Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

CRITO

Member
Aug 30, 2012
58
58
SAM_5169.JPG


  1. Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri Emmanuel Nchimbi,IGP Mwema,Paul Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa FFU,na RPC IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na au wafukuzwe kazi
  2. RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka
  3. Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya kisiasa.1.ARUSHA vifo 3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU MASHARIKI,vifo 5, 4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
  4. chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.
  5. Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli tata anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.
  6. TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli na haki,kuisusia TBC
  7. Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya hadhara ni lazima kwa mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni,pia kupata habari na taarifa
  8. Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)
  9. Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa mwanza Umevunjwa.


Imesomwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa
Kutoka mjengwablog
 
Well done kamati kuu kwa kutoa msimamo huu ambao tuliutegemea.
Huyu dogo Adam Chagulani nilishajua siku zake ndani ya Chadema zinahesabika, hatimaye yametimia.
Kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha Jijin la Mwanza linapata viongozi mahiri watakaoweza kwenda na kasi mpya ya mahitaji ya kisiasa kwa sasa.
 
Timely justice for all! Hapo kwenye kuisusia TBC mimi nilishaanza tangu aondoke Tido.
Kuhusu Tendwa Ukurasa wa 107 wa Kitabu cha Mwalimu Mkuu wa Watu kuna maneno haya "Mabadiliko yana tabia yake. Yakiamua kuja, huja. Huwa hakuna mjadala wala mbadala.Ni mwenye busara tu ndiye huyapokea mabadiliko kwa amani"
Mwandishi anaendelea ..."Nyakati za kukosoa utawala mbovu ukaitwa mchochezi zimepita. Nyakati za kuomba kura kwa wananchi kwa kuwapigia zumari, gitaa au kunengua viuno kwa taarabu zimepita. Nyakati za kumwona mtu mwenye mawazo ya kisiasa tofauti na wewe kuwa ni adui wa nchi au ni hatari kwa usalama wa Taifa zimepita"
 
Safi!!!!!!!! sana kamati kuu kwa maamuzi mazito.Nawapongeza kwa kuwavua uanachama viongozi ambao ni wasaliti.Bora kutokuwa na kiongozi kuliko kuwa na viongozi wenye majungu,fitina,kigeugeu na kila aina ya uchafu.Sasa vijana wa kitangili na Igoma tujipange kwa ajili ya uchaguzi mdogo wa udiwani.
 
Well done kamati kuu kwa kutoa msimamo huu ambao tuliutegemea.
Huyu dogo Adam Chagulani nilishajua siku zake ndani ya Chadema zinahesabika, hatimaye yametimia.
Kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha Jijin la Mwanza linapata viongozi mahiri watakaoweza kwenda na kasi mpya ya mahitaji ya kisiasa kwa sasa.


Lakini katika kura zilizopigwa(za kutokua na imani na meya) kati ya ishilini ni kura nane tu ndizo alizopata, inamaana wote ni kwa sababu ya Chagulani.
 
Haya ni maamuzi magumu ambayo yananifanya niwafurahie sana CDM. Wanatoa maamuzi kwa wakati. Naomba pia wangefanya harambee/au kuitisha michango kwa ajili ya familia ya Marehemu Mwangosi.
 
Hii ni nzuri kwa kuimarisha chama na kujenga dhana nzima ya uwajibikaji. Kuvumiliana kwa CCM ndo kumetuvikisha hapa. We need a new start, we need Chadema to take over.
 
CHADEMA, unafiki mwiko yaani sio kama CCM hafagiliwi mtu na watu wameupoteza udiwani.... hongereni sana makamanda mnajenga taifa lenye viongozi wasio wanafiki na wenye kujiamini
 
1.Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.....
2............maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka
3.Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata .....
4.Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa.....
5.TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,...
6.Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe....
......
1,2,3,4 safi
5, haswa, tena hii tv na redio ni adui mkubwa sana na anabidi kuogopwa.
6 ni kweli na kama wakikataa hayo basi hata siasa yenyewe hawaiwezi, maandamano ni sehemu ya wengi kusema yaliyo moyoni mwao, na hata hivyo katiba inaruhusu hivyo.
7 :israel:
:peace:
8 no comment
 
Labda ueleweshwe maana ya kususa! TBC huijui?

Kususiwa kutasababisha yafuatayo kutokea;
  1. Kibiashara TBC itaathirika kwa kupungua mapato yatokanayo na matangazo ya kibiashara
  2. image ya TBC itashika kwani hakuna wafanya biashara watakakubali kufanya biashara na tbc
  3. kupungua kwa watazamaji
Mambo haya ya kususia unaweza kuyaona madodgo lakini kwa taasisi yanaathari kubwa sana
 
Habari nzuri sana hii hasa hapo kwa TBCCM yaani wangesema kabisa iwe marufuku kwa tbccm kurusha habari za cdm!
 
The same old story.

Ninawaasa wananchi masikini kutokuwa mbele kwenye hayo maandamano ili na wao viongozi wapeleke misiba kwenye nyumba zao. Iweje wajiite wapigania ukombozi lakini wanaouwawa na kujeruhiwa ni masikini tu na sio wao viongozi?
 
Back
Top Bottom