Maazimio ya Kamati Kuu ya CHADEMA Sept 10, 2012

Kamanda TBC hakuna jipya wamezoea kuficha maovu ya serikali
 
Hivi TBC1 inaendeshwa kwa kodi ya watz au kwa michango ya chama cha siasa. Imekaa tenge kiasi ambacho uwezi amini kama ni taasisi ya umma au ya chama!
 
Hivi Chadema wanaisusiaje TBC sasa kwa mfano? Kinacholeta mantiki kwangu ni TBC kuisusia Chadema kwa kutotangaza habari zake na siyo kinyume chake.
 
MAAZIMIO YA KAMATI KUU YA CHADEMA leo,
1.Uwajibikaji wa kisiasa wa viongozi wa serikali na idara zake.,Waziri Emmanuel Nchimbi,IGP Mwema,Paul Chagonja,RPC Morogoro na Kamanda wa FFU,na RPC IRINGA na Kamanda wa FFU wajiuzulu na au wafukuzwe kazi

2.RPC Morogoro na Iringa,makamanda wa FFU Morogoro na Iringa,na maaskari waliouwa wakamatwe mara moja na kufunguliwa mashitaka

3.Rais aunde tume huru ya uchunguzi wa vifo tata katika matukio ya kisiasa.1.ARUSHA vifo 3.IGUNGA,vifo vingi havijulikani bado,3.ARUMERU MASHARIKI,vifo 5, 4.SINGIDA kifo 1, MOROGORO na IRINGA
chadema haitatambua wala kushirikiana na kamati batili ya NCHIMBI.

4.Msajili wa vyama vya siasa John Tendwa ni mtu hatari kwa taifa kwa kauli tata anazozitoa.anashirikiana na au anajipendekeza kwa CCM na Serikali yake.CHADEMA tangu sasa haitafanya kazi na Tendwa wala kufanya mawasiliano naye ya kiofisi.Labda kama atagundua makosa yake na kuomba msamaha,chadema itatafakari namna ya kufanya naye kazi tena.

5.TBC TAIFA Television na Redio ni hatari kwa taifa,kwa kubobea kupotosha umma juu ya matukio mengi.Hivyo CHADEMA Inatangaza mgogoro na TBC na inaelekeza na kuomba wanachama ,wapenzi,na wananchi wote wapendao ukweli na haki,kuisusia TBC

6.Jeshi la Polisi lijue kuwa Maandamano ndiyo siasa yenyewe na mikutano ya hadhara ni lazima kwa mawasiliano ya umma na siasa.kuzuia vitu hivyo ni kunyima wananchi haki yao ya kikatiba ya uhuru wa kukusanyika na kutoa maoni,pia kupata habari na taarifa

7.Operesheni MOVEMENT FOR CHANGE M4C,Inaendelea kadiri ya ratiba ilivyopangwa katika utaratibu uleule uliokuwepo awali.Inarejea Iringa Siku si nyingi.Na kamati kuu Imetoa msisitizo MAALUM kwa jimbo mojawapo singida,ambapo wamesema watatumia helcopita,magari,pikipiki na baiskeli na miguu,na badala ya kupita vijijini kama majimbo mengine,Chadema wanasema kwa sababu maalum katika jimbo hilo watapita kitongojikwa kitongoji,ili kufunza adabu baadhi ya viongozi (msisitizo ni wa msoma MAAZIMIO.jimbo hili laweza kuwa la Mwigullu Mchemba,kadiri ya wanahabari waliokuwepo)

8.Kutokana na mgogoro wa muda mrefu mkoani mwanza uliosababisha meye wa chadema kuvuliwa umeya kinyume na utaratibu na kwa njama za CCM na Serikali,na bahati mbaya sana kwa kushirikisha madiwani wa CHADEMA,KAMATI KUU imewavua UANACHAMA madiwani wake wawli 1 ADAMU CHAGULANI wa kata ya IGOMA na HENRY MATATA wa KITANGIRI, PIA uongozi wote wa CHADEMA mkoa wa mwanza Umevunjwa.

Imesomwa na Mwenyekiti CHADEMA Taifa
 
CRITO
Hivi Kamati ya CDM imedesa maazimio yake kutoka JF au wanajf ndo wamedesa CDM?
 
Last edited by a moderator:
KUWAFUTIA UANACHAMA KINA ADAMS CHAGULANI NI UCHEMKAJI. CDM mnajichafua mwana, Meya alikuwa ni kokoto!
 
CHADEMA hapa ndio napo wasifu kwakuchukua maamuzi magumu hawaangalii kuwa wewe ni kiongozi au la kama ufanisi wako upo chini unafukuzwa CCM wangekuwa wanaweza kufanya na yanayo fanywa na CDM wangekaa kwenye madaraka milele
 
Hiyo TBC wangeifanya ya kulipia sidhani kama kuna mtu angeinunua. S/times tuifungua tu coz tunaikuta kwenya package. R.I.P TBC
 
Mie naangaliaga TBC alhamisi kwa sababu ya Ze komedi kopi na kupest zaidi ya hapo hata wakiifunga kabisa poa tu.

Naona wewe hujasusa! Inabidi ususie kila kitu.Mi hata kingamuzi cha startimes naenda kufugia mende kwa sababu wako associated naTBC,naamia zangu ZUKU.
 
Well done kamati kuu kwa kutoa msimamo huu ambao tuliutegemea.
Huyu dogo Adam Chagulani nilishajua siku zake ndani ya Chadema zinahesabika, hatimaye yametimia.
Kazi kubwa iliyopo ni kuhakikisha Jijin la Mwanza linapata viongozi mahiri watakaoweza kwenda na kasi mpya ya mahitaji ya kisiasa kwa sasa.

Mimi huwa naamini maamuzi ya kamati kuu ya Chadema yako very objective. Huyu jamaa alianzisha harakati za kumwondoa mmeya wa chama chake bila kufuata taratibu za chama. Mwisho wa uhuni ndo huu. Mimi napenda ujasiri wa Chadema.
 
KUWAFUTIA UANACHAMA KINA ADAMS CHAGULANI NI UCHEMKAJI. CDM mnajichafua mwana, Meya alikuwa ni kokoto!
Mkuu tunaweza tukaona kama MEYA alikuwa Mchafu kumbe alikuwa anasababishiwa na Kina ADAMU CHANGULA hebu jaribu kufikiria ile Issue ya Maliasili na Maige ya kusafirisha Twiga kumbe yeye alikuwa anapokea order tuu
 
Hapa ktk kampuni yetu ngoja niicancel ktk vituo ambavyo nlipendekeza kuipa matangazo
 
Back
Top Bottom