Maandamano CCM BUKOBA kuunga mkono ilani za chama

Kaa la Moto

JF-Expert Member
Apr 24, 2008
7,903
1,053
Tunapoelekea uchaguzi tutaona mengi.

Tangu jana yamekua yakipita matangazo hapa mjini kwamba wana ccm watakuwa na maandamano ya kuunga mkono utekelezaji wa ilani za chama na utahutubiwa na mjumbe wa nini sijui wa umoja wa watoto (No nilimaanisha vijana) wa ccm taifa.

Kama ilivyo ada nadhani ilikuwa ni kujaribu kupiku yale yaliyofanyika hivi karibuni wakati Lwakatare akipokewa rasmi CHADEMA.

Pia nadhani kupoza hali tete iliyojitokeza tokana na hotuba ya Dr Slaa hapa Bukoba kuhusiana na hali tete ya udhibiti wa uchumi wa nchi yetu.

Nimeshangaa kuona kikundi si cha zaidi ya watu mia moja tu wakifanya maandamano hali isiyo ya kawaida.

Sasa najiuliza je hii inaonyesha ni kiasi gani watu wameanza kukata tamaa na chama hiki?
Je kama hali ndiyo hii 2010 mambo si yatakuwa hatari zaidi?
5121d1246448535-maandamano-ccm-bukoba-kuunga-mkono-ilani-za-chama-dsc00470-i.jpg


5122d1246448535-maandamano-ccm-bukoba-kuunga-mkono-ilani-za-chama-dsc00471-i.jpg


DSC00470 i.jpg

DSC00471 i.jpg
 
Ni kweli tutaona mengi sana katika kipindi hiki cha kuelekea kwenye uchaguzi mkuu but kama wao wanasema kuwa Ilani ndio watu waanze kuona matunda ya Ilani na sio sasa hivi
 
Yaani sijaelewa., wanaziunga mkono gani?
Kwani nani kawambia anazipinga hizo ilani zao?

Wao si ni chama tawala ndo wanakusanya kodi zetu?

Mi nilitegemea watekeleze hizo ilani,kwa hizo kodi zetu wanazo kusanya, sasa wakisema wanaziunga mkono ili hali hawazitekelezi inatusaidia nini?


Completely nonsense!
 
most of the members involved in demo ARE HIRED OUTSIDE BUKOBA!
 
Siwezi kushangaa maana waliposema masuala ya EPA, wao walipita na kupongeza na kumbuka ile bajeti wao walianza kampeni na kudai kuwa ni nzuri,
 
Hao watu mia moja ni hatari sana ,hao ndio wanaotumika au watakaotumika katika kuvuruga uchaguzi,kushambulia wananchama wa vyama mbadala kwa minyororo na nondo. Kule Nchini Zanzibar wanawaita janjaweeds ,huwa wanaleweshwa wanaruhusiwa kuvuta bangi wanapikiwa ugali na maharage kisha kupewa maelekezo ya mikakati ya kushambulia na kutesa na huwa wanasindikizwa na gari la polisi kwa mbaaali ili wakionekana kuzidiwa nguvu wapate msaada na kinachotokea katika hali kama hiyo wao wataachiwa huru na wanachama wa chama mbadala kukamatwa na kubambikizwa kesi za uvunjaji wa amani ,kuweni makini na watu hao ambao huwa wanatumiwa katika shughuli za kuonyesha kuwa CCM nayo ina wanachama.
 
Hivi hao janjaweed bado wapo huko nchini Zanzibar?
Wapo si ulisikia vitu vyao kwenye uchaguzi wa magogoni ,walitegwa wakategeka ,sasa uchaguzi ushakuwa confirmed kuwa utasimamiwa na UN , na Pemba kuna tetesi kuwa wao huenda wasishiriki uchaguzi maana huenda wakajikata kivyao.
 
Bado wapo lakini wengi wao walilishwa coke kwa wingi nyakati za uchaguzi sasa wamekuwa majununi.
 

Attachments

  • _40966302_beating416ap.jpg
    _40966302_beating416ap.jpg
    29.8 KB · Views: 47
Tunapoelekea uchaguzi tutaona mengi.

Tangu jana yamekua yakipita matangazo hapa mjini kwamba wana ccm watakuwa na maandamano ya kuunga mkono utekelezaji wa ilani za chama na utahutubiwa na mjumbe wa nini sijui wa umoja wa watoto (No nilimaanisha vijana) wa ccm taifa.

Hii ni taarifa au kebehi?
 
Basi BK kura nyingi za CCM wanapata kutokea kwenye vikundi vya wanawake kwani tiyari walishapewa khanga na vitambaa na wamevitunza kama utafikiri ni nguo ya kutokea outing. Sasa Chadema ni vizuri nawao wakawa na yuniform ambayo inatambulika kama mashati, khanga, vitambaa, tena wauze vitanunuliwa hiyo ni njia mojawapo ya kuhamasisha chama.

Pili Vijana wengi unaowaona barabarani hawakujiandikisha au tiyari waliuza shada zao. Ni vizuri kuwa na mkakati wa hawa vijana wakaandikishwa kusudi watumie haki yao ya Uraia.
 
Back
Top Bottom