Maalim Seif: Tunataka Zanzibar yetu!

good point,hawana haja na muungano huu. Ni haki yao ya msingi kuchagua watakacho.
Waondoke sasa, maneno matupu kila siku hayasaidii.

Nimeona mwingineanasema watanganyika wadai tanganyika yao ili wao znz waondoke..alaaaa....nanianataka kuondoka? Anayeona tabu aondoke, full stop.
Muungano huu wa kijanja janja, ondokeni basi na msilete habari za mikataba hapa. Muingie kwenye ea community kama nchi kamili, tushirikiane katika level hiyo.

Kelele za nini?

laiti mngeweka mazingira rahisi kama unavyosema mbona zamani muungano usingekuwepo. Mnau;inda kwa magego na nguvu zote. Rais wa nchi moja kuondolewa urais na kuwekwa chini ya ulinzi kwa kuukataa muundo huu, unazani ingekua mnataka kirahisi hicho si mngemruhusu akarudi zanzibar na mkawauliza wazanzibari wenyewe wanasemaje?

Mkaweka sheria kali hata muungano usisemwe ukisema muungano utajuta. Majeshi yakachanganywa.. Security ya zanzibar ikauliwa na kuachwa ya muungano ili kijulikane kila kitendekacho zenji. Mmetungangania halafu mudai tuondoke
 
kwani mnachokitaka hasa ni nn wenzetu nyie?? Au mmeahidiwa kwamba mtapewa pesa za bure mkijiunga o.i.c ambayo ni vigumu kujiunga mkiwa ndani ya muungano??? Kama hamzioni faida za muungano mjetenge, then nje ya muungano mtazijua faida lukuki ambapo itakuwa ngumu kuwapokea tena

tunataka nchi yetu sasa tumechoka......
 
Kwa kauli hiyo, Mkuu alitakiwa kuwa amekwisha kamatwa. Ila kwa hilo na mimi naunga mkono, Let Tanzania RIP.
 
kwa kauli hiyo, mkuu alitakiwa kuwa amekwisha kamatwa. Ila kwa hilo na mimi naunga mkono, let tanzania rip.
zamani hio ingeliwezekana sio leo. Na nnakuambia watu wa muungano wanajua kishanuka,

kwa kweli wazanzibari kwa sasa wanadai nchi yao, huyu seif unaweza kumwita just kapima upepo tu ili asichushe lkn kwa sasa wazanzibari wameamua kuachana na cuf na ccm. Kuna moving ya nguvu wanaojua siasa wanajua nn kiko kule.

Kule ni kimoja tu watu wanataka nchi yao tena yenye mamlaka kamili. Wamechoka kupigwa hadithi. Ss na nyny ndugu zetu wadamu udugu wetu haukuletwa na muungano.

Kama hujui huyo sultan wa zanzibar basi ukoo wake unahusu tanganyika, mama zake ni wana kindaki ndaki wa tanganyika. Salim ahmed salim mama yake mmanyema kama hujui ni mtanganyika. Mwinyi. Jumbe, moyo na wengineo wana asili ya tanganyika hata mm niandikie nna asili pia ya tanganyika. Ila hii haiondoi haki yetu ya kudai nchi yetu zanzibar

udugu wetu wa damu utabakia hata muungano ukiwa haupo kama ilivyokua zamani
 
kwa hio umekubali kama unaspin ?

wazanzibari waliomuondoa mkoloni muarabu ili wawe huru, wawe na sauti ya kuamua juu ya hatma yao ndio hao hao leo wanaona kua kumbe kuungana na hawa ndugu zetu kumepelekea kupoteza kile ambacho ss tulikipigania kutoka kwa mkoloni na sultan.

hatukumpindua sultan ili tutawalie na muafrika mwenzetu. ss tunataka muungano wa usawa muungano unaoheshimu hadhi yetu na maamuzi yetu.

ktk muungano huu ambao watanganyika wao ndio muungano hatuhuhitaji.wizara zote zisizo za muungano watanganyika wanashiriki kama Tanzania na zanzibar haina sauri juu ya hilo. tukisema ss walalamishi.

sizani kama Tanganyika ingekubali kuchukua nafasi ya zanzibar na zanzibar kuwa Tanganyika. TFF imajulikana na FIFA kua muwakilishi wa Tanzania wakati michezo si muungano. elimu ngazi ya chini si muungano UNESCO inatambua Tanganyika kama Tanzania. Ardhi , Miundo mbinu na mengineyo. tuwe wa kweli na wapenda haki hata kama nyny ndio mnazulumu jueni kua zanzibar wana haki juu ya madai yao

MSITUMIE MBINU ZA GHILBA NA SPINNING NA KUTUGAWANYA
Mkuu wangu hakuna mtu anaye spin hapa isipokuwa nakueleza Historia ya Zanzibar na ukombozi wa Afrika. labda nikujuze tu ya kwamba harakati za Uhuru wa nchi zetu ulianzia Zanzibar kwa baada ya kuundwa African Association (AA) na kisha wakaenda bara kufungua tawi lake. Hawa ndio walikuja Ungana na Shiraz party Zanzibar wakaitwa ASP na Bara wakabadilisha jina na kuitwa TANU lakini vyama hivi vyote vinatokana na mbegu moja na azma moja.

