Maandamano ya CHADEMA ni jitihada zisizo na majibu

MDAU TZ

Member
Jun 9, 2023
8
40
WAKATI niliposikia tangazo la maandamano lililotolewa na uongozi wa CHADEMA,Binafsi nilipata tumaini kuwa sasa ni ule muda uliosubiriwa na Watanzania kwa ajili ya kusimama,kupigana na kutetea haki zao za msingi kwa kupaza sauti kwa viongozi wao na kuwakumbusha juu ya wajibu na majukumu walionayo.

Na kupata nguvu kwamba bado kuna watu nyuma ya watu wanyonge wasio na sauti wenye uwezo wa kusimama na kuwatia nguvu ya kupambana kwa kuwahamasisha na kuwaongoza kufikia njia ya haki qambayo itawasaidia kuwaokoa kutoka kwenye matatixo walionayo.

Pia nikahisi sasa ni wakati wa kumfunga paka kengere,paka ambaye ameingia kwenye dali lililo na chakula,kilichokuwa wanakitegemea,akajimilikisha kwa madaraka na nguvu alizonazo ka kuwasahau wenginene kuwa nauhitaji wa chakula hicho.

Paka ambaye hasikii kelele zao,hahisi maumivu ,wala haoni machozi yao ,paka anaejali watu wenye nguvu na uwezo tu,wakati wao wakisema gharama za mtandao ziko juu,mbona nauli zinapanda mara mbilimbili,kwanini sukari inauzwa elfu nne miatano kwa kilo,wakati zanzibar ni elfu moja na miatisa,kwnani umeme unakata kata,wakati mvua zinanyesha kila kukicha mpaka mafuriko,paka kimya

Lakini wenye nguvu wakisimama na kusema hawawataki wamachinga kwasababu hawalipi kodi,asubuhi mgambo wako barabarani,wakipaza sauti,sasa nauli ziongezeke kwasababu mafuta na gharama za uendeshaji uko juu,LATRA vikao vya usiku,na nauli zinapanda.

KUVUNJIKA KWA MATUMAINI

Hakuna hata punje la tumaini kuwa maandamano yangewapatia suluhu,na kuwa msaada kwa kero na maswali yote waliokuwa nayo licha ya kuwa tambo na hamasa walizokuwa nazo wananchi ya kuwa sasa wangeweza kumfunga paka kengere.

Kuvunjika kwa tumaini kunatokana na udhaifu wa ajenda,uelekezwaji wa ajenda zenyewe na namna ya uhamasishaji haukubeba uhalisia wa hisia,maumivu na machozi ya wahusika,baadala yake umehusisha kwa kiwango kikubwa masilahi binafsi ya kisiasa na kiutawala kwa kupitia mgongo wa wananchi.

AJENDA DHAIFU

Kuomba kuondolewa kwa misuada ya sheria za uchaguzi bungeni ni ajenda muhimu lakini isiyo na nguvu,haikugusi hisia za watu wengi,haileti matokeo chanya na kwa haraka,na wala sio njia ya uhakika ya kutatua kero za watu amabazo kiuhalisia ndio chanzo cha maumu.

Ni ajenda ambayo imejaa ubinafsi wa kiutawala na nguvu ya kisiasa na sio kubeba nguvu ya kiutetezi na kutafutwa kwa suluhisho kwa matatizo yanayowakabili jamii.

Kupanda kwa gharama za maisha,pia ni hoja muhimu lakini imepaziwa sauti wakati na sehemu isiosahihi,kwasbabu gharama za maisha na vichocheo vyake vilianza muda mrefu na wakati huo ndio ulikuwa wakati sahihi wa kupaza sauti,mfano wakati wa kuanzishwa kwa tozo,makato ya kodi ya pango,kupata kwa nauli,na mengineyo,huu ndio ndio ulikuwa muda sahihi wa kuandamana ili kupinga hivi vichocheo ya hari ngumu ya maisha kama kweli kulikuwa na nia thabiti.

