Maandamano ya Aprili 26, 2018: Yanayojiri kutoka maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi

Status
Not open for further replies.
Yan
IMG-20180426-WA0003.jpg
 
Maandamano ya mapinduzi ya serikali huwa yanatokea siku ambayo polisi hawajajiandaa na wala wananchi hawakujiandaa kuandamana ila wanajikuta wapo barabarani tena chanzo chake huwa kidogo sana.
 
Hahahah!!!nicheke tu maana kulia nataka kucheka nataka sasa nichague kipi?dah ila poa tutafika tu!
 
Leo nilishuhudia police nchi nzima wakiandamana kupinga kuminywa kwa uhuru wa kusema na ukandamizaji wa demokrasia kuitikia wito wa dada mange kimambi alieko marekani

Sasa kuna watu wanasema mbona raia hawakuonekana wamekuwa waoga

Ingekuwa yameandaliwa kisiasa wangesema tunasababisha vurugu tukiandamana tusipoandamana tumeogopa
 
Habari wadau

Mungu wetu ni msingi wa demokrasia. Aliumba wenye nguvu na wanyonge, wajinga na werevu, watawala na watawaliwa. Uhuru wa mihimili ni utashi wa muumba ili amani iwepo. Mungu akikupa nguvu anakunyima hekima ili ushauriwe; akikuumba mfupi, anakupa akili za kutumia warefu wakuchumie maembe. Dunia ya wafupi tu ni taabu. Ya warefu tu ni balaa. Ya wababe tu, mnyonge ndiye kiongozi.

Ukisema sina nafasi au anaogopa kuongea angalau kama si kudai kwa vitendo haki yako, Basi hiyo haki siyo muhimu kwako. Usimlaumu mtu mwingine au kumsingizia mwingine ameshindwa kukutetea.

Hakuna mnyonge, Kuna waliokubali kuwa wanyonge! Huwezi kukaa kusubiri kupewa haki zako unazimamia na kudai ukinyimwa na usisubiri mtu aje adai kwa niaba yako. Si jukumu la mtu mwingine bali ni jukumu lako binafsi! Stand up for your right!!

Huwezi kusema maisha magumu na unasubiri mtu aje aongeae kwa niaba yako, hakuna.

Huwezi kusema ninaonewa, unasubiri mtu aje akutetee. Amua leo kwamba wewe si mnyonge na kama ni haki yako unahitaji.

Tuache kuwa na taifa haiwezekani kila kitu, kinawezekana tukiweka nia ya dhati mabadiliko tunayoyatamani tunaweza kuyapata kwa nguvu zetu wenyewe.. Kila mtu awajipike na achukue hatua iliyo ndani ya uwezo wake.

mr mkiki
Wewe uko kundi gani ?
 
Duh, tuache kujibaraguza. Leo tumeangukia pua aisee.

Ebu niambie una shamba lako unatangaza una mpango wa kulima,unajiandaa kwenda kulima unapofika shambani unakuta shamba limeshalimwa vizuri kabisa.

Ukiwa na akili finyu utalilima upya ukiwa na akili nzuri utaanza mipango ya kupanda na kupalilia.

Kamanda upo mpaka hapo !!!. Sasa sijui wewe utajiweka kundi gani.
 
Sasa ni sababu zipi zinazofanya tutafute mafanikio au kushindwa kwake kwa kumfananisha na mawe yaliyoutingisha ulimwengu ?

Kwanza umemwelewa mleta thread?? Kauliza swali kwamba; Pilika pilika za majeshi yetu zisizo za lazima na hadi sherehe fupi fupi za Sikukuu yetu tena bubu, Je tuone kama mafanikio kwa Mange?? Ni swali tu ila usimpinge kwa hoja zisizoendana na mada. Si ungemjibu Hapana au ndiyo kwa sababu kadhaa?? Mfano, Wadhani kuwa migari yote, pikipiki na masilaha waliyoonesha majeshi yetu mitaani ni gharama kidogo?? Nadhani huy dada ni wa kudhibiti kwa hali yeyote ile. Amelitia taifa hasara kubwa. Nalaani wazo lake lililotufanya tutumie fedha iso na mpango leo. Nisingependa aungwe mkono kwa vyovyote
 
Tunaelezwa Watanzania kadhaa walijitokeza kuandamana Dar es Salaam na kukamatwa mtaa wa Samora, Posta. Watanzania wachache waliopo Marekani, Ujerumani, Sweden na kwingineko waliitikia wito. Je, matokeo hayo ni kushinda au kushindwa kwa Mange Kimambi ambaye ni mwasisi na mhamasishaji mkuu wa maandamano hayo?

