1. Kwa hiyo, unataka tuamini Mkristo akipasi ina maana Mwislamu kadhulumiwa na akifeli ni haki yake na pia unataka tuamini Mwislamu akipasi ni haki yake na akifeli kadhulumiwa?
2. Sisi wengine ambao tumekaa sehemu za mwambao na baadhi ya mikoa ya Tanzania na tuna marafiki sehemu hizo 'experience' yetu ni kwamba Waislamu wanaamini elimu ya maana ni elimu ya dini na elimu dunia ni ya makafir. After all, haikuwahi kupewa kipaumbele na Waarabu waliotawala sehemu hizo. Na mara nyingi unasikia Waislamu wakisema: "Wakristo kwa elimu dunia wanajitahidi kweli lakini elimu ya dini hawana kabisa. Hii wawaachie Waislamu." Tembelea hiyo mikoa na uone kama kweli mwamko wa watu kielimu unapingana na takwimu zilizotolewa. Mtaa nikakokaa - utaona watoto wenye majina ya Ali, Salumu, Halima wakishatoka madrassa wanacheza mpira au michezo yao hadi wakati wa kwenda kulala usiku wakati wenye majina ya John, Maria, Titus wazazi wao wanawalazimisha kwenda tuition na wakitoka huko wanakalishwa chini kufanya homework. Obviously, matokeo ya darasani ya watoto kama hawa ni tofauti sana. Kwa upande mwingine, wazazi Waislamu ambao wako serious na elimu watoto wao wana'perform' vizuri. Nina family friends (couple) ambao mtoto wao walimpeleka shule ya mission (English Medium School ya Wakatoliki) na muda wote ambao amesoma hapo alikuwa akishika namba 1 (na maksi zake hakupewa Mkristo) na kwa bahati nzuri shule inaruhusu watoto wavae mavazi kulingana na jinsi wazazi wao wanavyowalea kiimani (wenye hijabu au kofia wanavaa pia) ila uniform yao ni moja ili kutoa utambulisho kuwa ni watoto wa shule fulani.
3. Mimi nimetembelea Wilaya ya Mkuranga na pia nawasiliana na baadhi ya walimu wanasema watu hawana mwamko kabisa wa elimu dunia bali elimu ya dini na ngoma za asili. Watoto wanasoma "kilele mama" na walimu wakiwakanya wazazi wao wanakuja juu.
4. Wakristo wao, elimu ya dini ni nzuri na elimu dunia ni nzuri pia maana havipingani provided elimu zote zinamfanya mwandamu ajitambue zaidi yeye ni nani na atoe mchango gani katika kuboresha maisha yake na ya wenzake na pia apate stahili mbele ya Mwenyezi Mungu. Kwa Wakristo in fact wazazi wanamkazania mtoto apate elimu dunia kwanza maana elimu ya dini ipo wakati wote.
5. Kwa hiyo, tafsiri ya hizo takwimu (kama zilivyoletwa humu) si tafsiri ya kuonesha nani kadhulumiwa na nani kadhulumu bali ni nani anachangamkia fursa na nani bado hana mwamko huo.
6. Nawapongeza baadhi ya viongozi wa Waislamu wanaowashauri waumini wapeleke watoto wao shule kuliko kulalamika tu. Maana wanajua suluhisho liko katika elimu hii ambayo baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu wanaiita "elimu dunia" ambayo kwao si muhimu sana. Hata baadhi ya viongozi tu wanasema hivyo. "Elimu bora zaidi ni elimu ya dini. Hii nyingine waachieni makafir maana wao hawana dini." Sasa mtu akihubiri hivi halafu wafuasi wake wakifuata anachokihubiri na kuwaletea tatizo la kielimu alaumiwe yule mwingine ambaye anachangamkia fursa?
7. Ndiyo maana mimi huwa naona kama baadhi ya haya malalamiko yanatokana na kujiona kundi moja liko nyuma na kundi jingine mbele (kielimu na kiajira) na sasa badala ya kutafuta chanzo cha tatizo hitimisho linakuwa "lile kundi jingine linatudhulumu".
8. Hata kama kulibadilishwa majina na kutumia namba idadi ya Waislamu baadaye ilikuwa juu (kwani utafiti gani ulionesha ilikuwa juu kwa vile kule kudhulumiwa kulikwisha) na je kwa nini pamoja na kutumia namba bado kuna malalamiko? Pili, walimu wanasahihisha (nasikia) kila mwalimu mmoja swali moja na wako mchanganyiko na siyo kwamba ni wa dini moja na kwa vile ni namba tu zinazoonekana nani anakuwa anaweza kuona huyu ni Mwislamu apewe alama ndogo na huyu ni Mkristo apewe namba kubwa? Mbona wanafunzi Waislamu wanaofanya vizuri wanaendelea kufanya vizuri tu? Jamani tubadilike!
Unajua kina kitu kina shangaza sijui huelewi au unafanya kusudi.
Umepewa takwimu na mifano yakutosha kwamfano:
1. Nime kwambia baada ya Prof Malima kubadili taratibu na kutumia namba kutoa matokeo ya darasa la saba waislam kwaasilimia arubaini waliongezea, hii haikuwa bahati mbaya.
2. Nimekupa mfano wa matokeo ya Form six ya waislam yalio katwa hivi karibu jamaa wakadai ilikuwa computer lkn baada ya kufanya marekebisho yule alie kuwa kapata "D" kabla ya marekebisho akapewa "c" na aliekuwa na "E" akapewa "B" sasa huoni kama jamaa wamekaa ndani tu na kupika matokeo.
3. Bro Mohamed Said amekupa data za kufungwa seminary za kiislam, Nyerere alifanya hilo makusudi.
4.Nyerere alivunja umoja wa waislam uliokuwa namanufaa akaweka BAKWATA na kuweka vibaraka ili kuwaumiza waislam.
SASA WALETA HOJA KUWA WAISLAM HAWAPENDI KUSOMA MBONA KILA KUKIFANYIKA MABADILIKO MATOKEO NAYO YANABADILIKA?