Maandamano makubwa kumpongeza Jakaya Kikwete!

Rais wetu ni very clever...alijua akiwafukuza mawaziri(washkaji zake) mwenyewe basi anaweza jenga uadui na hao mabeste wake so kaamua ni bora aite kamati kuu ili wamshinikize kufukuza hao mawaziri..so hata akiwatosa atawaambia mabeste kua haikua yeye ila ni viongozi wa chama ndio walimforce yeye kuwatimua...kwa kufanya hivo anabakia marafiki na hao watu...very clever MR PRESIDENT nimeipenda hiyo:A S thumbs_up:
 
Kuvuja baraza kila term ya uongozi wa JK ni dalili ya Rais aliye zaifu kupita kiasi. Sikumbuki ni nchi gani duniani imewahi kuwa na hali kama yetu, kila term baraza linavunjwa. Kimsingi hii inaonyesha ni jinsi gani raisi alivyo kuwa zaifu katika uongozi wake, na hata atakao wachaguwa natumaini hawatakua na jipya zaidi na wao kuambulia chochote kwa mda uliobaki (Natumaini watakua tu maswahiba ama masheji), kwani sasa ni mda wa lala salama.

Mimi sintatoa jasho langu wala kupoteza mda wangu kwa kufanya ama kufualia maandamano kwani hakuna kitu chochote cha kishujaa kilichofanyika, kama ni ushujaa jk angeufanya pindi alipochagua kwa mara ya kwanza mawaziri ambao ni wachapa kazi, na wala wasiomajambazi.

Nawashauli wadau wote msipoteze mda wenu kwa upuuzi kama huu.

Nyoka ni nyoka,
ccm ni ccm,
Sera ya ccm ni moja
Anae toka na anaeingia wote sawa
Wanamisemo mizuri sana bali shida zinaendelea
Tusubili 2015
 
Yaani kuvunja baraza la mawaziri ni uamuzi mgumu??
Labda kwa kuwa naye JK ni mchafu
nami naapa akichukua maamuzi magumu kweli na kuamua kujiuzulu yeye mwenyewe, nitawashawishi wakazi wote hapa kisiwani tuandamane kumuunga mkono. Tuatatembea kwa miguu mpaka Msoga kumpongeza!

 
[h=3]Rais Banda amtimua waziri[/h]


Kiongozi mpya wa Malawi Joyce Banda amemtimua Waziri wake wa mashauri ya kigeni, Peter Mutharika, nduguye Rais aliyefariki akiwa afisini.

Bw.Peter Mutharika alitazamiwa kama mrithi wa marehemu kakake katika uchaguzi wa mwaka 2014 wakati ikitazamiwa kua Rais aliyetoweka angestaafu.





Mabadiliko haya ya baraza la mawaziri linatokea siku chache baada ya mazishi ya aliyekua Rais.

Bibi Banda alikua ni makamu wa Rais kuanzia mwaka 2009 lakini baadaye akakosana na Rais na kujitokeza kua mkosoaji wake mkali.

Bi Joyce Banda alilazimika kujiuzulu kutoka chama cha Democratic Progressive mwaka 2010 alipokaidi amri ya kumkubali Peter Mutharika awe mrithi wa rais.


Kufuatia kifo cha Bw Mutharika tareh Aprili, kulikuepo na tetesi kua washirika wa waziri wa mashauri ya kigeni wangejaribu kuzuia mkondo wa katiba wa kumkabidhi madaraka Bi Banda,ambaye tangu hapo alikua ameisha unda chama chake.
Chanzo bbcswahili
 
Mnapongeza kwa late of action. wabongo bwana kweli njaa simewazidi na kupenda t-shirt na kofia za bure.
 
Utaingia ktk maandamano hayo wewe mwenyewe,ivi KIM KARDASH HUONI HAYA KULIPWA BUKU 2
 
Mm nawapongeza Wazee wa magwanda, maana wao ndio walioshikia bango suala la mawaziri. Kwa hao magamba nampongeza Filikunjombe. JK na magamba wenzake wameogopa Peeeeeeople's Poweeeer tu. Ulitegemea wangefanyaje na CDM imeyaambia hayo magamba kuwa itawachongea kwa wananchi? Big up Sugu kwa mkwara uliowachimba pale mjengoni. Karibu Kisimamkojo uhamasishe CDM.
 
Sioni la kumpongeza apo zaidi ya kumlaumu tuu bse aliweka viwavi jeshi kwenye baraza lake uku akitegemea mazao kuchipua thubutuuu

fedha walizotafuna zingekuwa zimenunua ct scan kwa ajili ya kanda ya kusini na nyanda za juu kusini. Kuna wagonjwa wengi wanahitaji kipimo hicho hawapati. Ultrasound zilizopo wilayani zilinunuliwa ten years ago na hazijafanyiwa matengenezo. X ray ndo zipo hoi kabisa! Unakuja kuniambia unapongeza mtu kuwaondoa wezi bila kuwachukulia hatua na kuwabadilisha wezi wengine.
 
Labda kwa kulaani kwa kuchelewa kwake kuchukua hatua hadi hali ikawa hivi.

Amechelewa? amma kweli wewe una fikra potofu sana. Na ile sheria ya kuruhusu mdhibiti mkuu wa mahesabu afanye kazi zake bila kuingiliwa na wizara au taasisi yoyote uliileta wewe au aliileta Slaa?
 
Hapa ni sawa na kumpongeza jirani wa nyumbani kwako kwa uamuzi wako wa kumfukuza mkeo, yaani ni wapi na wapi? Kamat kuu
 
Back
Top Bottom