UWELEKEZAJI WAKE, SIO SAHIHI

Kitendo cha Mandamano kuishia Umoja wa mataifa ni ishara ya udhaifu wa viongozi wa kutojua nini tunachokitaka,na wapi tunaweza kupeleka malalamiko yetu na kuweza kufanyiwa kazi kwa haraka,na kwa lengo husika juu ya makusidio ya mandamano husika.

Mara nyingi lengo la maandamano ni kufikisha malalamiko,kero au ombi lenye kusudi la kupatiwa majawabu au Suluhu kwa wakati,na pia husaidia kusikilizwa kwa haraka na wahusika wanaofikishiwa kero hiyo,hivyo Umoja wa mataifa haikuwa sehemu husika ya kwenda kupeleka malalamiko kwasababu masuala tunayolalamikia ni masuala ya mambo ya ndani ya nchi,

Hata hivyo maandamano yalipaswa yaelekezwe aiza kenye ofisi za bunge kwa ajenda za Misuada ya sheria ya uchaguzi,wao ndio wangekuwa na majibu sahihi kwasababu ndio wanahusika na utungaji na upitishaji wa misuada hiyo.

Au Yangelekezwa kwa ofisi ya waziri mkuu au Raisi ambao ndio viongozi wakuu wa serikali,na Nchi, na ndio watendaji wakuu,na wenye mamlaka ya kutoa na kuondoa matamko,kutoa amri,kuzuia au kuruhusu mambo yote yanayotokea ama kufanyika katika nchi,wao pekee ndio wangeweza kutoa majibu ya yale yanayolalamikiwa katika maandamano.

WATANZANIA TUJIPANGE UPYA, shughuli bodo mbichi|
 
Attachments

  • chadema 2.jpg
    chadema 2.jpg
    34.4 KB · Views: 3
Mkuu muda upo wa kutosha, unaweza kuitisha maandamano na kuweka hizo hoja zako zote uzitakazo na kuziwasilisha sehemu husika. Nyie ndio mlikuwa na nongwa cdm kutaka kuandamana, saa hii cdm wamefanikiwa kuandamana mnakuja na tathmini uchwara.
 
Kwa kuanzia UN ni hatua ya kimkakati tu kwa kuanzis maana wangeelekea Bunge au ofisi za serikali wasingepata kibali na wangepigwa tu. it was strategic. kuhusu hoja zao wacha tuone reaction ya serikali. ni mapema kufanya judgement.
 
WAKATI niliposikia tangazo la maandamano lililotolewa na uongozi wa CHADEMA,Binafsi nilipata tumaini kuwa sasa ni ule muda uliosubiriwa na Watanzania kwa ajili ya kusimama,kupigana na kutetea haki zao za msingi kwa kupaza sauti kwa viongozi wao na kuwakumbusha juu ya wajibu na majukumu walionayo.

Na kupata nguvu kwamba bado kuna watu nyuma ya watu wanyonge wasio na sauti wenye uwezo wa kusimama na kuwatia nguvu ya kupambana kwa kuwahamasisha na kuwaongoza kufikia njia ya haki qambayo itawasaidia kuwaokoa kutoka kwenye matatixo walionayo.

Pia nikahisi sasa ni wakati wa kumfunga paka kengere,paka ambaye ameingia kwenye dali lililo na chakula,kilichokuwa wanakitegemea,akajimilikisha kwa madaraka na nguvu alizonazo ka kuwasahau wenginene kuwa nauhitaji wa chakula hicho.

Paka ambaye hasikii kelele zao,hahisi maumivu ,wala haoni machozi yao ,paka anaejali watu wenye nguvu na uwezo tu,wakati wao wakisema gharama za mtandao ziko juu,mbona nauli zinapanda mara mbilimbili,kwanini sukari inauzwa elfu nne miatano kwa kilo,wakati zanzibar ni elfu moja na miatisa,kwnani umeme unakata kata,wakati mvua zinanyesha kila kukicha mpaka mafuriko,paka kimya

Lakini wenye nguvu wakisimama na kusema hawawataki wamachinga kwasababu hawalipi kodi,asubuhi mgambo wako barabarani,wakipaza sauti,sasa nauli ziongezeke kwasababu mafuta na gharama za uendeshaji uko juu,LATRA vikao vya usiku,na nauli zinapanda.