Pili, Nimekwambia hawa Wazanzibar wanaitaka zanzibar yao ni kina nani? maana wengi wao walikuwa wanachama wa Hizbu chama cha Sultan ktk uatwala wa Sultan kama ilivyotokea Mapinduzi ya Libya. Na hakuna hata mmmoja wa hawa watu alijkuwa katika baraza la Mpainduzi la kwanza - HAKUNA...Pengine huyo mzee wetu Nassor Moyo kasema hoja hii ni ya Wanzanibar wasikiwe japokuwa naye uzee unamwingia vibaya maana huyu alikuwa ktk watu ambao Karume alitaka kuwamaliza akasalimishwa na Nyerere. Na huyo Mke wa Karume yeye alikuwa nani? si mke tu wa Karume kwani alijua hata Mapinduzi yatakuwepo..

Mkuu wangu, Nakukubali sana unaposema Wazanzbar wanataka kujitenga lakini so hawa wachumia tumbo. na kama kuna ukweli mkubwa kwamba Wazanzibar ndio wanaotaka kujitenga basi hakuna njia bora na rahisi kama kufanya refendum na tuwasikie kwa kura zao badala ya kuikabidhi nchi hiyo mikononi mwa wagaidi wengine wenye agenda zao. Jiulize kwa nini Maalim Seif anakwepa kura za maoni? huyo Jussa alisema nini kuhusu kura za maoni kwa kuhofia Wazanzibara!.. Wazanzibar pekee ndio wenye haki ya kuweka madai haya na ipitie kura zao sio maneno ya Jussa na Maalim Seif.. Hawa ni wachumia tumbo tu.
 
Ni jambo la kusikitisha kwamba, wakati nchi ndogo zinajaribu kuungana na nchi jirani ili kuunda Federation au Union kubwa, kuna viongozi kama Maalim Seif wanataka Zanzibar yao wenyewe. Kama Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere alivyosema, mwishoni watataka Pemba yao, na wengine Unguja yao.

Hivi karibuni, East African Community ya Tanzania, Kenya na Uganda walikaribisha Rwanda na Burundi; na mchakato unaendelea kuimarisha soko la pamoja na huduma za pamoja; papo hapo kujaribu kukaribisha D.R.C., Zambia, Malawi na Msumbiji. Sasa huyu Seif alikuwa wapi asipinge, kama anataka kanchi kake ka Zanzibar kawe nchi pekee inayojitegemea?

Large countries with huge populations offer markets which can attract capital for the proper exploitation of natural resources to provide emplyment for the people. The larger the country, the better. Indeed if tiny countries' delegates at the U.N. where Seif wants to go to represent Pemba, start talking, most delegates walk out for smoking, coffee or to prepare their statements. They have no influence and make no impact.

Hakuna hata nchi moja katika hizo ulizozitaja zitakuwa tayari kupoteza Mamlaka ya nchi zao (maamuzi) . Muungano ambao unawafanya wengine wawaamlie wengine kwasababu ambazo wanazijua wao,huo sio Muungano wa kweli.

Nia ya Tanganyika haikuwa Muungano na Zanzibar, bali kuipokonya Zanzibar mamlaka yake na mwisho wake iwe ka-mkoa wa Tanganyika. Kwahili bwana Mtei ,hatutakubali sio kizazi hichi.
 
Huyu Maalim Seif Hamad alikwisha Apa ya kwamba ni lazima atakuwa rais wa Zanzibar hivyo ndoto yake bado inaendelea na tusimshangae sana - Ambition, Ambition, ambition - it's all about him, hivyo inabidi tumwelewe ya kwamba swala sio Wazanzibar isipokuwa yeye kapanda pipa hadi NY na kasimama UN maana Mwinyi alituwakilisha hiyo haihesabiki, Kuna Mawaziri na Manaibu mawaziri kutoka Zanzibar ktk wizara za Jamhuri kutwa wanaoenda nje kila siku kuwakilisha Tanzania hawa pia hawahesabiki isipokuwa pale yeye Maalim Seif atakapo pokelewa kwa ving'ora na vifijo ndio ataiona Zanzibar huru..

Kumuandama nyuki mmoja katika sega ,ni kupoteza muda wako bure. Maalim Seif anatumia uhuru wake wa ki-demokrasia kupigania Zanzibar huru...Kama yeye tupo wengi sana na tutaendelea kudai mpaka kieleweke.

Nyakati za ukoloni mambo leo zimekwisha...
 
Kumuandama nyuki mmoja katika sega ,ni kupoteza muda wako bure. Maalim Seif anatumia uhuru wake wa ki-demokrasia kupigania Zanzibar huru...Kama yeye tupo wengi sana na tutaendelea kudai mpaka kieleweke.

Nyakati za ukoloni mambo leo zimekwisha...
Simuandami nyuki mmoja isipokuwa Malikia wa nyuki, sielewi wewe wamwitaje?. Na pamoja na yote nyuki siku zote kwa nguvu zao hujenga mzinga, lakini wanaokula asili sii nyuki mkuu wangu, fikira hilo nalo neno!. Kuwa kwenu nyuki wengi haikatazwi isipokuwa tunao wazungumzia sisi ni hawa wanao chonga mzinga. nadhani hata Mada hii inasema Maalim Seif asema...

Binafsi yangu nilisha sema siku nyingi sana ya kwamba Uhuru wa Zanzibbar sio wa ile bendera ya Sultan wala nyimbo za sultan Jamheed isipokuwa WATU wake waliokombolewa ktk Mapinduzi ya mwaka 1964, na maadam hawa ndio wenye haki ya urithi wa nchi hiyo ndio pekee wanaoweza kutaka uhuru wao sio ule wa bendera vya Sultan wala mipaka..Na tutaweza tu kuwajua kupitia referundum na sio maneno ya Jussa au Maalim Seif wachonga mizinga..
 
laiti mngeweka mazingira rahisi kama unavyosema mbona zamani muungano usingekuwepo. Mnau;inda kwa magego na nguvu zote. Rais wa nchi moja kuondolewa urais na kuwekwa chini ya ulinzi kwa kuukataa muundo huu, unazani ingekua mnataka kirahisi hicho si mngemruhusu akarudi zanzibar na mkawauliza wazanzibari wenyewe wanasemaje?

Mkaweka sheria kali hata muungano usisemwe ukisema muungano utajuta. Majeshi yakachanganywa.. Security ya zanzibar ikauliwa na kuachwa ya muungano ili kijulikane kila kitendekacho zenji. Mmetungangania halafu mudai tuondoke
Hivi ina ingia akilini kwamba Makamu wa kwanza wa rais anakwenda jukwaani kusema tunataka Zanzibar yetu, huku rais wake ambaye wanakutana kila siku asubuhi akiamini katika Tanzania huru?

Hivi inaingia akilini kwamba Maalim Seif hajui njia sahihi za kufuata zaidi ya kelele za majukwaani na kuunda vikundi vya kufanya fujo?
Ina maana Maalim na Jusa hawajui kwamba sheria zinawaruhusu kuanzisha mchakato wa referendum? mbona iliwezekana kwa katiba mpya ya Znz? Kama serikali ya JMT ndio kikwazo, kwanini hawasemi wazi wazi, kwanini wasiseme wewe Kikwete na CCM yako, mnatuwekea mizengewe tusiwe na Zanzibar huru?

Siku zote ukweli humuacha mtu huru.........huyu maalim anakuwa mnafiki wa kurusha maneno aangalie nani ata react.
Unakula ubuyu huku unalalmika huupendi mbuyu? inawezekana kweli?
 
Tatizo la ZNZ si uwepo wa Tanganyika ni Zanzibar huru!
Usichanganye vitu, Tanganyika ikirudi haina maana matatizo ya ZNZ yataisha.Nimekujibu katika mada yako.
Next time jikite katika mada, kutafuta namna ya kumtaja Nyerere ni udhaifu wa hoja.

Nyerere hayupo madarakani miaka 30 na kafariki miaka 14, nchi ipo na itakuwepo! Jukumu la kutafuta suluhu ya nchi halipo kwa marehemu bali watu wenye kutumia vichwa, wenye kufikiri kwa wakati na si kutafuta mchawi.

JF ni chombo huru, anzisha mada juu ya Nyerere utapata wachangiaji.

Nguruvi3.

