Maandamano nchi nzima, yanaweza kutatua kero zetu?

Sipendi maandamano hata kidogo na wengi humu watasupport ila ushiriki wao unaweza usionekane.

hehehe na watakaokwenda naomba wasitaje kabisa kwamba kuna member JF anaitwa klorokwini. kamchumba kenyewe nimekapata juzi halaf honeymoon nikaifanyie rumande? khaaaa!
 
Mnatuchelewesha. semeni maandamano yaanze lini. Tuko tayari kuandamana kutoka kila kona ya nchi tuje tumtoe Vasco da Gamba white house.
 
Ww masabuli tu, kaz kujilovekeza tu kwa wakubwa, jamaa ameorozesha mambo ya msingi kabisa harafu unataka kuleta upupu wako hapa, maandamano yata mtoa anayesababisha haya ambaye ni ccm kwa nguvu ya uma.

hata huu nao ni upupu!
 
Kuwe na mkakati wa kuongea na polic nao washiriki vip maandamano
Mimi nnao wanajeshi sita mpaka sasa ambao wana ushawishi mkubwa sana jeshini Jf mambo yanasidi kuwa msuri sasa

mimi naifanya sana hii kazi kifupi polisi wote wa vyeo vya chini tuko nao na watatuunga mkono tusiogope vitisho jamani, hakuna atakae tutoa kwnyw makucha haya sichama cha upinzani wala dini yeyote, misri, tunisia libya wanavyama vya kisiasa vya upinzani siku zote na vina makelele kama mbwa asie na meno tuu..

TUSIOGOPE VITISHO...TUMECHOKAA
 
hehehe na watakaokwenda naomba wasitaje kabisa kwamba kuna member JF anaitwa klorokwini. kamchumba kenyewe nimekapata juzi halaf honeymoon nikaifanyie rumande? khaaaa!
hahahaha! Hebu rudi kwako chit chat. Humu tunaongea matatizo yetu.lol.
 
Mnatuchelewesha. semeni maandamano yaanze lini. Tuko tayari kuandamana kutoka kila kona ya nchi tuje tumtoe Vasco da Gamba white house.

We kunguru acha kuponza wenzako. Tunajua kuwa utaishia kwenye screen na key board kuhamasisha wasio na uelewa kama mlivyofanya kule Arusha. Hii ni dhambi kubwa kuponza wenzako wakadhurike miili yao baadaye mgombee maiti zao kisiasa kama mlivyofanya Nyamongo. Kuponza wenzako ni dhambi.
Kwa nini usijitundike tu kama una hamu ya kufa??
Mnastahili laana.
 
We kunguru acha kuponza wenzako. Tunajua kuwa utaishia kwenye screen na key board kuhamasisha wasio na uelewa kama mlivyofanya kule Arusha. Hii ni dhambi kubwa kuponza wenzako wakadhurike miili yao baadaye mgombee maiti zao kisiasa kama mlivyofanya Nyamongo. Kuponza wenzako ni dhambi.
Kwa nini usijitundike tu kama una hamu ya kufa??
Mnastahili laana.
Kama umetumwa, basi hapa hapakufai. Nani asiyejua kufa. Heri kufa ghafla kuliko kufa pole pole kwa mateso makuu ya mafisadi wa hii nchi. Je wewe utaishi milele?
 
Lini? Tujiandae kikamilifu, mimi nitaruka na ungo wangu kutoka Alaska.
 
Mnatuchelewesha. semeni maandamano yaanze lini. Tuko tayari kuandamana kutoka kila kona ya nchi tuje tumtoe Vasco da Gamba white house.
Kaka ni siku wanashereke uhuru wa kuitawala nchi kama ya kwao tunataka nasi tuonekane tupo natunaweza
 
No. Maandamano yatakuwa ni ya kupinga hali ngumu ya maisha, uchumi mbaya, na uendeshaji mbaya wa nchi. Kwanza tutataka mabadiliko ya mara moja, ikiwamo kuonesha wazi mabadiliko hayo, kwa kuwachukulia hatua wale wakuu wa ufisadi, kurudisha majumba na mali za serikali, kupunguza bei za bidhaa mara moja....
 
mmechemsha kwenye uchaguzi, mmechemsha bungeni kujenga hoja za msingi na kushirikiana na wenzenu sasa mnataka kuandamana!!! insp. saidi mwema shughulika hawa; tandika na virungu pamoja na maji ya washawasha!!!!!!!!!!!

Mkuu nguvu ya hoja zilifunikwa na wenye kutumia mitulinga ya hoja,ila ukweli haukwepeki,na haki haiombwi.Maandamano ya amani ni haki ya msingi ya mwanadamu.
 
Tatizo langu kubwa lipo kwa ndugu zangu waislamu wametekwa na ile dhana ya kuwa muislamu mwenzio ni nduguyo jambo hili leo ndio technique ya ccm wanayoitumia katika kutenganisha nguvu ya uma ya watanzania. Ikiwa mufti wa bakwata na waislamu wote Tz anatamka azarani kuwa analaani maandamano yoyote yanayofanywa na watz ya kutetea maslahi ya mtz mnyonge na kwenda mbali zaidi na kuyaita ni ya kuvunja amani tuliyonao eti kisa tu rais ni muislamu.

Tutafoutiana katika madhehebu ya dini lakini hatutofautiani katika matatizo yanayokumba taifa letu.Kuwagawa watu kwa misingi ya dini ni njia ya mwovu kukwepa matatizo ya msingi.
 
Mtaishia kusema kitambo kidogo......ooh wakati umefika bla bla ....hakuna kitu hapo.<br />
Kundi lenu la wanung'unikaji endeleeni tu kulalamika badala ya kuchapa kazi......Wazalendo wa kweli tulishaamua uvivu ni bye bye. Nyie endeleeni kuudekeza kwa maandamano.....kwa mtindo huo??.... maendeleo yatakuwa ndoto kwenu na kwa kundi lenu la wafuasi wa CDM.
<br />
<br />
Eti kuchapa kazi. Wewe si umeajiriwa kulinda maslahi ya mafisadi! Muda wote uko jf kukatisha watu tamaa pole! Kwa kusoma unazozitoa mtu yeyote atakuwa na wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri na hata elimu yako! Du nchi ya Magamba na M.T. I. N. D. I. O wa ubongo.
 
Mtaishia kusema kitambo kidogo......ooh wakati umefika bla bla ....hakuna kitu hapo.
Kundi lenu la wanung'unikaji endeleeni tu kulalamika badala ya kuchapa kazi......Wazalendo wa kweli tulishaamua uvivu ni bye bye. Nyie endeleeni kuudekeza kwa maandamano.....kwa mtindo huo??.... maendeleo yatakuwa ndoto kwenu na kwa kundi lenu la wafuasi wa CDM.
Eti kuchapa kazi. Wewe si umeajiriwa kulinda maslahi ya mafisadi! Muda wote uko jf kukatisha watu tamaa pole! Kwa kusoma hoja unazozitoa mtu yeyote atakuwa na wasiwasi na uwezo wako wa kufikiri na hata elimu yako! Du nchi ya Magamba na M.T. I. N. D. I. O wa ubongo.
 
Kama unaona wewe siyo mmoja wa Watanzania basi tunakuomba mkaanzishe nchi yenu,ama mkaombe uraia Zimbabwe, sisi Watanzania wenye chanjo ya Ndui.

Tumechoka sana, Tumekata tamaa, Hatuoni haja ya kuwa Watanzania kama hata kuweka wazi yaliyomo moyoni. Hakuna hata moja serikali ya Kikwete imeshafanya ama itafanya Kizalendo, kwani hata kwenye dhifa za Kitaifa wanashindwa hata kuimba wimbo wa Taifa kizalendo.
 
Hakuna mtu ambaye hajui kuwa kuchapa kazi ni moja wapo ya kujikwamua kiuchumi na kijamii.SWALI kama mtu amesomea ufundi,useremala na anategemea kuajiliwa lkn hamna na kuna serikali ambayo inabidi iwape ajira au kuwawezesha watu kujiajiri na inashindwa kufanya hivyo nini hatima ya watu kama hao.

Inabidi tuwe na mawazo jenzi na yenye tija siyo kupotosha jamii,hii ni dhambi kubwa unaposema ukubaliani na maandamano ambayo yanalenga kuleta ukombozi wa kweli.

Pia ukumbuke power and authority that legitimise government belongs to the people who have civic obligation to make the government accountable but those who have marriage with the plutocratic and stinking government are blind by these filth.
 
Jamani matatizo yote haya acha yatupate kwani shida huleta maarifa .

Tulizoea raha, Amani pasipo kujua nini chanzo cha Amani. Amani tuliyokuwa nayo ilighalimiwa si lele mama hivyo ili tuzidi kuwa na Amani inabidi wawepo watu wa kujitoa muhanga Umma uelimishwe waondokane na imani potofu juu ya amani ya nchi hii huku maisha yakibana siku hata siku. naona maandamano si jibu ila tujipange wale wenye uchungu na nchi hii kwa udi na uvumba tuipige shule jamii kwa kuwa hali halisi wanaiona wakati ukifika mabadiliko ni lazima.

Ebu tuungane tuuelimishe umma nao ndio utaamua kwani hata tukiandamana kama watu hawajui kwanini wanaandamana kama ni kwa woga wakidhani wana amani na kuandamana wanaambiwa ni kutaka kuiondoa amani ambayo wengi wanadhani ilishushwa kama mana toka mbinguni, kumbe amani inatokana na kutenda haki hivyo hawa watu tunaowaita waoga au wajinga siku uvumilivu ukiwashinda wataamua pasipo hata kuwaambia tuandamane.

Najua Mungu ana makusudi na nchi hii vuguvugu linaloendelea ni maandalizi ya jambo kubwa litakalokuja kutokea ole wao mafisadi na wale wote wasiouonea huluma umma huu kwani ipo siku watatoweka kama moshi.

Amini nawaambia ipo siku wale watakaokuwepo watashuhudia tuombe uzima mimi na wewe ila amini siku yaja. tumeonewa vya kutosha, tumenyanyaswa vya kutosha, tumepolwa vya kutosha ila siku yaja.
 
Back
Top Bottom