Mange ameweka maskani Marekani. Akiwa huko alitangaza kuwa leo, Aprili 26 yangefanyika maandamano. Ilikuwa kama utani. Mara mfumo wa utawala ukashituka. Ukaanza kumjibu Mange na kutoa vitisho dhidi ya wale ambao wangeandamana.

Vitisho vilijiri kila pembe ya nchi. Hata Rais John Magufuli alichimba mkwara kuhusu maandamano. Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba aliyazungumzia na kutoa onyo. Inspekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro alikoroma. Kuna mkoromo mkubwa zaidi wa Kamanda wa Polisi Dodoma, Gilles Muroto aliyeahidi kutoa mkong'oto wa mbwa koko. Dooh!

Kimsingi Mange aliuamsha mfumo wa nchi kudhibiti maandamano yake ambayo aliyasema bila kuyaratibu. Mange alisema kungekuwa na maandamano, mfumo wa nchi ukaanza kupambana na maandamano kana kwamba yaliandaliwa. Je, Mange ameshinda au ameshindwa?

TUMUULIZE OSAMA BIN LADEN

Agosti 7, 1998, balozi za Marekani nchini Tanzania na Kenya zililipuliwa. Watu takriban 200 walipoteza maisha. Memba wa Al-Qaeda, Fazul Mohammed na Abdullah Ahmed walitajwa kuwa 'mastermind' wa milipuko hiyo ya mabomu yaliyotegwa kwenye magari.

Ni kuanzia wakati huo Marekani walielekeza umakini wao kwa aliyekuwa bosi mkuu wa Al-Qaeda, Osama Bin Laden na msaidizi wake, Ayman Al-Zawahiri kama watu hatari mno kwao.

Septemba 11, 2001, Al-Qaeda ilitekeleza mashambulizi makubwa zaidi Marekani. Watekaji 19 walioongozwa na kijana msomi, Mohammed Atta, waliteka ndege na kushambilia jengo la Kituo cha Biashara Ulimwenguni (World Trade Centre 'WTC') kwa mafanikio makubwa, wakalenga ngome kuu ya ulinzi Marekani, Pentagon lakini shambulizi lilidhibitiwa, shambulizi la Makazi ya Rais, White House lilifeli.

Baada ya matukio hayo na mengine mengi, Marekani iligeuka mtumwa wa Osama na Al-Qaeda. Kila mara walikuwa wanatangaza kufanya shambulio kisha Marekani walitumia nguvu nyingi kupambana kulikabili shambulio lililotajwa.

Ikawa mwendo ndio huo, Al-Qaeda wanatangaza tarehe na eneo ambalo wangeshambulia kisha Marekani nao ikatumia nguvu kubwa kulikabili shambulio. Nguvu ya Marekani iliyotumika haikuwa inakabili shambulio, bali maneno matupu. Nguvu kubwa ya kijeshi ilitumika kukabili shambulio hewa.

Mwaka 2003, Osama alitoa hotuba iliyorushwa na televisheni ya Al-Jazeera, akitoa dira ya mapambano ya Al-Qaeda dhidi ya Marekani. Alikiri kwamba mtandao wao usingeweza kuishinda Marekani kutokana na uwezo mkubwa ambao taifa hilo linao, ila shabaha yao ni kuidhoofisha kiuchumi.

Osama alisema kuwa baada ya mashambulizi ya Septemba 11, 2001, mafanikio ya shambulizi la WTC na kufeli kwa mashambulio ya Pentagon na White House, Al-Qaeda iliifanya Marekani iwaheshimu, kwa hiyo kila ilipotangaza kwamba ingeshambulia sehemu fulani, Serikali ilitumia fedha nyingi kupambana na tishio lao.

Osama alitoa makisio yake kwamba Marekani ilitumia fedha mpaka kiasi cha dola 500 milioni (Sh1.1 trilioni) kukabili shambulio ambalo wao walilitangaza kuwa wangelitekeleza wakati hata hawakuliandaa.

"Lengo letu ni kuidhoofisha Marekani kiuchumi. Jeuri ya Marekani ni uchumi wao. Tutaendelea kuwatishia na wao hawatadharau kwa sababu wanajua tunaweza kuwashambulia na kuwaumiza. Jinsi wanavyotumia nguvu kubwa kujilinda ndivyo uchumi wao unavyoathirika," alisema Osama.

Chukua hii; Osama na Al-Qaeda walikuwa wakiiumiza Marekani kwa kutishia kushambulia kisha wao waliingia benki kutoa fedha ili kudhibiti shambulizi lililoahidiwa. Shambulizi hewa!