Unarudi kule kule kwa kufikiri kuwa Nyerere hakuwa na makosa wala hakutenda makosa. Kumbuka kuwa hata mwenyewe katika moja yya hotba zake aliwahi kukiri kuwa yeye ni mwan'Adam na alifanya makosa ya kibin'Adam kama wanavyofanya wan'Adamu wengine.

Kumbuka kuwa Kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika kunaweza kuwa chachu kubwa SIO TU ya kupunguza manung,uniko ya wananchi wa nchi hizo mbili LAKIN PIA inaweza kuwa chache ya kupunguza Kero za Muungano wenu na hivyo kuuimarisha au hata kuharakisha kuuvunja kama mtaujadili vibaya.

Kumbuka kuwa wakti wa harakati za Pili za kuanzishwa kwa Serikali ya Tanganyika kulikofanywa na wabunge 55 wa bunge la JMTz, Nyerere hakuwa madarakani kabisa sio Tu ya katika Serikali bali hata kwenye Chama chake.

Usiwe na khofu kujadili jambo kuwa huru kujadili HOJA .

Kumbuka kuwa hapa hatumjadili mtu bali kinachojadiliwa ni mustakabali wa nchi zenu mbili na mvungano wenu.

 
images

Mmmm, Mkataba huo
 
Mbona tumewapa kila njia ya kuweza kupata Zanzibar huru; tunachowaambia ni kuwa hatutaki muungano wa mkataba. Watoke kwanza wakishatoka (watoke kabisa na kutangaza kuwa huru) halafu waone kama tutaitisha kura ya maoni Tanganyika ya kujua kama tunataka muungano wa mkataba.

Sio wznz wote wanaotaka Muungano wa mkataba , na sio watanagnyika wote wanaotaka Muungano huu uendelee kama ulivyo. Katika kila upande wa Muungano kuna makundi yanayopingana kuhusu Muungano. Wakati umefika wa kuwa na Kura ya Maoni kuhusu Muungano. Tuulizwe kama tanataka Muungano ? na kama ndio ,wa aina gani ? Lakini sio huu tulionao hivi sasa , kwasababu unaelekea kutuletea majanga yakujitakia wenyewe.
 
zamani hio ingeliwezekana sio leo. Na nnakuambia watu wa muungano wanajua kishanuka,

kwa kweli wazanzibari kwa sasa wanadai nchi yao, huyu seif unaweza kumwita just kapima upepo tu ili asichushe lkn kwa sasa wazanzibari wameamua kuachana na cuf na ccm. Kuna moving ya nguvu wanaojua siasa wanajua nn kiko kule.

Kule ni kimoja tu watu wanataka nchi yao tena yenye mamlaka kamili. Wamechoka kupigwa hadithi. Ss na nyny ndugu zetu wadamu udugu wetu haukuletwa na muungano.

Kama hujui huyo sultan wa zanzibar basi ukoo wake unahusu tanganyika, mama zake ni wana kindaki ndaki wa tanganyika. Salim ahmed salim mama yake mmanyema kama hujui ni mtanganyika. Mwinyi. Jumbe, moyo na wengineo wana asili ya tanganyika hata mm niandikie nna asili pia ya tanganyika. Ila hii haiondoi haki yetu ya kudai nchi yetu zanzibar

udugu wetu wa damu utabakia hata muungano ukiwa haupo kama ilivyokua zamani
Mtu wa Pwani,

..sasa huu undugu utabaki vipi wakati kuna washabiki wa UAMSHO wanatamka waziwazi kwamba Watanganyika wanapeleka UKIMWI, madawa ya kulevya, ujambazi, popobawa, umalaya, ushoga, na mambo mengi mabaya??

..tena wanasema hivyo mchana kweupe, na wale Mashekhe viongozi hawafanyi juhudi zozote zile kuwaweka sawa.

..tatizo siyo Zanzibar kudai kutoka ktk muungano, tatizo ni CHUKI inayopandikizwa dhidi ya Watanganyika. Hivi ni lazima kujenga CHUKI ili kuweza kuvunja muungano kati ya Tanganyika na Zanzibar??

NB:

..hata huku Tanganyika, kabla ya muungano, na wakati tunakua, kulikuwa hakuna ukimwi,udokozi,ujambazi, madawa ya kulevya, etc etc.

..je, unadhani ni sahihi kwa wa-Tanganyika kudai kwamba mambo yote hayo mabaya yamesababishwa na muungano, na tumeletewa na wa-Zanzibari??
 
Last edited by a moderator:
I'm Ordinary Tanganyikan,Sitaki kuusikia huu muungano hata kidogo,Hakuna faida zaidi ya mikelele tu kila kukicha!,Let them Go for good,They're busy beaking every now n' then!
 
Back
Top Bottom