Precious Diamond
JF-Expert Member
- Jun 9, 2023
- 397
- 993
Wakuu,
Baada ya polisi kutoa tamko la maandamano kufanyika nchini, kila kona ni sifa tu kuwa 4R zimefanyiwa kazi, demokrasia imekuwa nchini, mama ametenda na kadha wa kadha, huku pongezi za akina Mbowe, Sugu zikitumika kama rejea ya kuwa hata wapinzani wenyewe wanakubali kuwa sasa Tanzania Demokrasia imekua kwelikweli.
Swali ni je, Maandamano haya pekee yanatosha kuwa kipimo cha demokrasia iliyokomaa nchini?
Uhuru wa vyombo vya habari bado ni changamoto kubwa, uhuru wa kujieleza bado nako, Watanzania wanakimbia kuwekeza nchini na kwenda nchi jirani sababu mazingira ya kuwekeza nchini ni mabovu, kodi chungu mzima zinazoongeza mzingo mzito kwa wananchi, ubadhirifu wa mali ya umma uko juu mpaka wanaambiwa wale kwa urefu wa kamba zao ripoti za CAG zinakuwa kama karatasi za makumbusho, bidhaa ziko juu na maisha yanaendelea kuwa magumu, huduma za kijamii mbovu mpakaka leo baada ya miaka 60+ bado tuna kampeni za kumtua mama ndoo, umeme changamoto maji safi shida nk, polisi hawana haki ya kuzuia maandamano kufanyika, jukumu lao ni kutoa ulinzi na kama ikitokea siku iliyotakiwa kufanya maandamano kuna kitu kinazuia polisi wanatakiwa kutoa siku nyingine.
Maandamano, mikutano ya hadhara sio hisani kusema Rais amefanya jambo kubwa kuleta kitu ambacho katiba hakikua imeruhusu, hakupaswa kuhushukuriwa kwa kurudisha au kuruhusu kitu ambacho tayari kimeruhusiwa na katiba, ilitakiwa awajibike kwa kwenda kinyume na Katiba!
Maandamano pekee yanatosha kuonesha utekelezaji kabambe wa 4R za Rais? Maandamano pekee yanatosha kuonesha Demokrasia imekua nchini?