KUVUNJIKA KWA MATUMAINI

Hakuna hata punje la tumaini kuwa maandamano yangewapatia suluhu,na kuwa msaada kwa kero na maswali yote waliokuwa nayo licha ya kuwa tambo na hamasa walizokuwa nazo wananchi ya kuwa sasa wangeweza kumfunga paka kengere.

Kuvunjika kwa tumaini kunatokana na udhaifu wa ajenda,uelekezwaji wa ajenda zenyewe na namna ya uhamasishaji haukubeba uhalisia wa hisia,maumivu na machozi ya wahusika,baadala yake umehusisha kwa kiwango kikubwa masilahi binafsi ya kisiasa na kiutawala kwa kupitia mgongo wa wananchi.

AJENDA DHAIFU

Kuomba kuondolewa kwa misuada ya sheria za uchaguzi bungeni ni ajenda muhimu lakini isiyo na nguvu,haikugusi hisia za watu wengi,haileti matokeo chanya na kwa haraka,na wala sio njia ya uhakika ya kutatua kero za watu amabazo kiuhalisia ndio chanzo cha maumu.

Ni ajenda ambayo imejaa ubinafsi wa kiutawala na nguvu ya kisiasa na sio kubeba nguvu ya kiutetezi na kutafutwa kwa suluhisho kwa matatizo yanayowakabili jamii.

Kupanda kwa gharama za maisha,pia ni hoja muhimu lakini imepaziwa sauti wakati na sehemu isiosahihi,kwasbabu gharama za maisha na vichocheo vyake vilianza muda mrefu na wakati huo ndio ulikuwa wakati sahihi wa kupaza sauti,mfano wakati wa kuanzishwa kwa tozo,makato ya kodi ya pango,kupata kwa nauli,na mengineyo,huu ndio ndio ulikuwa muda sahihi wa kuandamana ili kupinga hivi vichocheo ya hari ngumu ya maisha kama kweli kulikuwa na nia thabiti.

UWELEKEZAJI WAKE, SIO SAHIHI

Kitendo cha Mandamano kuishia Umoja wa mataifa ni ishara ya udhaifu wa viongozi wa kutojua nini tunachokitaka,na wapi tunaweza kupeleka malalamiko yetu na kuweza kufanyiwa kazi kwa haraka,na kwa lengo husika juu ya makusidio ya mandamano husika.

Mara nyingi lengo la maandamano ni kufikisha malalamiko,kero au ombi lenye kusudi la kupatiwa majawabu au Suluhu kwa wakati,na pia husaidia kusikilizwa kwa haraka na wahusika wanaofikishiwa kero hiyo,hivyo Umoja wa mataifa haikuwa sehemu husika ya kwenda kupeleka malalamiko kwasababu masuala tunayolalamikia ni masuala ya mambo ya ndani ya nchi,

Hata hivyo maandamano yalipaswa yaelekezwe aiza kenye ofisi za bunge kwa ajenda za Misuada ya sheria ya uchaguzi,wao ndio wangekuwa na majibu sahihi kwasababu ndio wanahusika na utungaji na upitishaji wa misuada hiyo.

Au Yangelekezwa kwa ofisi ya waziri mkuu au Raisi ambao ndio viongozi wakuu wa serikali,na Nchi, na ndio watendaji wakuu,na wenye mamlaka ya kutoa na kuondoa matamko,kutoa amri,kuzuia au kuruhusu mambo yote yanayotokea ama kufanyika katika nchi,wao pekee ndio wangeweza kutoa majibu ya yale yanayolalamikiwa katika maandamano.

WATANZANIA TUJIPANGE UPYA, shughuli bodo mbichi|
Uchambuzi wa mbuzi mfia kijani.... huu ni uchambuzi wa kimakalio makalio
 
Jua kwanza aina za maandamano:-
  • Kuna maandamano ya kimapinduzi (hufanyika bila kibali)
  • Maandamano ya kueleza jamii/mamlaka nini mnataka kiwe/mfanyiwe (hufanyika kwa kibali)
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom