macho_mdiliko
JF-Expert Member
- Mar 10, 2008
- 22,107
- 40,238
Ukiendekeza mbwa atakufuata mpaka msikitini. Serikali imechezeshwa ngoma na huyu dada. Kuna watu watakuwa wanafurahi kuwa Mange na kundi lake wameshindwa lakini mimi naona kama aliyepoteza hapa ni serikali and co! Wamepoteza kwa sababu wameonyesha dalili zote za kugwaya kwa mtu ambaye yupo mbali na anatumia vidole tu ku-type. Hebu fikiria upande mmoja yuko mwanamke mmoja tena mwenye mwili mdogo mdogo amejikali kwenye computer/simu ana-type na upande mwingine wamekaa makundi kwa makundi ya maaskari wanaruka ruka na kuzunguka mitaani kama vichaa! Kulikuwa na umuhimu wa kufanya hayo yote isipokuwa ni over-reaction ya vyombo vya usalama? Yaani mpaka yeye nadhani hakuwa anaamini kama anaweza kuwapelekesha namna hii! Na mbaya zaidi amenogewa... anasema sasa hivi anavizia serikali ifanye tukio lolote baya (kwa bahati mbaya au kwa uzembe kwa makusudi) ili akiamshe tena! Huoni hapo ameiweka serikali kwenye mtihani mkubwa? Hii inanikumbusha kuishi sehemu zenye vibaka... Unakuwa umejenga nyumba yako nzuuuuri lakini usiku na mchana huna raha kwa wasiwasi wa kuvamiwa! Tafakari!mkuu, kuna analysis nyingi sana
mange kafuta maandamano yote yajayo pia!!