili kubwa.
Msoga akiendekezwa hii nchi tutaendelea kuvuna MABUA!
Kwanza hii ni dharau sana kwetu wa Tanzania. Hebu sisi tuinuke tukatae watu akama hawa kwa maslahi mapana ya Nchi yetu. Kama anamtaka yeye akamtafutie nchi nyingine! Na haya yote ni kwa ajili ya maslahi yao na ubinafsi wa kiwango cha lami.
 
Back
Top Bottom