TUMKOKOTOE MANGE

Mange alisema maandamano yangefanyika. Serikali imefanya kazi kubwa mno kuyakabili. Maonesho ya vikosi vya majeshi ya ulinzi na usalama, magari na ndege zilizorushwa hewani ili kutishia watu wasiandamane, unaweza kujiuliza Serikali imetumia pesa kiasi gani?

Watu wamekamatwa kwa hofu ya maandamano. Biashara nyingi zimefungwa kwa hofu ya maandamano. Usiku jana nilikuwa kwenye klabu moja naangalia mpira wa Klabu Bingwa Ulaya kati ya Bayern Munich na Real Madrid. Tukashituka TV zinazimwa, kila kitu kikazimwa, tukaambiwa tutoke. Nje kulikuwa na Land Cruiser ya Polisi.

Awali uongozi wa klabu ulijieleza kwamba wao wanaruhusiwa kisheria kukesha, lakini Polisi waliwajibu: "Hapa hatuangalii sheria, ni agizo la dharura kwa leo." Watu wakaondoka wanasema "Mange huyo katuponza, wanahisi tutaanza kuandamania humu."

Hesabu rasilimali zilizoteketezwa kukabili tishio la maandamano ya Mange. Biashara zilizofungwa kisa Mange. Rejea ufafanuzi wa Osama kuhusu malengo yao ya kushambulia na kuitishia Marekani, baada ya hapo jiulize; Mange amefanikiwa au hajafanikiwa?

Ujumbe ambao utawala unatakuwa uwe nao ni kwamba tishio la maandamano ya Mange limeufanya uonekane haujiamini. Kama Mange aliye Marekani kwa kutumia simu yake pamoja na akaunti zake za mitandao ya kijamii ameweza kuipeleka puta, vipi viongozi wa upinzani wenye wafuasi wengi nchini?

Lingine kubwa la kukaa nalo ni kwamba maelfu ya watu kutookana barabarani isionekane ndiyo kushindwa kwa Mange na kufanikiwa kwa Serikali. Kokotoa kauli na hamasa za Mange kuhusu maandamano dhidi ya nguvu kubwa ya vyombo vya ulinzi na usalama iliyotumika kukabili maandamano, kisha chukua maneno ya Osama na mafanikio yao dhidi ya Marekani.

Dawa ya maandamano ni uongozi wenye kusikiliza sauti za watu. Siyo vifaru na maandamano ya askari barabarani. Heri watu waandamane ili watoe dukuduku zao, kuliko kuwadhibiti kwa nguvu kubwa. Kupambana na watu wenye kuandamana ni uoga. Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema alipata kusema bungeni kuwa heri wanaondamana barabarani kuliko maelfu wanaoandamana nyoyoni.

Nilichoona cha wazi ni kuwa Serikali inamheshimu Mange. Inajua ana ufuasi, kwa hiyo aliposema kungekuwa na maandamano iliamini yangetokea kweli. Kama Marekani ilivyomheshimu Osama, alipotishia kulipua Hollywood ilibidi shughuli zisimame na pesa nyingi zitumike kulikabili shambulio, walijua Osama alikuwa na uwezo kweli wa kushambulia. Kama tishio la Osama lilivyoifanya Marekani 'ipaniki' na kuboresha ulinzi, ndivyo Mange 'anavyoipanikisha' Serikali ya Tanzania.

Wewe umeonaje; Mange amefanikiwa au amekula za uso?
Mkuu nakubaliana na wewe, mawazo yako kama ya kwangu, madege yamerushwa chini chini ili kututisha, jf ilizimwa ili tusihabarike. Kwa ujumla tumeona aina ya viongozi wa sasa, waoga, washamba wasiojiamini
 
Sasa yanaitwa maandamano ya Mange Kimambi, ila kabla ya leo yaliitwa maandano ya April 26 na mbwembwe nyingi. Haya wahamisha magoli endeleeni kujifariji.
Ndo wange hack jamii forums
Nani anaweweseka Kati ya wananchi na serikali
 
Ebu niambie una shamba lako unatangaza una mpango wa kulima,unajiandaa kwenda kulima unapofika shambani unakuta shamba limeshalimwa vizuri kabisa.

Ukiwa na akili finyu utalilima upya ukiwa na akili nzuri utaanza mipango ya kupanda na kupalilia.

Kamanda upo mpaka hapo !!!. Sasa sijui wewe utajiweka kundi gani.
Well said
 
Sio Chadema tuu, hata kiongozi wa ACT alikuwa anachochea sana mitandaoni na ma-retweet kibao, mwisho wa siku, watanzania wakaona janja ya nyani.
Sio kwamba yamezuiwa kwa nguvu ila ni waandamanaji wameamua kutoandamana
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom