Maandamano Cardiff na New York Vs maandamano Dar es Salaam

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,268
UZOEFU WANGU WA MAANDAMANO UINGEREZA NA MAREKANI

Nimesoma hapa kuhusu mapokezi ya Tundu Lisu na maandamano yake na jinsi polisi walivyolitawala jambo lote kwa hekima na likapita salama salmini.

Miaka mingi illiyopita mimi kijana niko Uingereza na ni mgenikatika nchi hiyo kwa kila jambo.

Siku moja ghafla shule wanafunzi wamekusanyika wamepeana taarifa kuwa kuna maandamano tunakwenda kuandamana Mc Donald’s kupinga ukatili wao kwa wanyama kwa kuwachinja kutengeneza mikate ya nyama (Humburger).

Kwangu mimi hiki kilikuwa kichekesho cha mwaka.

Nikawa naiwaza hoteli ya Bakhresa ilikuwa Mtaa wa Mkunguni na Chura kwenye kona pale naleta picha wanafunzi wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam wamesimama nje na mabango wanamlani Bakhresa kwa kupika pilau au biriani ya kuku, mbuzi, ngo’mbe na kumwita jitu katili lisilokuwa na huruma kwa wanyama.

Mc Donald’s haikuwa mbali na chuo chetu na muda haukupita wanafunzi wako barabarani na mabango na polisi zamani wameshapata taarifa na wao wako mtaani kuongoza maandamano kwa salama.

Hakuna ving’ora vya magari ya polisi, hakuna marungu, washawasha wala mabomu ya machozi wala bendera nyekundu la onyo la kutawanyika mara moja fumba na kufumbua.

Lakini mimi kunguru muoga nimekwenda kule kwa kadha sikufata kadha wa kadha.

Sikushiriki katika maandamano.

Wanafunzi wamefika Mc Donald’s iko ‘’High Street,’’ (Uingereza mitaa mikubwa kama Oxford Circus London inaitwa hivyo) wamepiga makelele yao askari wako pembeni wanaangalia hadi mwisho wamemaliza ghadhabu zao wamefunga madiramu yao hao wanarudi shule.

Nikawa nimejifunza jambo kwa hawa Waingereza.

Nikawahadithia wenzangu nikawaambia ingekuwa kwetu saa hizi mko Msimbazi Polisi, Kituo cha Kati wengine mna ngeu mnavuja majasho na damu, mmevunjwa mikono na miguu, mmepoteza viatu saa simu na madhila chekwa mmeyapata na pale Mc Donald’s mgahawa ungefungwa na na maduka ya jirani pengine yamevunjwa vioo.

Jamaa wamepigwa na butwaa wanaiuliza, ‘’Why?’’

‘’Kwa nini?’’

Nikawajibu hayo mliyofanya mnahatarisha usalama wa nchi.

Hawakunielewa kabisa.

Kiasi wasinielewe.

Basi siku moja niko New Jersey kwa familia moja ya Kimarekani wamenialika chakula.

Tukaingia katika siasa.

Mtu na mkewe wote wasomi.

Wamenipa mshangao walivyokuwa wanaitukana serikali yao na kuiita serikali ya kidhalimu na wakaniambia kuwa kesho kuna maandamano Manhattan, New York sehemu niliyokuwa naishi na wakaniambia nisikose kuhudhuria kuwaunga mkono kupiga vita dhulma na ushenzi wa serikali yao.

Siamini masikio yangu

Kilichokuwa kinapingwa ni majeshi ya Marekani kueneza vita kila mahali na kwa wakati huo walikuwa Mashariki ya Kati.

Nikasema nitakwenda kujionea maandamano ya Marekani yakoje?

Naingia katikati ya mji naam niko mbali nimeshuka kwenye treni nakaribishwa na ‘’Ghetto Blaster,’’ haya ni maspika makubwa yenye ‘’watts,’’ kubwa zinazotoa sauti ya mdundo mkubwa ya kuhofisha.

Maspika yanamtoa Stevie Wonder anaimba ‘’protest song,’’ ‘’Pasttime Paradise,’’ nyimbo ya malaalmiko.

Maspika yanapiga muziki na maspika yanatoa cheche kali kutoka kwa wazungumzaji tofauti na kila anaechukua ‘’mike,’’ anatema moto mkali dhidi ya serikali.

Polisi wa New York wanatisha jinsi walivyosheheni silaha.

Wapo mtaani kwenye maandamano mikono wamekunja nyuma wamesimama pembeni mwa barabara wako wengi, waandamanaji wakisogea na wao wanafuata nyuma.

Waandamanaji wakisonga mbele na wao wanasonga mbele nyuma yao kimya, wako waandamanaji wanaosimama mbele yao na kuwapiga picha na wakati mwingine wakasimama pembeni yao na kupiga picha na wao utadhani wako ‘’picnic.’’

Wako tuli wala hawatikisiki wala hawasemi kitu.

Wapole.

Maghrib imeingia waandamanaji naona wanazima muziki na wasemaji hawazungumzi tena wanafunga vyombo vyao na mabango yao mengine wameyatupa barabarani hao wanatawanyika na askari nao hao wanaondoka taratibu na kwa usalama.

Yaliyotokea leo Dar es Salaam ni mwanzo mzuri.

Kuna msemo Wamarekani wanaupenda sana katika kueleza namna ya kuepuka shari wanasema, ‘’It takes two to Tango.’’

Tango ni mtindo wa dansi ambao huwezi kucheza peke yako sharti uwe na patna.

Picha: Angalia picha ya pili yuko askari katikati ya waandamanaji.

MAANDAMANO NEW YORK 4.jpg


MAANDAMANO NEW YORK 3.jpg


MAANDAMANO NEW YORK 5.jpg
 
Naam Sheikh ni mwanzo mzuri wa uungwana na ustaarabu lakini pia kuaminiana baina ya vyombo vya dola na raia. Nataraji kuona mwendelezo mwema katika hili.

Pia, liwe jukumu la waandamanaji kudhibiti "wahalifu" ambao hutaka kutumia fursa hiyo kutenda jinai zao kama kupora nk.
 
Back
Top Bottom