Maandamano ya Aprili 26, 2018: Yanayojiri kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi

Status
Not open for further replies.
Huyo kiongozi wa chama cha ujiji alishapoteza mwelekeo siku nyingi!unazijua tabia za mnyama anayeitwa Pimbi ?
Haha, unakikumbusha gazeti la zamani la Sani. Kulikuwa na cartoon ina jina la Pimbi.
upload_2017-5-25_14-6-13.gif
 
Tanzania tunahitaji jamii iliyojengwa katika misingi ya kupendana. Yaani kuanzia kiongozi wa juu mpaka wa chini tofauti na sasa kuwa vingoz wetu wanachojua nakuamini ni kuwa wao ndo wanaofanya tanzania yetu isimame!
Nawakumbusha Kuwa MUMGU WETU ANAPENDA WATU WOTE ndiyo maana anataka uthaminiana.
TATIZO KUBWA NI KUIJENGA HIYO MISINGI. NA HUENDA LIKAWA NI FUMBO LA MAUTI. KILA SIKU HUWA NAJIULIZA WAPI TULIKOSEA. TUNAWEZA TUKAWA TUNAPIGA KELELE KILA SIKU BILA KUJUA NINI CHANZO. KUMBE CHANZO NI MFUMO TULIO NAO. NCHI AMBAYO HAINA POLICY. KILA KIONGOZI AKIINGIA ANAKUJA NA YAKE YA MIAKA 5
 
Dah me naamini kabisa mange ameshinda embu tujiulize serikali imetumia pesa kiasi gani kukabiliana nakauli yamange yamaandamano alafu turudi kwamange tuone katumia bando labei gani kushawishi watu waandamane
 
Prof,mange kimambi umeshinda Vita,wao wametumia bunduki na vifaru wewe ametumia kalamu,umewaumiza sana sema wanakaza tu,lkn kipigo ulichowapa ni kipigo kitakatifu utabaki kwenye historia ya taifa letu kama Nyerere na kina mandela
Profesa wa chama cha demokrasia ya matusi mitandaoni! mijitu mizima mlikatanguliza hako kajitu! midume mioga ilikua nyuma iliogopa kukaa mstari wa mbele!mamake....Leo mngepokea kipigo cha mbwa koko!
 
Mbona kaweza kuwaandamanisha polisi Tanzania nzima. She deserves PhD, kushinda ya bichwa.
Naona leo gari la wazi limeonekana ni old fashion. Mkuu ameogopa nini?

Yule dada amanifunza kitu. Yaani yupo Amerika tena pekee yake na alikuwa anahamasisha maandamano kupitia mitandaoni ila ameweza kuitikisa serikali nzima, kuanzia top kabisa, mawaziri, wakuu wa mikoa, makamanda wa polisi mikoa, wakuu wa wilaya na kila mteule akawa anaimba juu ya maandamano mwisho wa siku wakaja kutumia kodi zetu kuwaandamanisha polisi kwa siku tatu.

Bila shaka serikali imejifunza kitu na itoe pamba masikioni ifanyie kazi kero za wananchi.

Muhamasishaji wa maandamano amefanikiwa kwa asilimia 90.
 
Narudia kukuambia ficha upumbavu wako
Serikali imsikilize anaye t

Watu kama wewe ndio mnamfanya Magufuli apotoke kwa umbumbumbu wenu!! Serikali ni mtumishi wa wote hata wendawazimu kama wewe hivyo ni lazima iwe sikivu!! Bila kutumia busara serikali itajikuta inatumia rasilimali za maendeleo kwa mambo ya kipuuzi kama kutumia vyombo vya ulinzi kufukuzana na wauza chips!!
 
Tatizo lako unachanganya mambo mengi ambayo hayana hata mantiki katika msingi wa hoja.

Kwa kukusaidia ili uelimike zaidi, Nchi inaitwa masikini kwa sababu wananchi wengi ni masikini na inaitwa tajiri kwa sababu wananchi wake wengi ni tajiri.

Rais alichaguliwa na wananchi wengi waliojitokeza kupiga kura. Suala sio waliojiandikisha kupiga kura bali waliojitokeza kupiga kura. Huu ni utaratibu wa kisheria uliowekwa nchini.

Kama hoja ni ujumbe, mbona kila siku wananchi wanatoa ujumbe kwa serikali/wanasiasa kupitia majukwaa mbali mbali.

Familia moja kujikusanya katika Tanzania House halafu unasema hayo ni mafanikio inaonyesha ni jinsi gani ulivyokuwa umeweka malengo katika mzani wa chini sana.

Kimsingi mimi sitoi maoni yangu yawe na majibu kama hesabu 2+2=4, bali natoa maoni yangu kwa utashi wangu bila kujali ww yatakuridhisga ama wengineo. Na sina hakika mpaka kundi liwe kubwa kiasi gani ndio ifahamike kwamba kuna maandamano ya kuwakilisha jambo fulani. Ninachojua ni hoja ya hayo maandamano.

Mfano mrahisi ili uelewe kwamba idadi ya watu sio kipimo pekee cha ujumbe kufika. Nyerere alipoenda UNO kudai uhuru hakwenda na watanzania kwa maelfu, lakini ujumbe wake ulitosha kueleweka na umoja wa mataifa na hatimaye kupatiwa uhuru wetu. Sasa ww subiri kundi kubwa la watu ndio uangalie ujumbe.
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom