Mabadiliko haya ya katiba ya ccm ni kunyimana demokrasia

mchongameno

Member
Feb 9, 2012
26
16
Kutokana na mikakati mipya ya kuleta Maendeleo yenye Tija Ndani ya Chama, Chama cha Mapinduzi kimeamua kutengeneza Katiba mpya yenye Mtazamo mpya tofauti na ile ya awali iliyotengenezwa mwaka 1977. Katiba hii ya sasa ni sehemu ya maandalizi ya Chaguzi kuu zinazotarajiwa kuanza siku kadhaa zijazo pamoja na Uchaguzi mkuu wa chama. Pia katiba hii mpya ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa Chama wa Kujivua Gamba kama inavyoelezwa. Ukiangalia kwa undani zaidi kulikuwa na sababu kadhaa za kufanyika kwa mabadiliko ndani ya Chama lakini pamoja na mpango huo pia kulikuwa na sababu ya msingi ya kuangalia ni lipi linalostahili kufanyiwa mabadilko na lipi lisilostahili ambalo linaweza kuleta Mtazamo hasi kwa Wanachama.
Tukianza na suala la Wajumbe wa Halmashauri kuu ya chama NEC kutoka Wilayani badala ya Mikoani kama ilivyozoeleka hili si wazo baya lakini ni dhahiri litawanyima Wajumbe wa Mkoa Haki ya Kidemokraia katika kufanya maamuzi mazito ya chama. Sababu inayotolewa kuwa ni kujenga ukaribu kati ya Chama na Wanachama walio Chini kabisa haina tija kwani hata mwanzo Chama bado kilikuwa karibu na watendaji wote kutoka Ngazi ya chini mpaka ngazi ya Juu.
Suala la Pili ni hili la Wabunge na Wawakilishi wa Kutokuingia moja kwa moja ndani ya NEC badala yake kuwa na nafasi 15 tu ni dhahiri linaweza kuleta mtazamo hasi unaoweza kupelekea mmong'onyoko wa Chama. Hili huenda limesababishwa na mtazamo kuwa kuna baadhi ya Wanaotaka kugombea nafasi ya Urais kuwa karibu na Wabunge hivyo kutishia uwezekano wa wao kuwa na nafasi kubwa ya kushinda azma zao za kuwania Urais kwa kutumia hila za kisiasa. Kama hii ndio sababu, bado naamini hao wanaotishia kugombea Urais kwa kutumia Wabunge wanayo nafasi hata ya kutumia hao wajumbe kutoka Wilayani wakatimiza azma zao. Labda tujiulize Swali. Hivi Utawala huu tulio nao ndani ya CCM haukuahi kutumia hila zozote wakati wanafanya mkakati wa kuingia Madarakani? Kama ni kweli hawakufanya hivyo. Hawa wanaojiita Wanamtandao ni kina nani?
Suala la Mwisho ambalo ni la hatari zaidi ni kitendo cha kuwanyima wakongwe wa Chama nafasi ya kuingia ndani ya NEC na badala yake kuwa Washauri tu ndani ya Chama kinaweza pia kuleta mtazamo hasi kutoka kwa Wakuu hao wa chama kunakoweza kusababisha Mtafaruku ndani ya Chama.
Hivi ni kweli mabadiliko haya ya KAIBA yalikuwa shirikishi kwa watu wote ndani ya Chama na ni maamuzi yanayokubalika na Wadau wote nadni ya Chama bila Kinyongo?

MWISHO
 
Wana ccm mpo wapi kutetea hoja au kuipinga? Tunawasubiri kwa hamu kusikia maoni yenu juu ya jambo hili maana inasemekana maamuzi haya yanalenga mchakato wa kumpata mgombea urais 2015.
 
si kuinyima democrasia bali itapanua uwakilishi wa hadi ngazi ya wilaya kwenye chombo cha juu cha maamuzi.mfumo uliopo sasa kwa kiasi kikubwa uliwaweka mbali wajumbe wa halmashauri kuu na wanachama.wengi wao waligombea nafasi hizo kwa manufaa yao binafsi
 
Back
Top Bottom