Maandamano makubwa kumpongeza Jakaya Kikwete!

Mimi pia naungana na watanzania wote, kumpongeza Rahisi wa Tanzania kwa atua hii nzuri ya mabadiliko, "Hakika sas Tanzania itapiga hatua ya Maendeleo. Wabunge Hongereni kwa uwamuzi mzuri mlio uchukua wakutaka mabadiliko kwa mawaziri.


naona idadi ya 'wahapa hapa' inazidi kuongezeka! ni ugonjwa mbaya kupita ebola! watu wenye huu ugonjwa ni wa kutengwa nao.
 
Kwahiyo vijana wa kitanzania wao kazi yao kuandamana kupinga na kupongeza!

Hii ni dalili tosha kwamba unemployment rate ipo juu sana!

mfano hai ulikuwa leaders, siku aliyopumzishwa muathirika wa mtikisiko wa ubongo! virus wa idleness walikuwa juuuuuu kupita maelezo!
 
Maandamano makubwa yanatarajiwa kufanyika nchi nzima kumpongeza rais kikwete na kamati kuu ya ccm kiujumla kwa kufanya kuchukua maamuzi magumu ya kulifanyia mabadiliko makubwa baraza la mawaziri.

Rais kikwete ameamua kufanya maamuzi magumu hayo licha ya kwamba kuna jukumu zito la maandalizi ya bajeti za wizara na kwa hiyo ni changamoto kubwa kuingiza watu wapya kwa maana ya nafasi za mawaziri, lakini hata hivyo, hao wapya itabidi wategemee zaidi mihtasari ya watendaji watakaokuwapo katika kila wizara husika itakayoguswa na mabadiliko.

Wananchi mbalimbali nchini wamepongeza hatua hiyo ibnayotarajiwa kuchuliwa na rais kikwete huku wakisema kwamba hatua hiyo itaifanya ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) iwe na nguvu kubwa ya kuisaidia serikali kupambana na ubadhirifu unaofanywa na mawaziri kwa kushirikiana na watendaji wa serikali wasio waaminifu.

Naye mbunge zitto kabwe ambae alishikia bango hoja ya kutaka bunge lipige kura ya kutokua na imani na waziri mkuu,akizungumza bungeni wiki juzi aliwapasha mawaziri kwa kuwaambia ''Mawaziri msimsingizie Raisi na kumchafua kwa uzembe wenu na ubaridhifu wenu wa kushindwa kusimamia mali na pesa za walipa kodi kwa manufaa yenu binafsi i lazima muwajibike na mchukuliwe hatua stahiki''
nani kakwambia mawaziri huwa wanaandaa bajeti zaidi ya kusoma pale bungeni ! na ndo maana huwa wanashindwa kujibu maswali
 
mbona mbowe hajawahi kuvunja hata kamati ya harusi,we unadhani kuvunja baraza la mawaziri mwezi mmoja na nusu kabla ya bajeti ni jambo jepesi..?
Jamani hilo baraza la mawaziri limevunjwa au LINATARAJIWA kuvunjwa? Leo hii mawaziri wanafanya kazi zao kama kawa!!!!
Amesema atavunja ila BADO hajalivunja!!!
 
mbona mbowe hajawahi kuvunja hata kamati ya harusi,we unadhani kuvunja baraza la mawaziri mwezi mmoja na nusu kabla ya bajeti ni jambo jepesi..?
Kwani bajeti ya tz ina umuhimu sana! Mbona haifuatwi? bilioni za rada zinatumiwa bila idhini ya bunge,
ulimsikia Cheyo alivyolalamikia matumizi makubwa nje ya bajeti na bila idhini ya bunge,
umesikia taarifa ya CAG, mapesa watu wanagawana tu - unafikiri huko kugawana gawana kunakuwepo kwenye bajeti?
Pili je kuvunja baraza bila kurudisha pesa zetu walizokwiba kunamsaidia sana mlalahoi?

Lipi gumu zaidi; Kuvunja kamati ya harusi au kuvunja baraza la mafisadi!
 
Mtoa taarifa hii ana mapungufu makubwa juu ya uelewa wa namna mfumo wa serikali unavyofanya kazi, hususan maandalizi ya bajeti ambayo tayari yanakaribia kufikia ukingoni. Ukiacha uwasilishaji wa kusoma unaofanywa kwenye Kamati na Bungeni, Mawaziri wa Tanzania hawaelewi mfumo mzima wa maandalizi ya bajeti na ndiyo maana wanashindwa hata kuelewa usimamizi na utekelezaji na usimamizi wa matumizi. Ni mawazi wachache sana wanaoelewa leo hii Tanzania inatumia mfumo gani wa Bajeti.

Pili hayo mabadiliko ya mawaziri bado ni njozi hadi hapo yatakapofanyika, hilo halikuwa suala la kusubiri muda wote huu, kwa hiyo hakuna maamuzi magumu yaliyofanyika hadi sasa, zaidi ya porojo. Tusubiri tuone zaidi ya kuwahamisha Wizara na moja kwenda nyingine kama ilivyozoeleka sioni mabadiliko makubwa kama wengi walivyoaminishwa.

tego sikio redioni kuanzia kesho asubuhi na keshokutwa ununue sana magazeti.
 
Apongezwe kwa lipi, kwani hii ni mara yake ya kwanza kufanya mabadiliko kwenye hilo baraza lake? wacheni kumpa maujiko yasiyo stahili, Nitampongeza siku atakapo kamata wote wanao husika na ufisadi na kuwafunga. Ila nitampongeza zaidi na kuandamana kumuunga mkono siku atakapochukua maamuzi magumu ya kujiuzulu nafasi ya uraisi kisha uitishwe uchaguzi mkuu.

Alafu kama ni kweli wasisubutu kuja kufanya hayo maandamano yao huku arusha.

Rais wa nchi gani huwa anafunga watu labda rais slaa..,mi ninavyojua kazi ya kuhukumu ni ya mahakama kwa nchi inayotawaliwa kwa kufuata misingi ya utawala wa sheria
 
Back
Top Bottom